Comment

Darasa Huru

Darasa Huru

Limitless Potential

Your future starts with knowledge—access it for free.

Topic

Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi

Estimated reading: 96 minutes 537 views

Summary: Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.

Uhakiki wa Fani katika Kazi za Fasihi Andishi

Uhakiki wa Fani katika Riwaya ya Takadini
Mwandishi: Ben J. Hanson
Wachapishaji: Mathews Bookstore and Stationaries
Mwaka: 2004

Jina la Kitabu:
Jina la kitabu “Takadini” lina maana ya “Sisi tumefanya nini”. Hili ni jina ambalo Sekai alimpa mwanae mara baada ya kumzaa. Jina hili lilitokana na majonzi aliyokuwa nayo juu ya kutaka kuuawa kwa mwanae bila hatia, ila tu kwa sababu ya mila za jamii yake. Jina hili ni sadifu kwani linasawiri vyema maudhui yaliyomo katika kitabu hiki. “Sisi tumefanya nini?” ni swali linalotokana na ukosefu wa haki ya kuishi, kubaguliwa, kutopendwa, na kutengwa kwa watu wenye matatizo katika jamii. Swali hili linawalelekea wanajamii ambao bado wanashikilia mila potofu zinazowakandamiza na kuwanyanyasa watu wenye matatizo mfano, ulemavu wa ngozi, wagonjwa, nk. Mwandishi ametumia jina hili makusudi ili kuionesha jamii hali halisi ya vilio vya albino, wasichana wadogo wanaolazimishwa kuolewa, nk.

Muundo:
Muundo alioutumia mwandishi wa riwaya hii ni muundo wa msago au muundo wa moja kwa moja. Amejenga matukio kwa mtiririko sahili, kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa maisha ya kijana Takadini. Matukio yamegawanywa katika sura kumi na tatu, ambapo visa vimejengwa kwa ufundi na kuvifanya vijengane na kukamilishana kuelekea kilele cha masimulizi.

Sura za Kitabu:

  • Sura ya Kwanza hadi ya Kumi na Tatu: Kila sura inaeleza hatua tofauti za maisha ya Takadini, kutoka kuzaliwa kwake, kukua, na changamoto mbalimbali anazokumbana nazo. Pia inaelezea juhudi za mama yake, Sekai, kumlinda kutokana na mila potofu za jamii yao.

Mtindo:
Mwandishi ametumia mitindo kadha wa kadha ili kuipamba kazi yake na kuifanya ivutie wasomaji. Mtindo wa matumizi ya nafsi mbalimbali, matumizi ya nyimbo, matumizi ya hadithi ndani ya hadithi, matumizi ya lugha fasaha, na matumizi ya tamathali za semi ni miongoni mwa mbinu alizotumia.

Matumizi ya Lugha:
Lugha aliyotumia mwandishi ni fasaha na rahisi kueleweka kwa wasomaji wake. Pia ametumia lugha za kikabila ili kuwaleta wasomaji kwenye mazingira halisi ya kiutamaduni ya jamii ile.

Tamathali za Semi:

  • Tashibiha: Muda huenda polepole mithili ya mwendo wa kakakuona.
  • Tashihisi: Ndege mbalimbali wakiimba kuikaribisha siku mpya.
  • Tafsida: Sehemu zake za siri.
  • Sitiari: Tapfumaneyi aligeuka mbogo.

Matumizi ya Semi:

  • Methali: Kipofu huwa hachagui shimo la kutegea wanyama.
  • Misemo: Kufikiri katika siri ni sawa na safari ya mbwa.
  • Nahau: Penzi langu kwake halikufua dafu.

Wahusika:

  • Sekai: Mke wa Makwati, jasiri, anapinga mila potofu, mvumilivu, mchapakazi, mtiifu, mwenye huruma, mnyenyekevu, na mwenye mapenzi ya dhati.
  • Takadini: Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino), jasiri, anabaguliwa, mvumilivu, msikivu, na mpiga mbira maarufu.
  • Makwati: Mume wa Sekai, ana mila na desturi potofu, hana mapenzi ya dhati kwa mwanae.
  • Chivero: Mzee wa kijiji, mwenye roho nzuri, huruma, busara, hekima, na mganga wa tiba za asili.
  • Mtemi Masasa: Kiongozi bora, mwenye busara, hekima, huruma, na msikivu.
  • Nhamo: Kijana mwenye majivuno na jeuri, hafai kuigwa.
  • Tendai: Mke mdogo wa Mtemi Masasa, mvumilivu, rafiki mzuri wa Sekai, na mwenye bidii.
  • Nhariswa na Mkewe: Wazazi wa Shingai, wanashikilia mila potofu, hawafai kuigwa.
  • Kutukwa: Mpigaji mbira maarufu, alimfundisha Takadini, na anafaa kuigwa.

Mandhari:
Mandhari aliyotumia Ben J. Hanson ni ya kijijini, inayoelezea maisha ya watu na mazingira yao, masuala ya kilimo, ufugaji, sherehe za mavuno, na makazi ya watu kijijini. Mandhari hii ni halisi na sadifu kwani inaakisi mambo ya imani potofu na za kishirikina kama vile kuwaua watoto sope au albino.

Leave a Comment

Share this Doc

Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi

Or copy link

CONTENTS

Agricultural Development

What is Agriculture? Agriculture refers to a fundamental human activity, which i...

Population and Development

POPULATION STUDIES Is the general activities carried out for the purpose of acqu...

Study of Soil

CONCEPT OF SOIL AND SOIL PROFILE Soil appears very complex and thus differe...

Water Masses

GROUND WATER WATER CYCLE Rain falls on the earth surface in filtrates (soaks int...

Topic

The Dynamic-Earth And Consequence

MATERIALS OF THE EARTH’S CRUST What is an element? A substance which cann...

Position Behaviours And Structure Of The Earth

GLOBE Is the model of the earth Earth Is ball of rock partly covered by wat...

Photograph interpretation

PHOTOGRAPHS OVERLAPING, PHOTOGRAMMERTRY, MAP MAKING AND DIAGRAMS SKETCHING. 1. P...

Maps and map interpretation

CONTENT OF MAPS Map content refers to a body of information inserted on a map wi...

Simple survey and mapping

INTRODUCTION TO SURVEYING Surveying is an art or a science of measuring and reco...

Field research techniques

Definitions of Research – Research is the systematic investigation into a...

Application of statistics in geography

STATISTICS Statistics is a branch that deals with every aspect of the data. Stat...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel