Topic Usimulizi Estimated reading: 3 minutes 57 views Summary: Usimulizi ni jumla ya maelezo yanayotolewa na mtu au watu wengi kuhusu tukio fulani. Tukio hilo linaweza kutokea katika wakati mfupi uliopita au zamani kidogo.Usimuliaji wa MatukioNjia za Usimulizi wa MatukioUsimulizi hufanyika kwa njia kuu mbili:Njia ya Maandishi:Hii hutumika wakati msimuliaji na msikilizaji hawapo karibu. Kwa mfano, unapotaka kumweleza mtu aliyembali kuhusu tukio fulani la kusisimua, utatumia njia ya kumwandikia barua.Njia ya Masimulizi ya Mdomo:Hii hutumika unaposimulia tukio kwa mtu ambaye yupo karibu nawe, yaani kwa mazungumzo ya ana kwa ana.Taratibu za Usimulizi wa MatukioUsimulizi wa matukio unalenga kumweleza mtu au watu tukio ambalo hawakulishuhudia. Msimuliaji hutakiwa kutoa maelezo muhimu ili watu hao waweze kuelewa tukio linalosimuliwa vizuri.Mambo Muhimu ya Kutaja katika Usimulizi wa Matukio:Aina ya Tukio:Msimuliaji anatakiwa kubainisha aina ya tukio, kwa mfano, harusi, ubatizo, ajali ya barabarani, au mkutano.Mahali pa Tukio:Ni lazima kumwelewesha msikilizaji mahali tukio lilipotokea, kama ni mjini, ni vyema kutaja jina la mtaa.Wakati:Ni muhimu kutaja muda ambao tukio limetendeka, kama ni asubuhi, mchana, au jioni, na muda halisi, kwa mfano saa ngapi.Wahusika wa Tukio:Ni muhimu kutaja watu walioshiriki katika tukio, wingi wao, jinsia yao, umri wao n.k.Chanzo cha Tukio:Kila tukio lina chanzo chake, hivyo ni muhimu kutajwa katika usimulizi.Athari za Tukio:Athari za tukio ni lazima zibainishwe. Kwa mfano, kama ni ajali, je, watu wangapi wameumia? Wangapi wamepoteza maisha?Hatima ya Tukio:Msimuliaji anatakiwa kubainisha matokeo ya tukio. Kwa mfano, kama ni ajali ya barabarani, hatima inaweza kuwa majeruhi kupelekwa hospitalini na dereva kukamatwa.Msingi wa UsimuliziUsimulizi wa tukio una sehemu kuu tatu:Utangulizi:Sehemu hii huwa na maelezo mafupi yanayolenga kuvuta hisia na umakini wa msikilizaji. Utangulizi huwa ni maneno machache yasiyozidi aya moja.Kiini:Hapa ndipo tukio halisi linapoelezwa, kuanzia chanzo chake, wahusika, muda, mahali, na athari za tukio.Mwisho:Hapa kuna matokeo ya mwisho ya tukio linalohusika, na wakati mwingine maelezo ya msimuliaji kuhusu mtazamo au maoni yake binafsi juu ya tukio.Mbinu za UsimuliziIli habari ipate kueleweka vizuri, msimuliaji anatakiwa kutumia mbinu mbalimbali za kusimulia ili kuvuta hisia za msikilizaji.Baadhi ya Mbinu hizo ni:Uigizi:Msimuliaji anatakiwa kuigiza mambo muhimu yanayohusiana na tukio kama vile milio, sauti, na matendo.Lugha Fasaha:Matumizi ya lugha fasaha na inayozingatia lafudhi sahihi ya Kiswahili ni muhimu.Kichwa cha Habari:Kwa usimulizi wa maandishi, lazima kuwe na kichwa cha habari. Kichwa kinatakiwa kuandikwa kwa maneno yasiyozidi matano, yaliyoandikwa kwa herufi kubwa.Kwa vile usimulizi wa tukio unahusu tukio lililopita, maelezo yake mengi huwa katika wakati uliopita.Tagged:kidato cha piliKiswahili Topic - Previous Uandishi Next - Topic Ufahamu