Topic Uandishi Wa Insha Na Matangazo Estimated reading: 3 minutes 106 views Uandishi wa Insha za KisanaaMisingi ya Kuandika InshaElezea Misingi ya Kuandika InshaInsha za kisanaa ni insha zinazoelezea mambo ya kawaida katika jamii lakini kwa kutumia lugha ya kisanaa. Lugha ya kisanaa inajumuisha matumizi ya tamathali za semi, misemo, nahau, methali, na taswira.Muundo wa InshaKwa kawaida, insha ina sehemu kuu nne: kichwa cha insha, utangulizi, kiini, na hitimisho.Kichwa cha InshaHudokeza kile utachokijadili katika insha yako na hubainisha wazo kuu la mada inayohusika.Kichwa cha insha huandikwa kwa sentensi fupi. Mfano: “Maisha ya Kijijini,” “Mimba za Utotoni.”UtanguliziUtangulizi unajumuisha kutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako.Unapaswa kuwa katika aya moja fupi.Kiini cha InshaKiini kina maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha yako.Maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.HitimishoHitimisho lina muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au msimamo juu ya kile kilichojadiliwa katika insha.Insha za KisanaaInsha ya kisanaa hutumia lugha ya kisanaa yenye tamathali za semi kama vile sitiari, tashbiha, taniaba, na mubalagha. Pia hutumia mbinu nyingine za kisanaa kama tashititi, takriri, na tanakali sauti. Insha za kisanaa zina lugha yenye mvuto na misemo kama nahau, methali, na tamathali za semi.Uandishi wa MatangazoTangazo ni taarifa za wazi zinazotoa ujumbe fulani kwa walengwa wanaohusika na ujumbe huo. Ujumbe unaweza kuwa na lengo la kushawishi, kuarifu, kuelekeza, na kadhalika.Vipengele vya Kuzingatiwa katika Uandishi wa MatangazoKichwa cha HabariKichwa cha habari kinasaidia kujua haraka kuwa tangazo linahusika na kitu gani.Kuonesha Aina ya Bidhaa/HudumaHiki ndicho kiini cha tangazo, ambapo tangazo linaonesha ujumbe uliokusudiwa kufikishwa kwa wahusika. Ujumbe huu unaweza kuwa bidhaa inayotangazwa, huduma inayotolewa, kazi inayotangazwa, au mwaliko.AnwaniTangazo linaonesha mahali ambapo watoa tangazo walipo, yaani ofisi zao zilipo, ambapo wahusika wa tangazo wanaweza kwenda na kuwakuta. Kama ni tangazo la mwaliko, lazima lioneshe shughuli yenyewe itafanyika wapi.Njia za MawasilianoKama ni tangazo la biashara, kazi, au mwaliko, ni muhimu kutoa mawasiliano. Mawasiliano hayo yanaweza kuwa namba ya simu, fax, wavuti (kwa taarifa zaidi), au barua pepe.Mbinu za Uandishi wa MatangazoMatumizi ya PichaMatangazo mengi ya biashara huambatana na picha, ambazo husaidia kumshawishi mteja kuamini kuwa bidhaa ni bora na hivyo ni muhimu kuwa nayo au kuinunua.Matumizi ya Maneno MachacheMatangazo hutumia maneno machache kwa lengo la kutomchosha mlengwa lakini wakati huo huo maneno hayo yana nguvu ya kumshawishi mlengwa.Lugha ya KisaniiManeno ya kisanii katika matangazo huwa ni mepesi kukumbukwa na yanaeleweka kirahisi. Mfano: “Litakuwa ni bonge la shoo,” “Njoo ujinunulie pamba za ukweli.”Matumizi ya Watu MaarufuMatangazo mengi, hususani ya biashara, hupenda kutumia watu maarufu ili kuwashawishi walengwa. Mfano: Tangazo juu ya bidhaa fulani linaweza kumwonesha msanii maarufu, Miss Tanzania, au mchezaji mpira maarufu. Hii inamsaidia mlengwa kushawishika na yeye kuitumia bidhaa hiyo.Tagged:Form 3kidato cha tatuKiswahili Topic - Previous Utungaji Wa Kazi Za Fasihi Andishi Next - Topic Kusoma Kwa Ufahamu