Topic Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi Estimated reading: 96 minutes 532 views Summary: Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.Maudhui katika Riwaya ya Joka la MdimuHakiki maudhui katika Riwaya ya Joka la MdimuDHAMIRAUgumu na hali ngumu ya maisha:Suala la ugumu wa maisha limejadiliwa katika riwaya hii kwa kiasi chake. Mwandishi ameonesha jinsi wananchi wanavyopata shida ya vyakula, mavazi nk. Yote haya yakisababishwa na mfumuko wa bei za bidhaa kutokana na uhaba wa bidhaa. Mfano. Uk.1“jiji la Mindule lilikabiliwa na uhaba mkubwa mno wa petroli, dezeli na mafuta ya taa nyumba nyingi zisizo na umeme zilibaki kiza usiku maana mishumaa ilikuwa ghali na adimu kupatikana, usafiri ulisimama isipokuwa kwa wale wachache waliojua mbinu za kupata dizeli na petrol”.Mwandishi ameonesha jambo hili ambalo linaakisi maisha ya hali ya kiuchumi miaka ya 80, ambayo kwa upande mwingine inaangazia maisha ya mtanzania wa leo ambapo bidhaa ni nyingi maasokoni lakini tatizo ikiwa ni mfumuko wa bei na upatikanaji mgumu wa fedha.Suala la utabaka:Utabaka uliojadiliwa ni kati ya walionacho na wasionacho (matajiri na maskini). Hili limeoneshwa pale ambapo wananchi wanaishi maisha ya dhiki na makazi duni mfano uk.29 mwandishi anaeleza,“nyumba yenyewe ya Tino ilikuwa bondeni juu tu kidogo ya mtaro mkubwa uliokuwa ukipitisha maji machafu”.Hii inatuonesha wazi hali mbaya ya makazi ya Tino na wakazi wengine, wakati hawa maskini wakiteseka na kuhangaika hata katika suala la huduma za kijamii kama matibabu ya gharama kubwa, matajiri wao walinufaika kwa kuwa na fedha nyingi, mali za kujilikimbikizia na za magendo. Mfano uk. 103 – 104 mwandishi anaeleza kuhusu makazi au nyumba ya Brown“ilisimama na kuzibeza nyumba zote jirani na hapo kwa haiba yake na bwawa lake la kuogelea”.Ufisadi: Suala la ufisadi limeoneshwa na mwandishi kwani amejadili kuhusu viongozi ambao wanahujumu mali za umma kwa maslahi yao binafsi, viongozi mfano wafanyakazi wa serikali kama vile Brown Kwacha amechorwa kuwa ni mtumiaji mbaya wa mali za umma, anasafiri safari za nje kwa pesa nyingi za serikali na kwa matumizi binafsi. Licha ya hivyo anafanya biashara ya magendo na pesa za kigeni katika ofisi yake. Alimudu kujenga nyumba za kifahari kwa pesa za serikali. Mfanouk.102“gharama ya nyumba iliyokuwa ikijengwa na Wafaransa ilikuwa shilingi milioni mia mbili na nusu na ile nyingine milioni mia tatu”.Hizi ni pesa nyingi ambazo zote alizichukua serikalini.Hili ni tatizo kubwa kwa jamii yetu ya leo. Viongozi wetu wa serkali wanatumia pesa vibaya za serikali kwa manufaa binafsi, hivyo kusababisha umaskini usioisha kwa Watanzania wa hali ya chini. Mwandishi amelionesha hili ili wanaohusika wabadilike.Biashara haramu na uharibifu wa mali za taifa:Suala hili limejadiliwa katika riwaya hii. Mhusika Brown ambaye ni mfanyakazi wa serikali anajihusisha na biashara za magendo mfano uuzaji na uwindaji wa wanyama na kuchukua pembe, ngozi na meno. Mfano uk.122-123 muwindaji kinara wa Brown anasema“sawa ziko pembe ishirini za faru na sitini za ndovu, unaweza kuzichukua zote maana vitu hivi ni hatari”.Wanyama muhimu katika hifadhi za taifa wanazidi kupungua na kutoweka kabisa kutokana na biashara hii. Mwandishi ameliangazia ili mamlaka husika na jamii viweze kuweka mikakati na sheria madhubuti za kuangamiza suala hili kwani hupelekea nchi kuendelea kuwa maskini.Rushwa na kutowajibika:Mambo ya hongo na rushwa na kutowajibika kwa viongozi ambao wamepewa mamlaka na wananchi ili wafanye kazi kwa maslahi ya taifa yamejadiliwa. Mfano mhusika Brown si mfanyakazi bora kwani hakutimiza wajibu wake bali alifanya kazi kwa upendeleo mkubwa bila kujali haki. Alipokea rushwa na kutoa pia. Mfano uk.100 anasema“……lakini Brown Kwacha alikuwa mtu wa nyendo akajua karata gani acheze na ipi aibakishe. Alisema kwa kiburi suala si kupata kiwanja ila mahali panapofaa kuporomoshwa kasri la kifahari”. Hivi ndivyo hali ilivyo, wenye uwezo wa kutoa rushwa ndio waliopatiwa huduma haraka. Pia anatuonesha jinsi Brown Kwacha alivyofanya kazi kwa upendeleo uk.97 mwandishi anasema “katibu wa Brown Kwacha alimtazama mkuu wake wa kazi akastaajabia namna alivyoweza kukaidi kuwahudumia wengine ila alivyolainika mbele ya wasichana kama jani la mboga au bufalo ndani ya maji.” Suala hili ni tishio kwa Wananchi kwani hupoteza wa haki, mwandishi anakemea suala hili vikali, na viongozi wanashauriwa kuenenda kwa mujibu wa maadili ya kazi zao.Mapenzi: Mapenzi aliyoyajadili mwandishi katika riwaya hii ni ya sura mbili tofauti.Mapenzi ya dhati;Hili limeoneshwa na mhusika Amani kwa rafikiye Tino, kwani alibeba suala la Tino kuuguliwa na mwanae kama lake, alimsaidia katika shida na raha, hakumuacha peke yake mfano uk.145. mwandishi anasema Tino akawaza“akawaza dunia hii ya leo nani atajitoa kwa hali na mali kumsaidia kapuku kama yeye. Nitamlipa nini Amani?”hii inaonesha fadhila alizokuwa nazo Amani. Pia mapenzi ya dhati yameoneshwa kwa Tino kwa mwanae Cheche na familia yake. Tino aliipenda sana familia yake hata kuhangaika kwa hali na mali kumtibu mwanae Cheche kwa kila gharama kwani alidiriki kuiba fedha benki ili amudu kumpeleka mwanae nje kwa ajili ya matibabu. Mwandishi anatufundisha kuwa na mapenzi ya dhati kwani ni ishara ya mafanikio na amani. Kwa upande wa pili amejadili juu ya mapenzi yasiyo ya dhati au ya kweli. Mhusika Brown amechorwa kutokuwa na mapenzi ya dhati na kukosa uaminifu kwa mkewe na watoto kwani ni muhuni sana. Alikuwa na mahusiano ya mapenzi na wanawake wengi hakujali familia yake kabisa. Hakuonesha hata chembe ya upendo kwa familia yake. Mfano uk.109“mabinti zake walitamani sana kusafiri na baba yao. Lakini licha ya safari zake nyingi mno hawakupata fursa hiyo.”Pia uk.106 anasema watoto walikosa upendo“walitapia mno, lau kungekuwa na maelewano na upendo mkubwa baina ya baba na mama yao!fauka ya hayo baba yao alikuwa mkali”.Pia mapenzi yasiyo ya uaminifu kwa Brown na wapenzi wake kama vile Leila, Josephine. Mapenzi haya yalikuwa ya pesa tu! Uk 112 mwandishi amemzungumiza Leila “badala ya kumfikiria zaidi Brown Kwacha akatarajia zaidi faraja kuangalia nwanyama kwenye hifadhi ya Kwale”.Piauk.99Josephine anaomba fedha kwa Brown“.. cha kutosha kununua vitu vya harusi kama paundi alfu sita hivi”Mapenzi yasiyo ya dhati na ukosefu wa uaminifu katika ndoa ni janga katika jamii za sasa kwani wazazi hujisahau na kukiuka maadili ya ndoa jambo ambalo ni hatari mno kwani husababisha migogoro na ugomvi katika familia (mafarakano) na hata kuambukizana magonjwa hatari.Nafasi ya mwanamke katika jamiiAmechorwa kama chombo cha starehe: Mfano ni Josephine na Leila, Brown Kwacha aliwatumia kujiburudisha kwa uasherati, pia wanawake walijiuza katika moja ya sehemu ambazo Amani alipenda kwenda.Amechorwa kama kiumbe mwenye upendo: Mwema mke wa Tino ni mwanamke ambaye alikuwa na upendo wa dhati kwa mumewe na watoto kutokana na matunzo aliyowapa.Amechorwa kama mlezi: Mfano mzuri ni Mwema na mke wa Brown ambaye yeye alikuwa ndiye mwangalizi mkuu wa familia kwani mumewe hakuwa na muda huo zaidi ya kuponda starehe na anasa kwa mda wa ziada aliopata badala ya kukaa na familia yake.Amechorwa kama mtu mvumilivu: Mke wa Brown alivumilia sana mateso ya mmewe, hakuamua kumuacha bali alivumilia pamoja na kumdharau kote, kumdunisha na kutomthamini kama mke.Amechorwa kama kiumbe duni: Brown hakumshirikisha mkewe katika maamuzi yoyote yale wala hakutaka ushauri wowote kutoka kwake alimdharau na kumpuuza tu.Kama mtu jasiri na mwenye msimamo: Pamela anaoneshwa kuwa ni mwanamke jasiri kwani aliweza kumkataa Brown kimapenzi pamoja na vishawishi vya kila aina. Mfano uk.99 mwandishi anasema“lakini Pamela kama mwanariadha stadi, aliviruka viunzi vyote vya Kwacha…… mwanzo alimchukia lakini taratibu alianza kumheshimu”.MIGOGOROMwandishi Safari pamoja na kujenga visa vyake vya kusisimua pia hakuacha kuibua migogoro ili kukamilisha masimulizi ya visa vyake.Mgogoro baina ya pande mbiliMgogoro baina ya Josephine na mke wa Brown: Sababu ya mgogoro huu ni Josephine kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi na Brown Kwacha na kufumaniwa na mke wa Brown. Walipigana na kuumizana lakini Josephine hakuacha mahusiano hayo.Mgogoro kati ya wafanyakazi wawili wasukuma makwama: Sababu ya mgogoro huu waligombaniana matenga ya kubeba na mwishowe kuishia kupigana.Mgogoro baina ya Jinja Malon na vibaka: Jinja Malon aliwapiga vibaka baada ya kutaka kumkwapulia mwanamke mmoja hereni, mkufu na hata kutaka kumbaka kichochoroni. Uk 51-52.Mgogoro kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya mila na utamaduni na kijana mmoja: Walipigana kugombania mwanamke ambaye alikuwa na mahusiano na wanawaume wote wawili. Uk.102.Mgogoro wa nafsi wa TinoTino alisumbuliwa na mgogoro wa nafsi kutokana na hali ya ugonjwa wa mwanae Cheche. Hakujua apate wapi pesa za kumtibia kwani hakuwa na pesa na alitakiwa kupelekwa nje kwa ajili ya matibabu. Lakini baada ya kushauriwa na Amani akaibe pesa alifanya hivyo na kufanikiwa na ndipo alipata amani baada ya kumudu gharama za matibabu ya mwanae.FALSAFA: Mwandishi anaamini kuwa chanzo cha matatizokatika jamii ni upotofu wa maadili, kutowajibika, mifumo mibovu ya uchumi, rushwa, ufisadi na biashara haramu na mengine mengi. Anaamini kuwa endapo jamii itabadilika basi hayo matatizo hayatakuwepo. Anatoa suluhu ya matatizo hayo kama vile kupinga utabaka, rushwa, matumizi mabaya ya mamlaka na kuwa na usimamizi mzuri wa mali za umma.MTAZAMO: Mtazamo wa mwandishi ni wa kiyakinifu. Ameonesha matatizo ndani ya jamii na kuonesha suluhu ya matatizo hayo. Anaonesha matatizo ya uhujumu uchumi, ufisadi, kutowajibika kwa viongozi, ukosefu wa huduma za jamii, matabaka na hali ngumu ya maisha. Anaona kuwa sababu ya matatizo haya si ya kidhanifu tu au ni mipango ya Mungu tu! Ila anonesha sababu za matatizo hayo kama vile kukithiri kwa rushwa, mifumo mibaya ya kiuchumi na anatoa suluhu kwa kuwapiga vita viongozi wasowajibika. Mifumo mibovu ya uchumi inayoendelea kutengeneza utabaka katika jamii.MSIMAMO: Mwandishi A. Safari ana msimamo wa kimapinduzi, hili linajidhihirisha wazi kutokana na mambo anayoyaeleza ambayo yanalenga kuibadili jamii. Analeta mapinduzi kwa viongozi wasiowajibika, mifumo mibovu ya uchumi inayoendelea kusababisha umaskini na kuwakweza wachache.Anatoa suluhu ya matatizo mbalimbali. Anakemea malezi mabaya kama ya Brown pia anasa na starehe na mengine mengi.UJUMBEViongozi na watumishi wa umma wanapaswa kuwajibika kulingana na majukumu yao.Rushwa, ufisadi na biashara za magendo ni vikwazo vya maendeleo hivyo si budi kupigwa vita.Serikali na mamlaka husika vinapaswa kusimamia vyema sheria na taratibu ili kuwawajibisha wanaoenda kinyume kama vile wahujumu uchumi.Uaminifu katika ndoa na mapenzi ya dhati ni jambo la msingi kwani huongeza Amani katika familia.Jamii inapaswa kutambua nafasi ya mwanamake na kumshirikisha na sio kumdunisha bali apewe nafasi ya kuamua na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaedeleo.Docs: 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18Tagged:Form 3kidato cha tatuKiswahili Topic - Previous Maendeleo Ya Kiswahili Next - Topic Utungaji Wa Kazi Za Fasihi Andishi