Comment

Topic

Utungaji Wa Kazi Za Kifasihi

Estimated reading: 5 minutes 112 views

Summary: Kazi za fasihi simulizi hazikutokea tu, zilitungwa. Mtu fulani alikaa na akatunga kazi fulani ambayo inajulikana katika jamii. Katika mada hii utajifunza kanuni mbalimbli zinazohusika na utunzi wa kazi za fasihi simulizi. Pia utapata fursa ya kujifunza jinsi ya kutunga kazi mbalimbali za fasihi simulizi kama vile ngonjera, methali , nahau, vitendawili na kazi nyingine. Utajifunza pia kanuni zinazoongoza utunzi wa kila kazi ya fasihi simulizi.

Mashairi

Kanuni za Utungaji wa Mashairi

Milango ya Fahamu

Uandishi wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu kwa uangalifu. Milango ya fahamu mitano ni pamoja na:

  • Kuona: Mhusika unayemfikiria kichwani mwako unamwonaje? Umbo lake ni la kuvutia au kuchusha? Je, macho yake ni ya golori au la? Ni makubwa au madogo? Je, ni mlemavu wa macho?
  • Kunusa: Pua zako zinakufanya usikie harufu gani? Je, ni harufu mbaya au nzuri? Je, ni uvundo au marashi? Je, mhusika wako ananuka kikwapa au uturi? Je, ananuka mdomo?
  • Kuhisi: Je, unapokaa karibu naye unajihisi nini? Je, unapata mhemko wowote au huhisi chochote? Je, akikupapasa mwilini mwako unajisikia nini? Akikugusa bega unajisikia nini?
  • Kuonja: Je, ukiweka kitu hicho mdomoni unaonjaje – ni chungu au tamu? Je, ina pilipili au masala? Je, kuna chumvi au sukari? Je, kitu hicho kina ukakasi au uchachu?
  • Kusikia: Sauti unayoisikia ikoje? Inamtoa nyoka pangoni? Inakufanya ukose usingizi? Je, ni sauti nzuri au mbaya? Ni nyororo au nzito? Kama ni sauti ya muziki – je, iko chini au juu (kelele)?

Uzoefu wa Mwandishi

Uzoefu ni hali ya kukaa au kujishughulisha na jambo au kitu kwa muda mrefu. Mwandishi ana uzoefu wa kukabiliana na maisha kwa kiasi gani? Je, ni matatizo gani umekutana nayo katika maisha yako? Je, ni mafanikio gani umekutana nayo? Kwa mfano, katika ajali ya MV Spice (2011) baadhi ya watu waliokolewa na magodoro ya Tanzania kwa sababu yalikuwa na nailoni. Uzoefu wako ukoje?

Uchunguzi/Utafiti

Uchunguzi unapaswa ufanywe na mwandishi ili aweze kuandika jambo au tukio bila kuongopa. Kwa kufanya udanganyifu, mwandishi atapoteza imani yake kwa wasomaji wa kazi zake. Uchunguzi unamwezesha mtunzi kujua jinsi mtu, mnyama, mdudu na kadhalika, anavyotembea, anakulaje, analalaje, anaishije, anachekaje, analiaje, anazaaje, na anahusianaje na wenzane na mazingira yake.

Dhana ya Shairi

Shairi ni kipande cha maandishi kilichopangwa kwa utaratibu katika mistari. Sauti za silabi hufanana zikiwa kati au mwisho mwa mstari. Maandishi hayo yakisomwa huleta ujumbe na hisia fulani ya kimaisha.

Mpango wa maneno ya shairi, ambao huweza kuimbwa, hutoa picha wazi, maana halisi na burudani ya kimuziki. Nyimbo nyingi za makabila zimepangiliwa kishairi ijapokuwa hazikuandikwa.

Mambo Muhimu katika Mashairi

  • Beti: Kifungu kimoja cha shairi ambacho kina uzani sawa.
  • Vina: Mwisho wa mistari ambayo huwa na silabi zenye sauti ileile mwishoni mwa sentensi.
  • Mizani: Idadi zilizo sawa za silabi katika kila mstari, ubeti hadi ubeti.
  • Kituo: Mstari wa mwisho wa ubeti. Kuna vituo vya aina tatu:
  • Kituo cha bahari: Mstari unaotoka mwanzo hadi mwisho bila kubadilika katika kila ubeti.
  • Kituo cha kimalizio: Kituo ambacho mstari wa mwisho maneno yake hubadilika ubeti hadi ubeti.
  • Kituo nusu bahari: Mstari wa mwisho ambao maneno yake nusu hubadilika na nusu hubaki kama ulivyo ubeti hadi ubeti.

Vipengele vya Fani katika Mashairi

  • Jina / Anwani
  • Mandhari
  • Wahusika
  • Muundo: Tathnia, tathlitha, tarbia, tathamisa, sabilia n.k
  • Mtindo: Pindu, msisitizo, beti kubadilishana vina, kurudiwa kipande kizima cha mstari wa mwisho kikiwa ni chanzo cha ubeti unaofuatia.

