Topic

Usimulizi

Estimated reading: 3 minutes 738 views Contributors

Summary: Usimulizi ni jumla ya maelezo yanayotolewa na mtu au watu wengi kuhusu tukio fulani. Katika mada hii utajifunza juu ya taratibu za usimulizi wa matukio kupitia njia kuu mbili za masimulizi, yaani kwa njia ya mdomo au kwa njia ya maandishi. Pia utaweza kujifunza juu ya mbinu mbalimbali za usimulizi.

Usimulizi wa Hadithi

Njia za Usimulizi wa Hadithi

Elezea njia za usimulizi wa hadithi

Usimulizi hufanyika kwa njia kuu mbili yaani kwa njia ya maandishi na kwa njia ya masimulizi ya mdomo. Kila njia hutegemea namna msimuliaji anavyoweza kuwasiliana na msikilizaji. Ikiwa msimuliaji na msikilizaji hawakukaribiana, njia ambayo itatumika ni ile ya maandishi. Kwa mfano kama utahitaji kumweleza mtu aliyembali kuhusu tukio fulani la kusisimua utalazimika kutumia maandishi, yaani utatumia njia ya kumwandikia barua.

Lakini kama unamsimulia mtu ambaye yupo karibu nawe, utatumia njia ya mazungumzo ya ana kwa ana.

Usimulizi wa Habari

Taratibu za Usimulizi wa Matukio

Fafanua taratibu za usimulizi wa matukio

Usimulizi wa matukio dhamira yake ni kumweleza mtu au watu tukio ambalo wao hawakulishuhudia. Hivyo katika usimulizi msimuliaji hutakiwa kutoa maelezo muhimu ambayo yatawawezesha watu hao kulielewa tukio linalosimuliwa sawasawa na huyo anayeshuhudia.

Mambo muhimu ya kutaja katika usimulizi wa matukio ni pamoja na haya yafuatayo:

  1. Aina ya tukio – msimuliaji atatakiwa kubainisha katika maelezo yake aina ya tukio. Kwa mfano, kama ni harusi, ubatizo, ajali ya barabarani au mkutano.
  2. Mahali pa tukio – ili msimuliaji aweze kuielewa habari inayosimuliwa, ni lazima kumwelewesha ni mahali gani tukio hilo limetokea. Kwa mfano, kama ni mjini inafaa kutaja hata jina la mtaa.
  3. Wakati – katika usimulizi ni muhimu pia kutaja muda ambao tukio limetendeka kama ni asubuhi, mchana au jioni bila kusahau kutaja muda halisi yaani ilikuwa saa ngapi.
  4. Wahusika wa tukio – ni muhimu kutaja tukio limehusisha watu gani, wingi wao, jinsia yao, umri wao n.k.
  5. Chanzo cha tukio – kila tukio lina chanzo chake hivyo ni muhimu kutajwa katika usimulizi.
  6. Athari za tukio – athari za tukio nazo ni sharti zibainishwe. Kama ni ajali, je watu wangapi wameumia; wangapi wamepoteza maisha n.k.
  7. Hatima ya tukio – msimuliaji katika usimulizi wake ni lazima abainishe baada ya tukio kutokea na kushughulikiwa hatima yake ilikuwaje. Kwa mfano, kama tukio ni ajali ya barabarani hatima yake inaweza kuwa majeruhi kupelekwa hospitalini na dereva aliyehusika kukamatwa.

Kwa hiyo misingi hii ya usimulizi hufanya usimulizi wa tukio kuwa na sehemu kuu tatu:

  • Utangulizi – sehemu hii huwa na maelezo tu ya utangulizi ambayo hulenga kuvuta hisia na umakini wa msikilizaji au wasikilizaji. Kwa kawaida utangulizi wa tukio huwa ni maneno machache kiasi yasiyozidi aya moja.
  • Kiini – kiini cha usimulizi huelezea tukio halisi kuanzia chanzo chake, wahusika, muda, mahali na athari za tukio.
  • Mwisho – mwisho wa usimulizi ni matokeo yanayoonyesha matokeo ya mwisho ya tukio linalohusika, wakati mwingine matukio haya yanaweza kuambatana na maelezo ya msimuliaji kuhusu mtazamo au maoni yake binafsi juu ya tukio ambalo amesimulia.

Mbinu za usimulizi

Ili habari inayosimuliwa ipate kueleweka vizuri, sharti msimuliaji ajue mbinu za kusimulia katika hali inayovuta hisia za msikilizaji wake.

Baadhi ya mbinu hizo ni uigizi, utumizi wa lugha fasaha inayozingatia lafudhi sahihi ya Kiswahili.

Kwa upande wa uigizi msimuliaji atatakiwa kuigiza mambo muhimu yanayohusiana na tukio ambalo anasimulia. Nayo ni kama vile milio, sauti na matendo.

Kwa upande wa usimulizi ambao unafanyika kwa njia ya maandishi, sharti usimulizi huo uwe na kichwa cha habari. Kichwa cha habari kinatakiwa kuandikwa kwa maneno yasiyozidi matano, yaliyoandikwa kwa herufi kubwa.

Kwa vile usimulizi wa tukio huwa unahusu tukio lililopita, maelezo yake mengi huwa katika wakati uliopita.

Test Your Knowledge

Click below to generate a short, interactive 5-question quiz based on this lesson.

Share this Doc

Usimulizi

Or copy link

CONTENTS

Kiswahili Syllabus F5-F6

MUHTASARI WA KISWAHILI ELIMU YA SEKONDARI KIDATO CHA V–VI Kiswahili Syllabus F5-

Kiswahili Syllabus Fasihi Ya Kiswahili F5-F6

MUHTASARI WA FASIHI YA KISWAHILI ELIMU YA SEKONDARI KIDATO CHA V– VI Kiswahili S

Kiswahili Syllabus Fasihi Ya Kiswahili F3-F4

MUHTASARI WA FASIHI YA KISWAHILI ELIMU YA SEKONDARI KIDATO CHA III–IV Kiswahili

Bookkeeping Form Four TIE Book PDF – Free Download

Form Four bookkeeping is exam-year bookkeeping. Everything students have built u

Bookkeeping Form Three TIE Book PDF – Free Download

Ask a Form Three student what bookkeeping is for, and most will say “passing the

Bookkeeping Form Two TIE Book PDF Download-Get Free New Book

Stepping into your second year of secondary commercial studies brings a shift to

Physics Form Six TIE Book PDF – Free Download

Physics Form Six TIE Book PDF Form Six is the finish line of Advanced Level phys

Physics Form Five TIE Book PDF – Free Download (Official A-Level 5 Textbook)

Physics Form Five TIE Book PDF Form Five is where physics stops being descriptiv

Physics Form Six Notes, Books and New Syllabus PDF

Studying Physics form six requires access to reliable textbooks and structured r

Physics Form Five Notes and books – New Tanzania Syllabus (TIE)

Looking for reliable Physics Form Five notes and books aligned with the New Tanz

Mathematics Form Five Teacher’s Guide TIE Book PDF Download – New Syllabus

Delivering high-quality Advanced Level instruction requires structured lesson pl

Mathematics Form Five and Form Six BAM TIE Book PDF Download -New Syllabus

Navigating non-mathematical Advanced Level subject combinations still requires a

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel