Comment

Darasa Huru

Darasa Huru

Limitless Potential

Explore, learn, excel—educational resources made simple and free.

Topic

Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi

Estimated reading: 96 minutes 538 views

Summary: Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.

Fani katika Riwaya ya Joka la Mdimu

Utangulizi wa Kitabu

Joka la Mdimu ni riwaya iliyojengwa kwa visa tofautitofauti vinavyoungana kukamilisha masimulizi. Riwaya hii inasawiri mambo yaliyopita ya nyakati za shida kama vile uhaba wa mafuta ya petroli, nguo, na vyakula. Pamoja na hayo, inajumuisha dhamira zinazohusiana na maisha ya Mtanzania wa leo kama vile masuala ya rushwa na uhujumu uchumi.

Jina la Kitabu

Jina la kitabu, Joka la Mdimu, ni picha ya nyoka anayeishi katika miti ya kijani, hasa Minyaa na Midimu. Nyoka huyu ni hatari kwani rangi yake inamfanya awe ngumu kumtambua. Taswira hii inatumiwa kufananisha na viongozi wanaoonekana kama wananchi wa kawaida, lakini ni hatari kwani wanageuka na kuwa mafisadi, wala rushwa, na wasiojali maslahi ya wananchi.

Muundo

Riwaya hii imetumia muundo changamani na muundo sahili au msago. Kwa mfano, katika sura ya Mindule, mwandishi anaanza na habari za Amani, dereva wa taxi, na kisha kurudi nyuma kueleza jinsi Amani alivyopata kazi ya udereva. Pia kuna sura kama Boko ambapo mwandishi anarukia kisa kingine kisha kurudi nyuma na kuendeleza hadithi ya awali. Mwandishi ameweka visa na matukio katika sura kumi, kila sura ikiwa na jina la mhusika.

Mtindo

Mwandishi ametumia mitindo mbalimbali ili kuipamba kazi yake na kuvutia wasomaji.

  • Nafsi ya tatu umoja: “Amani aliangalia…”
  • Nafsi ya tatu wingi: “wote walitoka nje kuelekea klabuni…”
  • Nafsi ya pili: “mmechoka kuangalia video?”
  • Nafsi ya kwanza: “mimi nimemaliza…”

Mwandishi pia ametumia nyimbo, masimulizi ya hadithi ndani ya hadithi, na matumizi ya lugha nyingine kama vile Kiingereza na Kiarabu.

Matumizi ya Lugha

Lugha fasaha na inayoeleweka imetumiwa, pamoja na lugha za mtaa na tamathali za semi kama vile tashibiha, sitiari, tashihisi, tafsida, takriri, onomatopea, tashtiti, nidaa, methali, misemo, na nahau. Mfano wa matumizi ya tashibiha: “ngozi yake nyeusi kama udongo wa mfinyanzi”.

Wahusika

  • Amani: Dereva taxi, mwenye upendo, mchapakazi, mwenye hekima na busara, huruma, na ni rafiki wa kweli wa Tino.
  • Tino: Mchapakazi, mlezi bora wa familia, baba wa Cheche, ana huruma na upendo wa dhati, jasiri, na mwanamichezo.
  • Brown Kwacha: Mkurugenzi wa idara ya fedha za kigeni, muhuni, malaya, fisadi, mpenzi wa anasa, na si mwaminifu kwa familia yake.
  • Jinja Maloni: Jasiri, mwenye nguvu, huruma, mchapakazi, mlevi, na maskini.
  • Daktari Mikwala: Daktari bingwa wa mifupa, mpenda rushwa, asiye mwajibikaji, na mlevi.
  • Shiraz Bhanj: Mfanyabiashara, mtoa rushwa, na anayefanya biashara za magendo.
  • Zitto: Mfanyakazi bandarini, mwanamichezo, jasiri, na ana kipato duni.
  • Cheche: Mtoto wa Tino, ana nidhamu, bidii, mwanamichezo, na upendo kwa wazazi wake.
  • Mwema: Mke wa Tino, mvumilivu, mchapakazi, na ana mapendo ya dhati kwa familia yake.
  • Josephine na Leila: Wasichana wahuni waliojiuza kwa Brown Kwacha.

Mandhari

Mandhari iliyotumika ni ya mjini, ikijumuisha maeneo ya nje ya jiji la Dar es Salaam kama vile Boko, Sega, na Mindule. Mandhari hii ni sadifu kwa masuala ya rushwa, upotevu wa haki, hali ngumu ya uchumi, na maisha kwa ujumla, ambayo ni matatizo halisi ya jamii ya Tanzania.

Kwa muhtasari, riwaya ya Joka la Mdimu inajitahidi kuakisi maisha ya Mtanzania kwa kutumia fani mbalimbali kama muundo, mtindo, matumizi ya lugha, na uumbaji wa wahusika wenye sifa za kuigwa na jamii.


Leave a Comment

Share this Doc

Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi

Or copy link

CONTENTS

Agricultural Development

What is Agriculture? Agriculture refers to a fundamental human activity, which i...

Population and Development

POPULATION STUDIES Is the general activities carried out for the purpose of acqu...

Study of Soil

CONCEPT OF SOIL AND SOIL PROFILE Soil appears very complex and thus differe...

Water Masses

GROUND WATER WATER CYCLE Rain falls on the earth surface in filtrates (soaks int...

Topic

The Dynamic-Earth And Consequence

GEOMORPHOLOGY Is the science which deals with development of land forms, (relief...

Position Behaviours And Structure Of The Earth

GLOBE Is the model of the earth Earth Is ball of rock partly covered by wat...

Photograph interpretation

PHOTOGRAPHS OVERLAPING, PHOTOGRAMMERTRY, MAP MAKING AND DIAGRAMS SKETCHING. 1. P...

Maps and map interpretation

MAP SCALE Maps are all generally, much smaller in size as it an be compared to t...

Simple survey and mapping

INTRODUCTION TO SURVEYING Surveying is an art or a science of measuring and reco...

Field research techniques

Definitions of Research – Research is the systematic investigation into a...

Application of statistics in geography

STATISTICS Statistics is a branch that deals with every aspect of the data. Stat...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel