Topic

Uandishi

Estimated reading: 5 minutes 792 views Contributors
Don't Miss Out! Join Darasa Huru

Get instant educational updates, notes, books, and alerts straight to your phone.

Insha za Hoja

Muundo wa Insha za Hoja

Kichwa cha Insha:
Kichwa cha insha hudokeza kile ulichokijadili katika insha yako. Kwa mfano: “Madhara ya Matumizi ya Madawa ya Kulevya”.

Utangulizi:
Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako.

Kiini cha Insha:
Katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha yako. Maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.

Hitimisho:
Hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichohadiliwa katika insha.

Barua Rasmi

Dhima ya Barua Rasmi

Barua rasmi ni barua zinazohusu mambo rasmi ya kiofisi. Dhima za barua rasmi ni kutoa taarifa, kuomba kazi au huduma, kuagiza vitu na kutoa mwaliko kwa mfano kwa kiongozi fulani wa nchi, kutoa malalamiko na kuweka kumbukumbu au marejeo.

Muundo wa Barua Rasmi

Anwani ya Mwandishi:
Huwekwa juu kabisa na huwa katika upande wa kulia wa karatasi.

Tarehe ya Barua:
Tarehe huandikwa chini ya anwani ya mwandishi.

Anwani ya Mpokeaji:
Anwani ya anayeandikiwa huwa katika upande wa kushoto wa karatasi, na huwekwa mstari mmoja chini ya tarehe.

Read Also:

Salamu:
Chini ya anwani ya mpokeaji, barua huanza kwa kumrejelea mpokeaji kama bwana au bi. Ni makosa kumsalimia mpokeaji wa barua rasmi au kumwuliza hali yake.

  • Ndugu Bwana Meshaki, => Taja jina lake ikiwa mnajuana na unayemwandikia.
  • Kwa Bw/Bi, => Ikiwa humjui mpokeaji wa barua, tumia bw/bi.

Mada:
Kichwa cha barua rasmi huja pindi tu baada ya salamu. Hutangulizwa na maneno kama vile YAH:(yahusu). Ni sharti kichwa kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe mstari. Kichwa kinapaswa kuwa kifupi na kinachoelezea mada ya barua kiukamilifu.

Utangulizi:
Hukaa chini kidogo ya mada ya barua. Haya ni maelezo mafupi yasiyozidi aya moja ambayo huelezea kusudi kuu la barua kama kidokezo.

Ujumbe:
Ujumbe wa barua rasmi lazima uwe mfupi na unaotumia lugha rasmi.

Tamati:
Mwandishi humalizia kwa maneno ya hitimisho kama vile: Wako mwaminifu, [jina], Sahihi.

Simu ya Maandishi

Dhima ya Simu ya Maandishi

Simu za maandishi ni aina ya barua fupi ambazo husafirishwa kwa haraka sana kuliko barua za kawaida. Simu hizo huandikwa kwenye fomu maalumu ambazo hutolewa na shirika la posta. Simu za maandishi hujulikana kama telegram.

Kwa kawaida simu za maandishi hutumika kutuma ujumbe wa dharura. Kuandika simu za maandishi ni njia ya haraka ya kufikisha ujumbe kwa sababu, baada ya kuandika simu yako ujumbe humfikia huyo unayemtumia katika muda usiozidi siku tatu. Gharama za simu za maandishi hutozwa kulingana na idadi ya maneno yaliyotumika. Kwa hiyo ujumbe unaotumwa huandikwa kwa maneno machache ili kuepuka kutozwa gharama kubwa.

Mfano wa Simu ya Maandishi:

MUSA KINGAMBE SLP 5299 DSM
NJOO HARAKA
DADA MGONJWA LINGIDO

Muundo wa Simu za Maandishi

Muundo wa kuandika simu za maandishi una mambo yafuatayo ya kuzingatia:

  • Anwani ya mpelekewa taarifa
  • Ujumbe
  • Jina la mwandishi au mtuma simu

Mambo mengine ya kuzingatia ni kuandika maneno yote kwa herufi kubwa ili kurahisisha usomaji na kuandika simu ya maandishi katika karatasi maalumu ambayo hutolewa na posta.

Kadi za Mialiko

Muundo wa Kadi ya Mialiko

Mambo muhimu yanayotakiwa kuonyeshwa katika kadi ya mwaliko:

  • Jina la mwandishi au mwalikaji
  • Jina la mwalikwa, ni muhimu kuandika cheo chake kama vile: Profesa, Bi., Bw., Bw&Bi n.k.
  • Lengo la mwaliko
  • Mahali pa kufanyika shughuli
  • Tarehe ya mwaliko
  • Wakati wa shughuli
  • Jina na anwani ya mtu atakayepelekewa majibu

Mialiko huweza kuandikwa kwa namna mbili yaani kama barua au kadi. Jina la mwalikwa katika kadi ya mwaliko hutakiwa kuanza na maneno ya heshima kama vile Bwana…, Bi…, au Ndugu… Ikiwa waalikwa ni mume na mke kadi itaanza na Bwana na Bibi.

