Topic Uandishi Estimated reading: 5 minutes 60 views Insha za HojaMuundo wa Insha za HojaKichwa cha Insha:Kichwa cha insha hudokeza kile ulichokijadili katika insha yako. Kwa mfano: “Madhara ya Matumizi ya Madawa ya Kulevya”.Utangulizi:Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako.Kiini cha Insha:Katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha yako. Maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.Hitimisho:Hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichohadiliwa katika insha.Barua RasmiDhima ya Barua RasmiBarua rasmi ni barua zinazohusu mambo rasmi ya kiofisi. Dhima za barua rasmi ni kutoa taarifa, kuomba kazi au huduma, kuagiza vitu na kutoa mwaliko kwa mfano kwa kiongozi fulani wa nchi, kutoa malalamiko na kuweka kumbukumbu au marejeo.Muundo wa Barua RasmiAnwani ya Mwandishi:Huwekwa juu kabisa na huwa katika upande wa kulia wa karatasi.Tarehe ya Barua:Tarehe huandikwa chini ya anwani ya mwandishi.Anwani ya Mpokeaji:Anwani ya anayeandikiwa huwa katika upande wa kushoto wa karatasi, na huwekwa mstari mmoja chini ya tarehe.Salamu:Chini ya anwani ya mpokeaji, barua huanza kwa kumrejelea mpokeaji kama bwana au bi. Ni makosa kumsalimia mpokeaji wa barua rasmi au kumwuliza hali yake.Ndugu Bwana Meshaki, => Taja jina lake ikiwa mnajuana na unayemwandikia.Kwa Bw/Bi, => Ikiwa humjui mpokeaji wa barua, tumia bw/bi.Mada:Kichwa cha barua rasmi huja pindi tu baada ya salamu. Hutangulizwa na maneno kama vile YAH:(yahusu). Ni sharti kichwa kiandikwe kwa herufi kubwa na kipigiwe mstari. Kichwa kinapaswa kuwa kifupi na kinachoelezea mada ya barua kiukamilifu.Utangulizi:Hukaa chini kidogo ya mada ya barua. Haya ni maelezo mafupi yasiyozidi aya moja ambayo huelezea kusudi kuu la barua kama kidokezo.Ujumbe:Ujumbe wa barua rasmi lazima uwe mfupi na unaotumia lugha rasmi.Tamati:Mwandishi humalizia kwa maneno ya hitimisho kama vile: Wako mwaminifu, [jina], Sahihi.Simu ya MaandishiDhima ya Simu ya MaandishiSimu za maandishi ni aina ya barua fupi ambazo husafirishwa kwa haraka sana kuliko barua za kawaida. Simu hizo huandikwa kwenye fomu maalumu ambazo hutolewa na shirika la posta. Simu za maandishi hujulikana kama telegram.Kwa kawaida simu za maandishi hutumika kutuma ujumbe wa dharura. Kuandika simu za maandishi ni njia ya haraka ya kufikisha ujumbe kwa sababu, baada ya kuandika simu yako ujumbe humfikia huyo unayemtumia katika muda usiozidi siku tatu. Gharama za simu za maandishi hutozwa kulingana na idadi ya maneno yaliyotumika. Kwa hiyo ujumbe unaotumwa huandikwa kwa maneno machache ili kuepuka kutozwa gharama kubwa.Mfano wa Simu ya Maandishi:MUSA KINGAMBE SLP 5299 DSMNJOO HARAKADADA MGONJWA LINGIDOMuundo wa Simu za MaandishiMuundo wa kuandika simu za maandishi una mambo yafuatayo ya kuzingatia:Anwani ya mpelekewa taarifaUjumbeJina la mwandishi au mtuma simuMambo mengine ya kuzingatia ni kuandika maneno yote kwa herufi kubwa ili kurahisisha usomaji na kuandika simu ya maandishi katika karatasi maalumu ambayo hutolewa na posta.Kadi za MialikoMuundo wa Kadi ya MialikoMambo muhimu yanayotakiwa kuonyeshwa katika kadi ya mwaliko:Jina la mwandishi au mwalikajiJina la mwalikwa, ni muhimu kuandika cheo chake kama vile: Profesa, Bi., Bw., Bw&Bi n.k.Lengo la mwalikoMahali pa kufanyika shughuliTarehe ya mwalikoWakati wa shughuliJina na anwani ya mtu atakayepelekewa majibuMialiko huweza kuandikwa kwa namna mbili yaani kama barua au kadi. Jina la mwalikwa katika kadi ya mwaliko hutakiwa kuanza na maneno ya heshima kama vile Bwana…, Bi…, au Ndugu… Ikiwa waalikwa ni mume na mke kadi itaanza na Bwana na Bibi.Mfano wa Kadi ya MwalikoFamilia ya Manyama na JosephWanapenda kukualika/kuwaalika Profesa/Dkt/Shekhe/Padri/Bi/Bw/Bw&Bi……… kwenye harusi ya kijana wao mpendwa Benny Joseph itakayofanyika huko Kiabakari katika ukumbi wa Simba siku ya Jumapili tarehe 9/12/2016 sasa 8.00 mchana hadi saa 3.00 usikuKufika kwako ndio mafanikio ya sherehe hii.Majibu kwa (wasiofika tu):Emmanuel JosephSimu: 0786 67 54 62Uandishi wa DayalojiaDhana ya DayalojiaDayalojia ni mazungumzo au majibizano baina ya watu wawili au zaidi wanaozungumza kwa kupokezana. Kama zilivyo kazi nyingine za utungaji, dayalojia inaweza kuwasilishwa kwa njia ya mazungumzo au maandishi.Katika kutunga dayalojia, mtunzi hana budi kujifanya kama mhusika katika dayalojia hiyo. Kwanza, anapaswa kutafakari kwa makini mada anayokusudia kuandikia dayalojia, kutayarisha na kupanga mawazo kimantiki na kwa mtiririko na kufikiria wahusika na kuwapangia majukumu kulingana na matendo yao. Kwa mfano, kama mhusika ni mkulima, lugha anayopewa, vifaa anavyosemekana kuvitumia na mandhari aliyomo ni lazima vifanane na hali ya mkulima halisi.Mambo ya Kuzingatia Katika DayalojiaKutoa maelezo ya ufafanuzi katika mabano ili kumfahamisha msomajiKuwa na mazungumzo ya mkato na yasiyozidiana sana kati ya wahusika. Mhusika mmoja asitawale mazungumzo kupita wengine.Kutumia vihisishi ili kufanya dayalojia iwe ya kusisimuaPawepo mwingiliano wa mazungumzo ya wahusika na kudakia maneno ili dayalojia iwe na uhalisia.Mfano wa DayalojiaWambura: (Anaonekana mwenye furaha, anamwita rafiki yake, Anna) Wow, Anna! Tumekutana tena, siamini macho yangu! (wanakumbatiana wote wakiwa na nyuso za furaha).Anna: (Anatabasamu huku ameshikilia mkono wa kulia wa Wambura, anaonesha shauku kuu) Wambura! Bado unanikumbuka? Nina furaha sana kwa kweli, ni muda mrefu sana.Wambura: (Anachekelea) Aaaah, nahisi kama naota, Anna. Siamini kama nimekutana na wewe leo hii ni muda mrefu sana, nimefurahi kwa kweli.Anna: (Anachekelea)Wambura: Mbona unachekelea tu… Topic - Previous Utungaji Wa Kazi Za Kifasihi Next - Topic Usimulizi