Topic Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi Estimated reading: 96 minutes 562 views Summary: Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.Fani katika Tamthiliya ya Watoto wa Mama N’tiliyeMwandishi: Emmanuel MbogoWachapishaji: Heko PublishersMwaka: 2002Jina la KitabuJina la kitabu Watoto wa Mama N’tiliye linasadifu yaliyomo ndani ya kitabu. Kinaeleza kuhusu maisha ya watoto wa mama ntilie, maisha ya dhiki, umaskini uliokithiri, na mazingira yasiyo ya faraja yaliyokosa malezi bora, chakula bora, elimu, na huduma ya afya. Jina hili linaakisi yaliyomo ndani ya kitabu na hali halisi katika jamii yetu, ambapo akina mama wengi wanakabiliana na changamoto za kifedha huku wakiwa na jukumu la malezi. Mwandishi ametumia jina hili ili kuibua kero na matatizo yaliyoko katika jamii.Utangulizi wa KitabuRiwaya ya Watoto wa Mama N’tiliye inasadifu maisha ya Mtanzania wa leo. Inaangazia masuala ya umaskini, hali ngumu ya maisha, wimbi la watoto wa mitaani, masuala ya uhalifu, wizi, na ujambazi, pamoja na malezi. Mwandishi Mbogo amejitahidi sana katika fani kwa kutumia muundo na mtindo unaovutia wasomaji na kuumba wahusika kwa usadifu wa hali ya juu huku mandhari yake ikisawiri maisha ya Tanzania.MuundoMuundo uliotawala katika riwaya hii ni muundo wa rukia au rejea. Mwandishi anatuelezea visa mbalimbali kwa njia ya kurukia matukio na kurudi nyuma kwa wakati. Mfano, katika sura ya tatu mwandishi anaelezea safari ya Mama Ntilie kwenda Matombo (uk.34), kisha anaacha kisa hicho na kuelezea kuzaliwa kwa watoto Kurwa na Doto. Vilevile, mwandishi anadokeza safari ya Musa (uk.80) na Zita kupandwa na kichaa (uk.81). Riwaya imegawanywa katika sura tano, na visa na matukio yamejengwa katika muundo unaotegemeana ili kukamilisha kilele cha masimulizi.MtindoMtindo uliotumika ni wa masimulizi ya mjazo au lugha ya nathari. Mwandishi ameueleza visa mwenyewe na vingine wahusika wamevielezea. Pia ametumia mitindo kadhaa, kama vile:Nafsi ya Tatu (wingi na umoja): “Peter aliokota kipande cha muhogo” (uk.15), “watu walisongamana walisukumana” (uk.26).Nafsi ya Kwanza (umoja na wingi): “nitasema nitasema!” (uk.58), “twende tule” (uk.56).Nafsi ya Pili (dayalojia): Majibizano kati ya Mama Ntilie na Zita (uk.89).Matumizi ya nafsi mbalimbali yanavuruga monotoni na kuvuta umakini wa msomaji, huku nyimbo na majibizano yakiburudisha na kuongeza mvuto wa masimulizi.Matumizi ya LughaRiwaya imetumia lugha rahisi, fasaha, na inayoeleweka kwa wasomaji. Kuna matumizi ya lugha ya Kiingereza (uk.36, “chloroquine”, “faster faster mama”), na lugha ya mitaani (uk.41, “kudeku”). Tamathali za semi zimetumika sana:Tashibiha: “mdomo wake ulio kaa kama bakuli la pombe” (uk.10), “miguu kama ya mamba” (uk.15).Tashihisi: “mabega yenyewe tayari yalikuwa yamechongwa kwa pombe ya gongo” (uk.10), “moshi wenye harufu ya kuudhi ulilelea hewani” (uk.19).Sitiari: “Nyama nyie” (uk.10).Ritifaa: “Mama? Mama yuko wapi, Baba yuko wapi?” (uk.38).Tafsida: “haja kubwa” (uk.91).Mbinu nyingine za kisanaa kama onomatopea, takriri, mjalizo, mdokezo, nidaa, na matumizi ya semi (nahau, methali, misemo) zimeongeza uhalisia na mvuto katika riwaya hii.WahusikaMama NtilieMama mzazi wa Peter na ZitaMke wa Mzee LomolomoMlezi mzuri wa familiaMvumilivu na mwenye hurumaMchapakazi na anayejitumaAna hali ngumu kimaishaMzee LomolomoMume wa Mama NtilieBaba wa Peter na ZitaMlevi na mvivuSi mlezi bora, hajali familiaAnakufa kwa sababu ya kunywa pombe sanaPeterMtoto wa Mama NtilieAnakosa elimu kwa sababu ya umaskiniAna bidii na mchapakaziAna hurumaAnafungwa jela kwa kufanya biashara haramu ya madawa ya kulevyaZitaMtoto wa kike wa Mama NtilieAnakosa elimu kwa sababu ya umaskiniMchapakaziAnagombana na Kurwa, hakupenda aje kwao, roho mbayaAnakufa kwa ugonjwa wa kichaa cha mbwaDotoMtoto yatima wa mtaaniAnauawa baada ya kujiingiza katika uhalifu wa wiziMgomvi na katiliKurwaNdugu yake DotoAnaishi mtaani, yatimaAna huruma, nguvu, na jasiriMchapakaziAnaishia jela kwa makosa ya Musa na PeterMusaMtoto aliyekosa elimu baada ya kukosa sare na adaAlikosa malezi mazuri ya wazaziMhalifu, anafanya biashara haramu za madawa ya kulevyaAna tamaa ya pesaRafiki mbaya kwani alimshauri Peter kuuza madawa ya kulevyaMwalimu ChikoyaMwalimu wa Peter na ZitaAliwafukuza Peter na Zita shule kwa kukosa adaSi mwalimu mzuriMandhariMandhari iliyotumika ni ya jiji la Dar es Salaam, kwa kutajwa maeneo kama Manzese, Tabata, Kiwanda cha Urafiki, Kisutu, na Muhimbili. Pia kuna mandhari ya nyumbani kwa Mama Ntilie (uk.5), hospitali ya Muhimbili (uk.89), na jaani-jaa la Tabata (uk.20). Mandhari haya yanasaidia kuibua dhamira halisi zinazosawiri maisha ya Mtanzania wa leo, kama vile umaskini na wimbi la watoto wa mitaani.Docs: 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18Tagged:Form 3kidato cha tatuKiswahili Topic - Previous Maendeleo Ya Kiswahili Next - Topic Utungaji Wa Kazi Za Fasihi Andishi