Topic Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi Estimated reading: 96 minutes 541 views Summary: Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.Maudhui katika Ushairi wa Malenga WapyaHakiki Maudhui katika Ushairi wa Malenga WapyaDHAMIRASuala la uongozi bora na uwajibikajiSuala la uongozi limejadiliwa katika pande zote mbili za uongozi mzuri na uongozi mbaya. Waandishi wameonesha yote haya wakiwa na lengo la kuikomboa jamii. Wamesisitiza kuhusu uongozi bora mfano katika shairi la “Payuka” anawaasa viongozi kuwa watekelezaji wa yale wanayoyaahidi na sio kuwa wapayukaji tu. Mfano ubeti wa pili anasemaAnakemea mapenzi yasiyo ya kweli ya usaliti. Mfano katika shairi la“Sili nikashiba” ”Si wewe?Mfano katika shairi la“Sili nikashiba”anasema juu ya usaliti;Pia katika shairi la “Puuzo” anawakanya viongozi wasiowajibika kutekeleza majukumu yao na kuacha uzembe. Anawaasa kujituma na kufanya kazi kwa bidii kwani ni wajibu wao. Anasema katika ubeti wa kwanzaUkombozi wa kiuchumiMwandishi anaona kuwa ili jamii ikomboke kiuchumi yapo mambo ya msingi kutekelezwa. Miongoni mwa mambo hayo ni kufanya kazi kwa bidii na kuacha uvivu. Mfano katika shairi la “Charuka” tunaambiwa kuwa.Pia anakazia suala la kilimo kama ndio msingi wa kujikomboa kichumi katika shairi la “Adui” na katika shairi la “Mkulima”anaonesha umuhimu wa kumthamini mkulima na kilimo. Vikiwa kama vigezo vya maendeleo nchini mwetu. Mfano katika shairi la “Adui” anasema;Pia katika shairi la“Tuyazingatie haya”mwandishi anatajamambo ambayo anaamini kuwa yakizingatiwa yataweka uchumi kuwa imara kama vile, kuchapa kazi, kukomesha ubaguzi kutopora mali za serkali, kushirikiana, kukosoana na kuepuka tamaa. Mfano ubeti wa pili anasema;Ukombozi wa mwanamkeMwandishi kwa kutambua nafasi muhimu ya mwanamke katika jamii, hakusita kuikumbusha jamii juu ya kuwaheshimu, kuwathamini, kuwapa uhuru na kupinga tamaduni zote zinazomkandamiza mwanamke. Anaamini kuwa kumkandamiza mwanamke ni kuikandamiza jamii. Anayazungumzia haya katika shairi la “Kifungo”, “Hina inapapatuka”, “Raha”.Mfano katika shairi la“kifungo”ubeti wa saba anasema:Suala la maadili mema na maonyoUmuhimu Wa kuwa na kauli nzuri.Mwandishi katika shairi la “Ulimi” anawaasa watu kuwa ulimi mzuri kwa maana ya kuongea vizuri na watu kwa adabu, na heshima. Anaona kuwa ulimi ni kiungo kidogo lakini kinaweza kusababisha matatizo au mambo mazuri. Anauasa ulimi akisema;Umuhimu wa kutenda wema kwa binadamu wenzetu:Mwandishi anaona kuwa wanajamii wanapaswa kutenda wema kwa wanajamii wenzao kwani matokeo ya wema ni mafanikio na shukrani. Anasema katika shairi la“Hisani hulipwa”Umuhimu wa kuwa na subira katika maisha:Mwandishi anawaasa wanajamii kutokurupukia maisha hasa vijana. Katika shairi la “Siharakie maisha”Anaona upo umuhimu wa kufanya mambo kwa wakati na kuacha tamaa kwani kila jambo na wakati wake. Anawaasa wanafunzi kushikilia masomo na kutolimbukia mambo ambayo si wakati wake. Anasema;Umuhimu wa kuishi vyema duniani:Katika shairi la “Ulimwengu”na“Maisha ni kama njia”mwandishi anaiambia jamii kuishi vizuri katika dunia kwani dunia ni mapito tu. Mfano katika shairi la“Maisha ni kama njia”anasema;Uaminifu katika ndoa:Suala ndoa kwa jinsi anavyosema mwandishi uaminifu ndio jambo la msingi kwani huleta upendo na amani kwa familia. Anawashauri wanaume kujali familia zao na kuwa na mahusiano mengine nje ya ndoa. Katika shairi la“Kwanini”anasema;Matumizi mazuri ya pesa:Mwandishi anaona upo umuhimu wa kutofuja pesa. Anashauri watu kuwa na utamaduni wa kuweka akiba. Anaona kuwa ufujaji pesa ni dhambi na si haki. Katika shairi la“Israfu”Kuzingatia dini na kumuabudu Mungu:Mwandishi anawaasa wanadamu kutii maadili ya dini zao. Kwani misingi ya dini huelekeza watu katika mema. Anasema haya katika shairi la“Maisha ni kama njia”.Ubeti wa tano anasema;Suala la Mapenzi:Katika shairi la “Ua” na katika shairi la “Nipate wapi mwingine”waandishi wanaona kuwa mapenzi ya dhati na ya kweli ni jambo jema. Anawataka watu kuthamini na kuwaheshimu wapenzi wao na binadamu wengine. Mfano katika shairi la“Ua”anasema;Pia katika shairi la“Nipate wapi mwingine” mwandishi anazungumzia jinsi ilivyo kazi kupata mpenzi wa kweli. Dunia sasa imebadilika watu hupenda vitu vingine badala ya kuwa na mapenzi ya kweli yanayojali utu wa mtu. Mwandishi anayaita kuwa hayo ni mapenzi ya ulaghai. Mashairi ya“Utanikumbuka”linaasa juu ya usaliti katika mapenzi kuwa haufai. Shairi la “Kuunge” na“kitendawili”yanakazia zaidi juu ya kuwa na msimamo katika mapenzi.Anafananisha watu wasio na mapenzi ya kweli na Njiwa anayerukaruka asiyetulia. Mwandishi anasema;Umuhimu wa wosia:Suala la kutoa wosia kwa mwanadamu ni jambo la muhimu sana pindi anapokufa. Suala hili huepusha migogoro na malumbano kwa wanafamilia wanaobaki. Katika shairi la “Niniwanangu” anasema:Suala la ukombozi wa kifikra:Mwandishi anaitaka jamii kukomboka kifikra. Mambo haya anayazungumzia katika shairi la “Usiwebendera”. Suala la kuwa na msimamo binafsi na thabiti katika maamuzi ya mambo ni jambo la msingi katika maisha ya kila siku. Anaona kuna athari ya kuendeshwa au kuamuliwa mambo kama bendera inavofuata upepo.Utetezi wa haki.Mashairi ya“Mpaka lini”, “Samaki mtungoni” “Sokomoko”yanazungumzia juu ya ukosefu wa haki. Mahali popote hapawezi kuwa na amani bila kuwepo haki. Hivyo mwandishi anaeleza;Katika shairi la“Samaki mtungoni”mwandishi anaona kuwa kwa sababu ya ukosefu wa hik watu hudhulumiwa na kuteswa anafananisha wadhulumu haki na wavuvi anasema;Utabaka na unyonyaji na unyanyaswaji:Mambo ya matabaka ndiyo yanayochangia kunyanyaswa, kunyonywa na kukandamizwa. Matabaka ambayo waandishi wanayazungumiza ni matabaka ya kiuchumi, kijamii na kisisasa. Katika shairi la“Samaki mtungoni”samaki anachorwa kama mtu mnyonge na mvuvi akiwa ni mwenye mabavu. Anaonesha jinsi watu wasivokuwa na uhuru bali kundamizwa na kuteswa. Hili limewekwa wazi ili kupiga vita mambo hayo katika jami. Anasema;Vilevile katika shairi la“Punda” mwandishi anaelezea jinsi ambavyo watu wa hali ya chini wanavyoendelea kuonewa na kuteswa kama Punda. Anaishauri jamii kukemea suala hili na kusaidiana kuwainua wanyonge na sio kuendelea kuwanyonya.FALSAFAFalsafa ya waandishi wa mashairi ya “Malenga wapya” ni kuwa jamii inaweza kubadilika kiuchumi na kupata maendeleo kama itafanya kazi kwa bidii bila kuzembea, wanaamini kupingwa kwa utabaka na unyonyaji ni suluhu ya amani na maendeleo. Wanaamini pia ukiishi vizuri duniani utafanikiwa, wanasisitiza kutenda wema. Haki usawa na ushirikiano ni chachu ya maendeleo.MTAZAMOMtazamo wa waandishi ni wa kiyakinifu kwani mambo wanayoyaeleza kama vile namna ya kutatua matatizo katika jamii. Mambo wanayoyapendekeza yanawezekana kutimizika mfano uwepo wa haki, kupinga utabaka, unyonyaji, kufanya kazi vizuri kuweka akiba na matumizi mazuri ya pesa na mambo mengine mengi.MSIMAMOMsimamo wa kimpinduzini msimamo wa waandishi wa diwani hii. Mambo wanayoyaeleza yanalenga kuleta mapinduzi katika jamii mfano kupiga vitu adui uvivu, kupinga dhuluma, kupinga maovu yote. Hiyo ni ishara kuwa wanalenga kuibadilisha jamii. Wanatoa pia changamoto na suluhu ya matatizo katika utekelezaji wa mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika jamii kama vilekufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili.UJUMBEKufanya kazi kwa bidii ni chachu ya mendeleo.Uaminifu katika ndoa, mapenzi ya kweli ni jambo lamsingi.Matumizi mazuri ya pesa husaidia kuwa na akiba nzuri na kupunguza umaskini usio na tija.Kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi, si budi kukithamini.Kauli nzuri huepusha migogoro na chuki.Kumkomboa mwanamke ni kuikomboa jamii, hivo si budi kupinga tamaduni zinazomkandamiza.Tunaaswa kupinga utabaka.Kutetea haki na kupuuza unyonyaji ili kuleta usawa katika maisha.Viongozi walaghai na wasaliti hawafai kwa maendeleo hivyo tunaaswa kuwa makini kuchagua vingozi bora na kuwawajibisha wasiofaa.Docs: 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18Tagged:Form 3kidato cha tatuKiswahili Topic - Previous Maendeleo Ya Kiswahili Next - Topic Utungaji Wa Kazi Za Fasihi Andishi