Topic Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi Estimated reading: 96 minutes 540 views Summary: Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.Maudhui katika Diwani ya ChekachekaHakiki maudhui katika Diwani ya ChekachekaDHAMIRAMwandishi amejadili dhamira mbalimbalizinazosawiri jamii yetu ya leo. Dhamira hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:Uongozi boraSuala la uongozi bora limejadiliwa na mwandishi wa diwani hii ikiwa kama jambo la msingi sana katika maendeleo ya Nchi. Mashairi ya“Mwinyi umewasha moto”na“indira”yanaelezea vyema juu ya viongozi ambao ni mfano wa kuigwa katika jamii.Mfano katika shairi la “Indira” anasema juu ya kiongozi Indira ambaye aliongoza vyema katika uongozi wake. Anawataka viongozi wa sasa kuiga mfano huo, anasema:Pia hakuacha kugusia suala la viongozi wasiotimiza majukumu yao. Haya anayasema katika shairi la“Muwapi nawauliza”, “Utaliwa kama pumba” “Gunia la mikutano”mfano katika shairi la“Muwapi nawauliza”anawaamsha viongozi ili watimize majukumu yao:Kupinga unyonyajiMwandishi anakemea masuala ya unyonyaji wa tabaka la chini. Shairi la“Kuna nini”, “Chatu mmeza matonge” “Chunguzeni walo mbele”, “Kazi yetu harakati”.Mfano katika shairi la“Chatu mmeza matonge”mwandishi anazungumzia jinsi wanyonge wanavyoteseka katika hali ngumu ya maisha. Amelionesha hili ili jamii na serikali viweze kuwasaidia na kuwainua watu hawa.Kupinga udikteta na ukosefu wa demokrasiaSuala la ukosefu wa demokrasia na haki ya kweli ni mambo ambayo yanafanya wanajamii kushindwa kujadili na kuweka wazi masuala nyeti ya kijamii pale inapobidi. Mwandishi kwa kuliona hili kama jambo la muhimu amelizungumzia katika mashairi ya“Raia si mali kitu”, “Dhahabu ya fahari”.Kupinga ukoloni mamboleaoMashairi ya“Lazima mniamini” na “Utumwa huru”ni mashairi ambayo yanaelezea juu ya ukoloni mamboleo. Mwandishi anaonesha kuwa nchi nyingi za kiafrika zimepata uhuru lakini ni uhuru wa maneno tu na si vitendo. Nchi hizi bado zinaamuliwa na kupangiwa mambo. Mwandishi anasema katika shairi la“Utumwa huru”anasema;Ukombozi wa kiuchumiSuala la ukombozi wa kiuchumi ni jambo ambalo huendana na maisha ya kila siku ya mwanadamu. Uchumi bora ndio huleta maendeleo zaidi katika jamii. Mwandishi analisema hili katika shairi la“Muwapi nawauliza”, “Kweli ilojaa udi”mfanokatika shairi la“Kweli ilojaa udi” anasemea juu ya uhaba wa bidhaa miaka ya themaninikwani uchumi ulizorota.Kupiga vita matabakaShairila“Chunguzeni walo mbele”, “Kazi yetu harakati”na“Gunia la mikutano”. Mfano katika shairi la “Gunia la mikutano”Hapa mwandishi anajaribu kutuonesha utofauti kati ya wenye navyo au watawala na wasio nacho. Maisha yao ni tofauti kabisa. Wakati wengine wakifanya mambo ya anasa na starehe zisizo na tija wengine waumia kwa njaa na dhiki. Hivyo si budi jamii kwa pamoja kupinga suala hili kwa kuziba mifumo yote ya kitabaka.Umuhimu wa Washairi kutunga mashairi boraBila kugusia masuala ya fani katika mashairi, Mashairi bora ni yale ambayo yanasema ukweli juu ya mambo jinsi ulivyo bila kificho. Ni mashairi yanayoangazia maisha ya kila mmoja katika jamii, hukosoa bila upendeleo