Mfano wa Kadi ya Mwaliko

Familia ya Manyama na Joseph
Wanapenda kukualika/kuwaalika Profesa/Dkt/Shekhe/Padri/Bi/Bw/Bw&Bi……… kwenye harusi ya kijana wao mpendwa Benny Joseph itakayofanyika huko Kiabakari katika ukumbi wa Simba siku ya Jumapili tarehe 9/12/2016 sasa 8.00 mchana hadi saa 3.00 usiku

Kufika kwako ndio mafanikio ya sherehe hii.

Majibu kwa (wasiofika tu):
Emmanuel Joseph
Simu: 0786 67 54 62

Uandishi wa Dayalojia

Dhana ya Dayalojia

Dayalojia ni mazungumzo au majibizano baina ya watu wawili au zaidi wanaozungumza kwa kupokezana. Kama zilivyo kazi nyingine za utungaji, dayalojia inaweza kuwasilishwa kwa njia ya mazungumzo au maandishi.

Katika kutunga dayalojia, mtunzi hana budi kujifanya kama mhusika katika dayalojia hiyo. Kwanza, anapaswa kutafakari kwa makini mada anayokusudia kuandikia dayalojia, kutayarisha na kupanga mawazo kimantiki na kwa mtiririko na kufikiria wahusika na kuwapangia majukumu kulingana na matendo yao. Kwa mfano, kama mhusika ni mkulima, lugha anayopewa, vifaa anavyosemekana kuvitumia na mandhari aliyomo ni lazima vifanane na hali ya mkulima halisi.

Mambo ya Kuzingatia Katika Dayalojia

  • Kutoa maelezo ya ufafanuzi katika mabano ili kumfahamisha msomaji
  • Kuwa na mazungumzo ya mkato na yasiyozidiana sana kati ya wahusika. Mhusika mmoja asitawale mazungumzo kupita wengine.
  • Kutumia vihisishi ili kufanya dayalojia iwe ya kusisimua
  • Pawepo mwingiliano wa mazungumzo ya wahusika na kudakia maneno ili dayalojia iwe na uhalisia.

Mfano wa Dayalojia

Wambura: (Anaonekana mwenye furaha, anamwita rafiki yake, Anna) Wow, Anna! Tumekutana tena, siamini macho yangu! (wanakumbatiana wote wakiwa na nyuso za furaha).

Anna: (Anatabasamu huku ameshikilia mkono wa kulia wa Wambura, anaonesha shauku kuu) Wambura! Bado unanikumbuka? Nina furaha sana kwa kweli, ni muda mrefu sana.

Wambura: (Anachekelea) Aaaah, nahisi kama naota, Anna. Siamini kama nimekutana na wewe leo hii ni muda mrefu sana, nimefurahi kwa kweli.

Anna: (Anachekelea)

Wambura: Mbona unachekelea tu…

Test Your Knowledge

Click below to generate a short, interactive 5-question quiz based on this lesson.

Don't Miss Out! Join Darasa Huru

Get instant educational updates, notes, books, and alerts straight to your phone.

Share this Doc

Uandishi

Or copy link

CONTENTS

Form One Ngoma TIE Book PDF Free Download

If you have been trying to track down an authentic and reliable digital copy of

Form One Netball Performance TIE Book PDF

Are you trying to track down a dependable digital copy of the Form One Netball P

Form One Music Performance TIE Book PDF Download

Trying to track down the official Form One Music Performance TIE book PDF? Findi

Form One Music And Sound Technology TIE Book PDF Download

If you are looking for the official Form One Music And Sound Technology TIE book

Form One Motorcycle Mechanics TIE Book PDF Download

Are you looking for the official Form One Motorcycle Mechanics TIE book PDF for

Form One Motor Vehicle Mechanics TIE Book PDF Download

Trying to find the official Form One Motor Vehicle Mechanics TIE book PDF for yo

Form One Civil Draughting TIE Book PDF Free Download

Are you trying to track down the official Form One Civil Draughting TIE book PDF

Form One Auto Body Repair TIE Book PDF Free Download

Here’s the Form One Auto Body Repair TIE book PDF for the vocational stream. Pub

Form One Art and Design TIE Book PDF Free Download – Vocational Stream

Looking for the official Form One Art and Design TIE book PDF for the vocational

Form One Animal Health And Production TIE Book PDF

Looking for the official Form One Animal Health And Production TIE book PDF for

Form One Agro Mechanics Tie Book PDF Download

Looking for the official Form One Agro Mechanics TIE book PDF for the vocational

Mathematics Syllabus Form 5-6 Free Download

MATHEMATICS SYLLABUS FOR ADVANCED SECONDARY EDUCATION FORM V-VI View and Downloa

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel