Topic Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi Estimated reading: 96 minutes 982 views Summary: Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.Maudhui katika Riwaya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha UzembeHakiki maudhui katika Riwaya ya Ngoswe Penzi Kitovu cha UzembeDHAMIRASuala la kuchanganya kazi na mapenzi:Mhusika Ngoswe ambaye alitumwa na serikali kwenda kufanya zoezi la sensa la sensa kijijini anajiingiza katika mapenzi na binti Mazoea uk.5 na hivyo kusababisha kutokuwa makini na kazi yake. Anaamua kutoroka na Mazoea jambo ambalo linamfanya Mzee Mitomingi ateketeze karatasi za takwimu kwa kutoroshewa mwanae uk.28. hivyo tunaona jinsi mapenzi yallivyohaaribu kazi.Suala hili ni halisi katika jamii yeetu ya leo kwani watu wamekuwa wakijisahau na kuchanganya kazi na mapenzi, mwandishi ameliweka jambo hili wazi ili jamii iweze kubadilika na kuacha tabia hiyo mbaya inayodidimiza maendeleo ya jamii.Hasara za ulevi:Suala la ulevi na hasara zake limejadiliwa na mwandishi akiwachora wahusika kama Ngoswe na Mzee Mitomingi na wanakijiji ambao ni walevi. Mfanouk.6 Mzee Mitomingi anasema “haya matatizo yote ni shauri ya pombe, sina shaka yuko kilabuni”.Ngoswe naye anapata hasara kutokana na ulevi kwani analewa sana na kuchoma karatasi za takwimu na kusababisha kuhesabu upya watu tena jamo ambalo lilipoteza mda zaidi.uk.18-19.Katika jamii yetu suala laulevilina hasara kubwa kama vile kurudisha nyuma suala zima la maendeleo, kusababisha vifo na ajali, migogoro ya kifamilia na matatizo mengine mengi. Jamii inaaswa kujirekebisha na kukemea suala hili kwani lina madhara makubwa katika koizazi cha sasa.Umuhimu wa elimu:Wanakijiji wa kijiji cha Mzee Ngengemkeni hawana elimu na wala hawatilii maanani juhudi za kupata elimu. Huduma za kielimu ni mbovu kama vile shule iko mbali sana hazipo kijijini kwao. Familia nyingi na watoto wao hawasomi. Uk.16. zoezi la uhesabuji watu linakuwa gunu zaidi kuutokana na watu kutokuwa na elimu.Ili kupata maendeleo katika jamii yoyote ile si budi suala la elimu kupewa kipaumbele na wanaoelimika wanapaswa kutumia vyema elimu yao. Wanapaswa kurejesha mchango chanya katika jamii na sio kurudisha nyuma maendeleo.Mfano Ngoswe ambaye hakutumia vizuri elimu yake. Elimu lazima itumike kuibadilisha jamii na kusukuma mbele zaidi maendelo.Suala la umaskini:Wanakijiji wanaelezwa kuwa na maisha duni sana ya hali ya chini, makazi duni. Mfano wanalala kwenye vibanda vibovu mfano Ngoswe anakaribishwa kulala katika moja ya kibanda kibovu kinaachovuja. Mwandishi amelionesha hilo makusudi kwani maeneo mengi ya mijini yamesahaulika na bado wapo nyuma kimaendeleo. Serikali iangazie maeneo ya vijijini na kutoa elimu ya namna ya kupambana na umaskini, kujenga makazi bora. Pia wanakijiji wanaaswa kuacha uvivu na kujishughulisha ili kumpinga adui maskini.Suala la malezi na ndoa za mitara:Wanakijiji wa Balozi Mitomingi wana utamaaduni wa kuoa mke zadi ya mmoja. Pia suala la malezi si la baba bali la mama pekee. Mzee Mitomingi aliwaachia wakeze suala la kulea watoto na kuwa watazamaji wa familia, hali kadhalika Mzee Jimbi mda wote alishinda kilabuni kwenye pombe na hakuwa na mda wa kufanya kazi yoyote ya kimaendeleo wala kuangalia familia suala hilo aliwachia wake zake. Hili si jambo zuri.Kuhusu ndoa za mitara kwa jamii ya leo zina athari kwanikatika malezi ni vigumu kumudu ukubwa wa familia, usalama wa kiafya huwa ni mdogo kwani wanandoa wana hatari kubwa ya kuambukizana magonja hatari.Imani potofu na ushirikina:Uk.14 tunaona wanawake wanakataa zoezi la kuhesabiwa kutokana na imani kuwa mtu anayehesabu watu ni mchawi. Kutokana na hili, zoezi la uhesabuji watu linakuwa gumu.Wanaamini kuwa mtu akifa basi amerogwa. Mfanouk.16 “wamemroga bure mume wangu. alikufa akiwa na nguvu zake”.Mambo mengine ya kimaendeleo hushindikana kutokana na imani potofu wanazoshikiliawanajamii. Mwandishi amelionesha ili jamii ijikomboe kutoka katika imani hizo potofu. Pia anaona upo umuhimu wa serikali kuelimisha jamii juu ya hili, kuacha kushikilia ukale na kuchangamkia maendeleo.Utabaka kati ya mjini na vijijini:Katika tamthiliya hii suala la utabaka kati ya mjini na vijijini. Kuna tofauti kubwa kati ya mjini na vijijini katika masuala ya huduma za jamii kama vile elimu, afya na mengineyo. Uk.29 Ngoswe anasema:“Shurti vijiji kurekebishwa,Ujinga, magonjwa naUmaskini kupigwa vita,Na njia ni moja tu!Kuishi pamoja kijamaa.”Hivyo mwandishi amelionesha jambo hili ambalo linahalisika katika jamii yetu ya leo, hivyo si budi serikali kulitazama jambo hili kwa jicho pevu. Teknolojia na mawasiliano yaboreshwe kwani ni msingi wa maendeleo.Nafasi ya mwanamkeTamthiliya ya Ngoswe imemchora mwanamke katika sura zifuatazo:Kama mlezi na muangalizi wa familia:Mama Mazoea na mama Inda na akina mama wengine ni waangalizi wa familia.Kama chombo cha starehe:Wanaume wameonekana kuwatumia wanawake kwa ajili ya starehe. Hii inathibitishwa na tabia ya kuoa mitara.Kama kiumbe duni asiyeweza kutoa maamuzi yoyote ndani ya jamii yake: Mfano Mitomingi anasemauk.26 “nyie wanawake akili zenu wote sawa si Mazoea si mama yake….”Jamii inashauriwa kumpa mwanamke nafasi na kumthamini hasa katika masuala ya uamuzi.Kama mtu asiye na msimamo: Mfano ni Mazoea ambaye anaamua kutoroka na Ngoswe huku alijua ametolewa mahari.MIGOGOROMgogoro kati ya Ngoswe na Mzee Mitomingi: Mgogoro huu unatokea baada ya Ngoswe kuamua kumtorosha binti wa Mitomingi. Mitomingi anaamua kuchoma moto karatasi za takwimu.Mgogoro baina ya Mazoea na wazazi wake: Sababu ya mgogoro ni Mazoea kujihusisha na mapenzi na kutoroka na Ngoswe hali akijua alishatolewa mahari. Baba yake alimuadhibu kwa kumchapa.Mgogoro kati ya Ngoswe na serikali: Sababu ya mgogoro ni kutokana na Ngoswe kushindwa kupeleka hesabu ya watu kama alivyoagizwa. Uk.28-29.Mgogoro wa nafsi wa Ngoswe. Ngoswe alisononeka na kuwaza kuwa angejibu nini serikalini kwani karatasi za takwimu ziliteketea kutokana na uzembe wake.FALSAFA: Imani ya mwandishi anaamini kuwa mabadiliko na maendeleo katika jamii yanawezekana kama watu watajishughlisha na pia kama serikali itagawanya vyanzo vya maendeleo bila ubaguzi nchini. Pia anaamini kuwa jamii inaweza kuingia matatizoni kama itachanganya mambo mawili kwa pamoja. Hivyo anashauri watu kuheshimu na kushikilia jambo moja ndipo utafanikiwa.MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu kwani anayaona mambo kiyakinifu, anaona kuwa kufanya kazi kwa bidii, kuheshimu kazi, kuwa na msimamo katika maisha ni suluhisho na chachuya maendeleo.MSIMAMO: Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi kwani anapingana na mambo mabaya na kuyaweka wazi mfano uvivu, uzembe, kuchanganya kazi na mapenzi. Pia anapinga suala la ushirikina na imani potofu. Anaona kuwa ipo haja jamii kuwa na msimamo wa kimapinduzi kwa kupinga mambo yanayodidimiza maendeleo.UJUMBESi vyema kuchanganya kazi na mapenzi kwani husababisha kazi kuharibika.Ulevi huleta madhara na matatizo ndani ya jamii hivyo si budi jamii kupinga ulevi.Elimu ni muhimu sana kwa jamii yoyote.Kufanya kazi kwa bidii ni msingi wa maendeleo.Wanawake wanapaswa kupewa nafasi ya kufanya maamuzi katika jamii.Serikali na jamii vinapaswa kugawanya maendeleo sehemu zote za vijijini na mijini ili kuwa na maendeleo yasiyopishana sana ili kufifisha umaskini uliokithiri.Wanaume wanaowavuruga wasichana kwa tamaa zao ipo siku watafikia tamati na kupata machungu ya ubaya wao.Msimamo katika maamuzi ya mambo na kufikiri kabla ya kutenda ni jambo la msingi.Nidhamu ya woga haijengi.Docs: 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18Tagged:Form 3kidato cha tatuKiswahili Topic - Previous Maendeleo Ya Kiswahili Next - Topic Utungaji Wa Kazi Za Fasihi Andishi