wala hayasiti kusema na kutetea haki mara inapobidi. Shairi la“Tuambae ukasuku”ni shairi ambalo linawataka washairi kutunga mashairi wakiangalia matatizo ya jamii.Suala la maadili mema na maonyoKuepuka tamaa: Katika shairi la “Moyo”mwandishi anauasa moyo kutokuwa na tamaa kwani unaweza kudhurika sababu ya tamaa.Kuwa na uadilifu katika dini: Shairi la“Chanzo cha huo uozo”linaeleza juu ya aupotofu wa maadili kwa viongozi wa dini anawaasa kuzingatia misisngi ya imani zao na kuwa mfano katika jamii.Kuthamini utu: Utu kuthaminiwa ni sehemu ya mambo muhimu sana kwa mwanadamu. Katika shairi la“Utu umekuwa kima”mwandishi naonesha jinsi ambavyo watu siku hizi hawatahmini utu na kuizingatia mambo mengine. Anaikumbusha jamii kuwa utu wa mtu ni muhimu sana kuthaminiwa.Umuhimu wa kuwa na msimamo katika maisha: Shairi la“Chura umegundulika”linafananisha watu wasio na msimamo katika maisha na chura. Anawaasa watu kutokuwa kama chura kwa tabia yake ya kutoeleweka kama anaishi majini au nchi kavu.Umuhimu wa kuwajali wazazi: Mwandishi kwa kutambua umuhimu mkkubwa wa wazazi, anaielimisha jamii kupitia shairi lake la“Ni wapi ushauri?”kuwa vijana wanapaswa kuwatunza na kuwasaidia wazazi wao pindi wanapozeeka.Umuhimu wa kujiheshimu katika mapenzi: Shairi la “Penzi lisilo heshima”linakemea juu ya tabia mbaya ya watu wasiojiheshimu katika ndoa au mapenzi. Anakemea mapenzi ya pesa. Anashauri jamii kupendana kuthamini utu wa mtu na sio pesa.Umuhimu wa kuwa na busara na hekima: Hekima ni jambo jema kwa mwanadamu. Mwandishi anaona kuwa kwa ktutumia hekima kuamua mambo ni vyema kuliko kukurupuka. Anayasema haya katika shairi la“Moyo”.Kuepuka shari: Mwandishi katika shairi la“Moyo”anaiasa jamii kuepuka shari na ugomvi wala kutoichochea. Anawataka watu kuwa chanzo cha amani na mapatano.FALSAFA: Mwandishi anaamini kuwa masuala ya haki na uwajibikaji ni suluhu ya maendeleo.MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu kwani kero na matatizo anayoyazungumzia katika jamii yapo kweli. Kama vile matabaka, uhujumu uchumi na hali ngumu ya maisha. Anatoa suluhu muafaka kwa matatizo hayo.MSIMAMO: Msimamo ni wa kimapinduzi kwani mwandishi analenga katika kuibadilisha jamii. Anapinga masuala ya unyonyaji na ukandamizwaji. Pia anaona ipo haja ya viongozi na watawala kujituma kadiri inavowapasa. Mwandishi pia aligeuzia jicho masuala ya kimaadili kwani hakusita kuwakanya wavivu, waliopotoka katika uadilifu nk.UJUMBEUadilifu katika dini na imani ni muhimu kuzingatiwa.Haki na usawa ni suluhu ya migogoro ya kisiasa.Wanajamii wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kukomboka kiuchumi.Busara ba hekima ni mambo ya kuzingatia katika uamuzi wa jambo fulani.Utu wa mtu unapaswa kuthaminiwa.Washairi wanapaswa kuandika mashairi yanayoipasa jamii badala ya kuwa na ukasuku.Mapenzi ya heshima na dhati ndio mapenzi ya kweli.Matabaka katika jamii ni kikwazo na kichocheo cha unyonyaji hivyo si budi kupiga vitaDocs: 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18Tagged:Form 3kidato cha tatuKiswahili Topic - Previous Maendeleo Ya Kiswahili Next - Topic Utungaji Wa Kazi Za Fasihi Andishi