Topic

Ngeli Za Nomino

Estimated reading: 3 minutes 2968 views Contributors

Kuzielewa ya Ngeli na Upatanishi wa Kisarufi katika Sentensi

Upatanishi wa Kisarufi katika Sentensi

Ngeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana.

Mfano 1

  1. Maji yakimwagika hayazoleki
  2. Mayai yaliyooza yananuka sana
  3. Yai lililooza linanuka sana
  4. Maji liliomwagika halizoleki

Katika mifano hii, tunaona kwamba sentensi (1), (2), na (3) ziko sahihi, wakati sentensi (4) si sahihi. Hii ni kwa sababu imekiuka upatanisho wa kisarufi. Sentensi ya kwanza ipo katika ngeli ya YA-YA, na sentensi ya pili na ya tatu zipo katika ngeli ya LI-YA. Sentensi ya nne si sahihi kwa sababu nomino “maji” haina wingi, hivyo haiwezi kuingia katika ngeli ya LI-YA. Kwa msingi huu, ngeli za nomino huzingatia sana upatanisho wa kisarufi.

Jedwali la Ngeli za Nomino kwa Misingi ya Upatanisho wa Kisarufi

NGELIUFAFANUZIMIFANO
A-WANgeli hii inahusisha majina ya viumbe hai kama vile wanyama, watu, wadudu, ndege n.kSungura mjanja ameumia
Sungura wajanja wameumia
Mkuu anawasili
LI-YAMajina yenye kiambisha awali li- katika umoja na ya- katika wingi huingia katika ngeli hiiJambia la babu limepotea
Majambia ya babu yamepatikana
KI-VINi ngeli ya majina ya vitu visivyo hai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Pia ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo k.v, kijito, kilimaChakula kimekwisha
Vyakula vimekwisha
Kijito kimekauka
Vijito vimekauka
U-IHuwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M- (umoja) na MI- (wingi). Pia majina ya baadhi ya viungo vya mwili huingia humu, kwa mfano mkono, mguu, mkia n.kMlima umeporomoka
Milima imeporomoka
Mkono umevunjika
Mikono imevunjika
Mto huu una mamba wengi
Mito hii ina mamba wengi
U-ZIHurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti /u/ k.v ukuta-kuta. Majina ya silabi mbili huongezewa /ny/ katika wingi. k.v ufa – nyufaUkuta umebomoka
Kuta zimebomoka
Wimbo huu unavutia
Nyimbo hizi zinavutia
Ufa umeonekana
Nyufa zimeonekana
I-ZIHutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (wingi).Nyumba imejengwa
Nyumba zimejengwa
Salam imefika
Salam zimefika
U-YANgeli hii inajumuisha nomino ambazo zina kiambishi awali u- katika umoja na ma- katika wingi.Ukuu umekuponza
Makuu yamekuponza
Unyoya unapepea
Manyoya yanapepea
KUMajina yanayotokana na vitenzi yanayoanza na ku- (vitenzi-jina)Kusoma kwako kumekusaidia
Kuchelewa kumemponza
PA/MU/KU-Huonesha mahaliAmekaa pale palipo na wadudu wengi
Amelala mule mulimojaa siafu
Amepita kule mbali

Matumizi ya Ngeli

Baadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:

  1. Kuweka Majina katika Makundi: Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.
  2. Umoja na Wingi: Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.
  3. Upatanishi wa Kisarufi: Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.
  4. Uhusiano wa Lugha: Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.

Kwa kuzingatia upatanishi wa kisarufi, sentensi zinakuwa na muundo sahihi wa kisarufi ambao hufanya lugha kuwa ya kueleweka zaidi na ya kuvutia.

Test Your Knowledge

Click below to generate a short, interactive 5-question quiz based on this lesson.

No comments yet — be the first to share your thoughts.

Leave a Comment

Share this Doc

Ngeli Za Nomino

Or copy link

CONTENTS

Kiswahili Syllabus F5-F6

MUHTASARI WA KISWAHILI ELIMU YA SEKONDARI KIDATO CHA V–VI Kiswahili Syllabus F5-

Kiswahili Syllabus Fasihi Ya Kiswahili F5-F6

MUHTASARI WA FASIHI YA KISWAHILI ELIMU YA SEKONDARI KIDATO CHA V– VI Kiswahili S

Kiswahili Syllabus Fasihi Ya Kiswahili F3-F4

MUHTASARI WA FASIHI YA KISWAHILI ELIMU YA SEKONDARI KIDATO CHA III–IV Kiswahili

Bookkeeping Form Four TIE Book PDF – Free Download

Form Four bookkeeping is exam-year bookkeeping. Everything students have built u

Bookkeeping Form Three TIE Book PDF – Free Download

Ask a Form Three student what bookkeeping is for, and most will say “passing the

Bookkeeping Form Two TIE Book PDF Download-Get Free New Book

Stepping into your second year of secondary commercial studies brings a shift to

Physics Form Six TIE Book PDF – Free Download

Physics Form Six TIE Book PDF Form Six is the finish line of Advanced Level phys

Physics Form Five TIE Book PDF – Free Download (Official A-Level 5 Textbook)

Physics Form Five TIE Book PDF Form Five is where physics stops being descriptiv

Physics Form Six Notes, Books and New Syllabus PDF

Studying Physics form six requires access to reliable textbooks and structured r

Physics Form Five Notes and books – New Tanzania Syllabus (TIE)

Looking for reliable Physics Form Five notes and books aligned with the New Tanz

Mathematics Form Five Teacher’s Guide TIE Book PDF Download – New Syllabus

Delivering high-quality Advanced Level instruction requires structured lesson pl

Mathematics Form Five and Form Six BAM TIE Book PDF Download -New Syllabus

Navigating non-mathematical Advanced Level subject combinations still requires a

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel