Topic Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi Estimated reading: 96 minutes 531 views Summary: Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.Hakiki ya Fani katika Riwaya ya “Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe”Jina la Kitabu: Ngoswe Penzi Kitovu cha UzembeMwandishi: Edwin SemzabaWachapishaji: Nyambari Nyangwine PublishersMwaka: 2006Utangulizi wa Kitabu“Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe” ni tamthiliya maarufu sana ambayo imewahi kuigizwa katika redio Tanzania na katika majukwaa mbalimbali hapa nchini. Ni tamthiliya ambayo imeundwa vyema katika vipengele vya fani na maudhui. Mwandishi ametumia lugha nzuri na yenye mvuto kwa wasomaji, yenye mbinu za kifasihi zilizosheheni, na muundo wenye mtiririko mzuri unaoakisi kuanza kuchipuka kwa matukio mpaka kilele cha matukio. Wahusika wamebeba vyema uhusika wao, mfano Ngoswe.Ameteua dhamira zinazogusa jamii ya leo kama vile uzembe, madhara ya ulevi, uzembe kazini, na suala la matabaka kati ya mjini na vijijini. Mtazamo, falsafa, na msimamo wa mwandishi ni kulenga kuibadilisha jamii na kuleta maendeleo.Jina la KitabuJina la kitabu “Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe” linasawiri vyema yaliyomo ndani ya kitabu hicho, kwani Ngoswe ndiye mhusika mkuu anayebeba dhamira kuu ya tamthiliya. Penzi limeonekana kuwa ni kitovu cha uzembe kwani ndilo lililopelekea kuteketezwa kwa karatasi za takwimu za sensa. Hivyo, jina la kitabu si tu kwamba linasawiri yaliyomo katika kitabu bali pia katika jamii.MtindoMwandishi ametumia mtindo wa dayalojia au majibizano. Mwandishi amepanga visa na masimulizi kwa kutumia majibizano ya wahusika.Matumizi ya Nafsi ya Kwanza: Mwandishi ndiye ameyafafanua na kuelezea baadhi ya matukio. Katika karibu kurasa zote, mwandishi ameonekana kuwa ndiye msimuliaji wa matukio.Matumizi ya Nafsi ya Pili: Hapa watu wawili na zaidi wanajibizana. Wahusika wanajibizana kuibua dhamira na migogoro. Kuna majibizano baina ya Mzee Mitomingi, Ngoswe, na Mazoea, nk.MuundoMuundo uliotumika ni muundo wa moja kwa moja au sahili, ambapo matukio yanaoneshwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Mwandishi amepanga visa na matukio yake katika maonesho matano. Kila kichwa kina maelezo yaliyojadiliwa katika onesho hilo.Kijito: Hapa yanaeleza jinsi mambo yanavyoanza, jinsi Ngoswe anavyoingia kijijini, anavyopokelewa, na kuanza kufahamiana na wenyeji wake.Vijito: Ngoswe anaanza kufanya kazi iliyompeleka kijijini na tunaanza kuoneshwa changamoto anazokumbana nazo.Mto: Ni mwendelezo wa matukio ya mwanzo ambapo visa vinazidi kukua.Jito: Ngoswe anakumbana na changamoto nyingi zaidi katika kazi yake. Anaanguka kwa sababu ya kujiingiza katika mapenzi na msichana Mazoea, anaendekeza ulevi, na kuharibu kazi kabisa.Bahari: Inaoneshwa mwisho wa mambo jinsi yalivyokuwa. Yanaonekana mahojiano baina ya Serikali, Ngoswe, na Mitomingi juu ya uzembe uliofanyika wa kupoteza takwimu na hapa ndipo suluhisho linapotolewa juu ya matatizo hayo.WahusikaNgosweKijana wa kiume mwenye umri kati ya miaka 20-25Ameelimika na amestaarabikaAnatumwa na serikali kufanya sensa kijijiniAnajihusisha na mapenzi na msichana MazoeaNi mlevi na hana umakini katika kaziAliharibu kazi ya serikaliHafai kuigwa na jamiiMazoeaMsichana mwenye umri kati ya miaka 18-20Binti wa Mzee Ngengemkeni MitomingiHana elimu na hajastaarabikaAna nidhamu ya woga na tamaHana msimamo; alikubali kuchukuliwa na Ngoswe hali akijua alishatolewa mahariHafai kuigwa na jamiiNgengemkeni MitomingiBalozi katika kijiji chakeBaba mzazi wa MazoeaAmeoa ndoa ya mitara, ana wake wawiliHajaelimikaAnashikilia mila na desturi za kaleMlevi na mkali sanaAnateketeza karatasi za takwimuWahusika WengineMzee Jimbi: Mwanakijiji, hajaelimika, ni mlevi, ana wake wawili, anashikilia ukaleMama Mazoea: Mke mkubwa wa Mitomingi, mama yake Mazoea, mlezi wa familia, hapewi nafasi ya kutoa maamuzi katika familiaMama Inda: Mke wa pili wa Mzee Mitomingi, mama yake Huzuni, hapewi nafasi ya kutoa maamuzi, ni mlezi wa familiaMandhariMandhari ya tamthiliya hii imechorwa katika mazingira ya kijijini. Mambo yanayoelezwa ni ya kijijini kama vile kilimo, hali ya watu kimaisha, huduma duni za kijamii kama vile shule, na umbali wa makazi toka nyumba moja hadi nyingine. Mandhari hii inaibua dhamira mbalimbali kama vile umaskini, ukosefu wa elimu, huduma duni za afya vijijini, na masuala ya imani potofu.Matumizi ya LughaMwandishi ametumia lugha fasaha na rahisi kueleweka kwa wasomaji. Pia kuna matumizi ya lugha nyingine kama vile “bell bottom” (uk. 1).Matumizi ya Semi:Methali: “Penye nia pana njia” (uk. 22), “Waona vyaelea vyaundwa” (uk. 27)Misemo: “Akuwaniae ujovu haji kweupe” (uk. 14)Nahau: “Hebu keti tutupe mawe pangoni” – tule chakula (uk. 11), “Mbongo zimelala” – ana maarifa (uk. 7), “Pombe na yeye ni pete na chanda” – anapenda pombe sana (uk. 14)Matumizi ya Tamathali za Semi:Tafsida: “Wala hajarudi, kama ingekuwa ni kujisaidia si angekuwa amekwishamaliza?” (uk. 21)Tashbiha: “Vumbi jekundu kama ugoro wa subiana” (uk. 1), “Sarawili yake miguuni kama kengele ya bomani” (uk. 8), “Wanaondoka huku wakitazamwa kama vile mizuka” (uk. 17)Sitiari: “Kiziwi mkubwa wee!” (uk. 7), “Pombe na yeye ni pete na chanda!” (uk. 14), “Karatasi? za takwimu? Ndio wanyama gani hao?” (uk. 26)Mubaalagha: “Kupeleka chakula ndio umefanya makao!” (uk. 11), “Kujibu swali ndio ukachukua mwaka mzima!” (uk. 11)Mbinu Nyingine za Kisanaa:Mdokezo: “Sijui….. siwezi….. namuogopa baba” (uk. 22), “Huyo mtoto wenu wa kwanza anaishi hapa au…..” (uk. 16)Takriri: “Mama Masikio! We Mama Masikio!” (uk. 9), “Hodi! Hodi!” (uk. 13), “Karibu karibu” (uk. 2)Tashtiti: “Hivyo waitwa nani?” (uk. 5), “Mchumba? Kwani mchumba ni kitu gani?” (uk. 22), “Karatasi? Za takwimu? Ndio wanyama gani hao?” (uk. 26)Onomatopea/Tanakali Sauti: Kifaruhande anacheka “Ha! ha! ha!” (uk. 7)Ujenzi wa TaswiraMwandishi ametumia taswira ya mto kuelezea visa vyake kwa mpangilio ufuatao:Kijito: Hapa mwandishi anaanza kueleza mambo yakiwa machanga kabisa, yanayoanza kuchipuka kama kijito kidogo ambacho ni sehemu ya mwanzo wa mto. Sehemu hii inafafanua jinsi Ngoswe anavyoingia kijijini na anavyoanza kufahamiana na wenyeji wake.Vijito: Huu ni muunganiko wa vijito vidogovidogo ambapo mwandishi anaanza kueleza visa vidogovidogo vinavyoungana na kujenga hadithi. Hapa Ngoswe anaanza kufanya kazi kijijini na tunaanza kuona changamoto anazokumbana nazo.Mto: Sehemu hii inaashiria kuwa mambo yameanza kuwa mazito zaidi, na visa vinaanza kukua. Ngoswe anazidi kuingia katika changamoto kubwa zaidi na matatizo yanazidi kumwandama.Jito: Hii ni taswira inayotumiwa kuashiria hatari kubwa zaidi. Mambo yamekuwa makubwa na magumu zaidi, na Ngoswe anakumbana na changamoto nyingi katika kazi yake. Anaanguka kabisa kwa sababu ya kujiingiza katika mapenzi na msichana Mazoea na kuendekeza ulevi, hivyo kuharibu kazi kabisa.Bahari: Hatimaye, mwandishi anaelezea hatima ya mambo. Ngoswe anazama na kupotea kabisa kama bahari yenye kina kirefu na maji mengi. Hafanikiwi kutoa takwimu kwani karatasi zilichomwa moto, hivyo kuonesha mwisho wa safari yake na kushindwa kwake kutekeleza majukumu.Docs: 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18Tagged:Form 3kidato cha tatuKiswahili Topic - Previous Maendeleo Ya Kiswahili Next - Topic Utungaji Wa Kazi Za Fasihi Andishi