Vipengele vya Maudhui katika Mashairi

  • Migogoro
  • Ujumbe
  • Falsafa
  • Msimamo
  • Mtazamo
  • Dhamira za mwandishi

Matumizi ya ushairi ni pamoja na: kuomboleza, kubembeleza, kuliwaza, kufundisha, kuburudisha, kukosoa, na kadhalika. Baada ya hapa sasa unaweza kuanza kutunga shairi lako la kwanza.

Kuigiza Ngonjera

Igiza Ngonjera

Katika kuigiza ngonjera, muigizaji hana budi kuzingatia fani yenye kanuni zifuatazo:

  • Mtindo wa mashairi ya kimapokeo
  • Muundo wa mashairi ya kimapokeo wenye mizani, vina, vipande, mishororo, na beti
  • Kuteua mandhari kutegemeana na mada
  • Kuwepo kwa wahusika wawili au zaidi au makundi mawili au zaidi
  • Matumizi ya lugha ya kishairi

Maigizo

Kanuni za Utungaji wa Maigizo

Hatua za Kutunga Maigizo

  1. Kuchagua wazo, tendo, visa au tukio la kuigizwa:
  • Ni lazima jambo hilo liwe na uzito, umuhimu au athari fulani katika jamii. Matukio hubainika kutokana na utafiti. Matukio yanayoweza kuwa kiini cha kutungiwa maigizo ni kama vile matumizi mabaya ya simu za mkononi, mitindo ya mavazi, madhara ya uganga wa kienyeji, madhara ya UKIMWI n.k.
  1. Kuchagua muktadha au mahali pa kutendeka kwa jambo:
  • Muktadha waweza kuwa ofisini, shuleni, kijijini, mjini, barabarani, kwenye daladala n.k.
  1. Kuamua mtindo wa kuwasilisha jambo la kuigizwa:
  • Mtunzi anaweza kutumia fumbo, vichekesho, historia, tanzia n.k. Inashauriwa mtunzi kuchanganya mbinu ili kuongeza mvuto.
  1. Kupanga hoja kuu zinazojenga maudhui ya igizo:
  • Maudhui hujikita katika migogoro au mivutano. Suluhisho la mivutano hupatikana pale migogoro inapofikia kilele. Kwa mfano, jambazi sugu anapokamatwa.
  1. Kuweka mpangilio wa maonyesho:
  • Maonyesho hujumuisha vitendo na hoja zinazokamilisha sehemu inayobeba aina moja au zaidi ya maudhui. Sehemu kadhaa nazo hukaa zikajenga kitendo ambacho hubeba jambo mojawapo muhimu. Katika migawanyo hii yapasa mtunzi atunge kauli na vitendo vinavyoandamana navyo.
  1. Kubuni wahusika na kuweka aina au idadi yao kulingana na matukio:
  • Mtunzi anashauriwa kutumia wahusika wanaohitilafiana. Kwa mfano, wazee, vijana, wanawake, wanaume, wanene, wafupi n.k. Mtunzi akishawateua anaweza kuwatungia kauli na zamu za matendo katika sehemu mbalimbali.
  1. Kuwaumba wahusika na kuamua maleba yao:
  • Uamuzi huu yapasa ufanywe kwa kuzingatia mazingira. Kwa mfano, siku hizi sio lazima wahusika wazee kuvaa ngozi, kutumia mkongojo na kuvuta mtemba.
  1. Urefu wa maigizo:
  • Urefu wa maigizo ni suala la kuamuliwa kutegemea tukio.
  1. Kutunga maelezo kuhusu mandhari:
  • Maumbile ya wahusika na vitendo vyao, ni muhimu kuelezwa katika mabano.
  1. Kuandika maigizo na kuhariri:
  • Ni muhimu kutumia lugha ya kimazungumzo inayovutia, yenye kuleta taharuki na yenye utamu unaoeleza maadili kwa mnato.

Leave a Comment


Share this Doc

Utungaji Wa Kazi Za Kifasihi

Or copy link

CONTENTS

Translation And Interpretation | English Form 5 & 6

Translation is a process by which ideas that are written in one language ar...

Writing Skills | English Form 5 & 6

Are the abilities that allow you to write effectively and concisely. A competent...

Reading Skills | English Form 5 & 6

Reading is the process of going through written information or piece of wor...

Speaking Skills | English Form 5 & 6

What is Speaking? SPEAKING SKILLS: Speaking is simply the act of talking wh...

Listening Skills | English Form 5 & 6

Listening is ability to accurately receive and interpret messages in the communi...

Word Formation | English Form 5 & 6

This is the field or branch of morphology which studies different principles or ...

Introduction To Language | English Form 5 & 6

Language is a symbol system based on pure or arbitrary  conventions…...

Topic

Form Five and Form Six

Ecology

Ecology is the study of the interactions between living things, such as humans, ...

Evolution

EVOLUTION Evolution is  a change in the genetic composition of a population...

Genetics

Genetics is the study of heredity and variationHeredity- is the passage of chara...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel