Topic Uundaji Wa Maneno Estimated reading: 4 minutes 54 views Kutumia UambishajiKubainisha Mofimu katika ManenoBainisha mofimu katika manenoUambishaji wa maneno ni kitendo cha kupata maneno kwa kubandika Mofimu kwenye kiini cha neno, uambishaji kutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini pig- unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji, amepigika nk.Mofimu zinazobadilika kwenye kiini cha neno huitwa Viambishi.Katika lugha ya Kiswahili viambishi hutokea kabla na baada ya kiini cha neno.MfanoWanapendana = Wa-na-pendan-a kiini cha neno ni-pend-.Mofimu zilizobadilisha baada ya kiini –an-na-a viambishi vinavyotokea kabla ya kiini cha neno huitwa viambisha awali au tangulizi. Viambisha vinavyotokea baada ya kiini cha neno huitwa viambishi tamati au fuatishi.Example 1Angalia mifano ifuatayo:NenoViambisha AwaliKiiniViambisha TamatiUnapendeleau-na--penda-el-e-aWaliongozanawa-li--ongoz-an-aAnalimaa-na--lim--aanayeiimbishaa-na-ye-imb--ish-aDhima za MofimuBainisha dhima za mofimuBaadhi ya dhima za uambishaji ni kama ifuatavyo:Kuonyesha upatanisho wa usanifu maana ya maneno yanayozalishwa kutofautiana katika msingi wa kusanifu tu, lakini uhusiano wa maneno hayo hutokana na kiini au mzizi wake uleule.Mfano;Fundisha kiini chake ni fund. Unaweza kuzalisha maneno mengine kwa kutumia mzizi/kiini kilichopo kama vile fundishana, mafundisho, mfundishaji, fundishwa, fundishana.Uambishaji huonyesha nafsiUambashaji huonyesha njeo (muda)Uambishaji huonyesha urejeshiUambishaji huonyesha ukanushiUambishaji huonyesha hali mbalimbali za kitenziVitenzi vikiambishwa huweza kujenga/kuunda/kuzalisha vitenzi vingine au nomino.Example 2MfanoVitenziKiiniNominoVitenziCheza-chez-Mchezaji, mchezowanacheza/atamchezeaPiga-pig-Mpigaji, Mpiganajiwatanipiga, aliyempiga/wanaompigaUambishaji hutumika kuzalisha viwakilishi na vielezi.Neno (Kiwakilishi)KiiniKieleziHuyu, HuyoHuHumu, humoWangu, wako, wakewaHii, hizo, hikihiViambishi awali vina dhima ya kudokeza nafsi, njia, idadi urejeshi na ukanushi.Mfano: HawakulimaHa-, kiambishi cha ukanushiKu-, kiambishi njeo/wakatiViambishi tamati vina dhima mbalimbali hudokeza hali ya utendekaji, ukamilishaji au kimalizio cha neno na kauli za matendo kama vile kutendwa, kutendewa,kutendeka nk.Dhima:Ukanusho, kutendeana, agizo na mtendwa, ukamilisho, usababishi.Example 3MfanoNenoViambishi TamatiAnapiga-aWanapigana-anAsipigwe-wAmempigisha-ish-Viambishi tamati vina dhima ya kutambulishwa mapema/nomino zilizoundwa kutokana na vitenzi.NenoKiiniViambishi TamatiPigapig--oMchezochez--oMtembezitembe--z-iMfiwa-fi--us-aKutumia MnyumbulikoMazingira yanayosababisha Mahitaji ya Maneno MapyaElezea mazingira yanayosababisha mahitaji ya maneno mapyaMnyumbulisho ni neno linalotokana na neno nyumbua. Kunyumbua kitu ni kuvuta, kuongeza urefu wa kitu hicho.Kunyumbua katika lugha ya Kiswahili ni kuongeza vinyumbulishi katika katika kiini ili kupata msamiati mpya. Hivyo basi, mnyumbulisho ni njia mojawapo na inasaidia kuunda maneno kwa njia ya kunyumbulisha.Viambishi vinapochukuliwa katika kiini cha neno, basi neno hilo huwa limenyumbulishwa. Kwa mfano neno lima kiini chake lim- huweza kunyumbulishwa na kupata maneno mengine mpya, kama lim-ishwa, lim-ia, lim-w-a.Pia maneno ya mnyumbulisho yanaweza kuundwa kwa kuongeza viambishi kwenye shina, kwa mfano:NenoKiiniShinaManeno ya MnyumbulikoElekeaelekelekaElekeana, elekea, elekwa, elekeshaShikishanashikshikishaShikishana, shikisha, shikishaneniKwa ujumla tunawaza kusema kuwa maneno ya kawaida hunyumbulika. Hivyo kiini/mzizi au shina moja huweza kuzalisha maneno mengine mengi ambayo yanatokana na msingi mmoja wa maana.Dhima ya Uambishaji na Mnyambulikoa wa ManenoFafanua dhima ya uambishaji na mnyambulikoa wa manenoDhima ya uambishaji ni kuleta upatanisho wa kisarufi, kuonesha idadi na umoja na wingi katika ngeli za majina, kuonesha njeo na kuonesha urejeshi pamoja na hali mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi kabla ya mzizi wa neno. Aidha dhima ya mnyambuliko ni kuonesha matokeo ya tendo na kuzalisha kauli mbalimbali kwa kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno.Kuunda Maneno mbalimbali kwa kutumia MnyambulikoUnda maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambulikoUundaji wa maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko hufanyika kwa kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno na hivyo kulifanya neno husika liweze kuonesha matokeo mbalimbali ya matendo pamoja na kuzalisha kauli mbalimbali za matendo.Activity 1Unda maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambulikoKutumia Maneno ya Mnyambuliko katika Miktadha mablimbaliTumia maneno ya mnyambuliko katika miktadha mablimbaliManeno ya mnyambuliko hutumika katika miktadha mbalimbali ambapo miktadha hiyo hujitokeza katika kauli mbalimbali za vitenzi. Kauli hizo ni kauli ya kutenda, kauli ya kutendwa, kauli ya kutendewa, kauli ya kutendea, kauli ya kutendeka, kauli ya kutendesha, kauli ya kutendana, na kauli ya kutendama.Activity 2Tumia maneno ya mnyambuliko katika miktadha mbalimbali Next - Topic Matumizi Ya Lugha Katika Miktadha Mablimbali