Comment

Darasa Huru

Darasa Huru

Limitless Potential

Education at your fingertips, with no price tag attached.

Topic

Mjengo Wa Tungo

Estimated reading: 8 minutes 84 views

Maana ya Tungo

Tungo

Maana ya Tungo
Tungo ni kipashio cha kisarufi kilichoundwa kwa kuunganisha pamoja vipashio vidogovidogo vilivyo chini yake. Kwa lugha rahisi, tungo ni neno au kikundi cha maneno ambacho hudokeza taarifa fulani, ambayo inaweza kuwa kamili au isiyo kamili.

Kwa maana hii, tungo hujengwa na vipashio vidogovidogo kama vile mofimu kuunda neno, neno kuunda kirai, kirai kuunda kishazi na kishazi kuunda sentensi. Kama tulivyokwisha kuona hapo juu, tungo huanzia neno; rejea aina za tungo.

Aina za Tungo

Tungo Neno
Tungo neno ni tungo ambayo huundwa na vipashio vidogo zaidi ya neno ambayo ni mofimu au fonimu. Mfano: anacheza, kakimbia.

Tungo Kirai
Kirai ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi lakini ambacho hakina muundo wa kiima-kiarifu. Mfano: mtoto mzuri, kiyama chake, bondeni.

Tungo Kishazi
Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho kinaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe.

Kirai na Uainishaji wake

Maana ya Kirai na Uainishaji wake
Dhana ya kirai itaeleweka vizuri kwa kuzingatia sifa zake zifuatazo:

  • Kirai huwa ni kipashio cha kimuundo kisichokamilika; yaani ni kipashio kisichokuwa na muundo wa kiima – kiarifu kama zilivyo sentensi ambazo zinahusisha mtendaji wa tendo na tendo linalotendwa.
  • Kirai huainishwa kimuundo kulingana na neno kuu la kirai husika.
  • Kirai ni tungo, yaani ni aina moja wapo ya tungo, aina nyingine za tungo ni neno, kishazi, na sentensi.
  • Kirai hudokeza maana, lakini maana hiyo si kamili.
  • Maneno katika kirai lazima yapangwe kimantiki kwa mpangilio unaokubalika katika sarufi ya lugha husika.

Japo virai huainishwa kimuundo, huweza kutumika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi. Kirai huweza kutokea upande wowote, wa kiima au kiarifu katika sentensi. Kirai ni kikubwa kuliko neno.

Kama tulivyobainisha hapo juu, aina ya virai hukitwa katika aina za maneno ambazo ndizo chimbuko la mahusiano maalumu ndani ya vipashio hivyo.

Aina za Virai

  • Kirai Nomino (KN): Ni kirai ambapo neno lake kuu ni nomino. Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa kwenye nomino au mahusiano ya nomino na neno au mafungu ya maneno.
  • Kirai Kitenzi (KT): Kirai-kitenzi ni kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi au katika mahusiano ya Kitenzi na neno au mafungu mengine ya maneno. Hii ina maana kuwa neno kuu katika aina hii ya virai huwa ni kitenzi.
  • Kirai Kivumishi (KV): Kirai-kivumishi ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika kivumishi. Kwa kawaida muundo huu huwa ni wa kivumishi na neno au fungu la maneno linaloandamana nacho.
  • Kirai Kielezi (KE): Tofauti na aina nyingine ya virai, miundo ya virai vielezi haielekei kukitwa kwenye mahusiano ya lazima baina ya neno kuu (yaani kielezi) na neno au fungu la maneno linaloandamana nalo. Badala yake, miundo inayohusika hapa ni ya maneno ambayo hufanya kazi pamoja katika lugha kama misemo, neno au maneno yanayofuata neno lililotangulia yakifafanua zaidi neno hilo.
  • Virai Viunganishi (KV): Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina ya kwa na katika, au kwenye na fungu la maneno linaloandamana nacho. Kwa maneno mengine, kirai hicho ni kile ambacho neno kuu ni kiunganishi.

Tungo Kishazi

Maana ya Kishazi na Uainishaji wake
Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho kinaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe.

Sifa za Kishazi

  • Kishazi hupatikana ndani ya sentensi.
  • Lazima kishazi kiwe na kitenzi, sehemu yoyote ya sentensi isiyo na kitenzi haiwezi kuwa kishazi.
  • Kishazi huru hutawaliwa na kishazi kikuu na kishazi tegemezi hutawaliwa na kishazi tegemezi.
  • Baadhi ya vishazi huweza kujitegemea kama sentensi hata vikiondoshwa katika muktadha wa sentensi kuu. Kishazi kinachoweza kujisimamia kama sentensi huitwa kishazi huru kikiwa ndani ya sentensi kuu na huitwa “sentensi sahili” kikiwa sentensi inayojitegemea.
  • Baadhi ya vishazi haviwezi kujitegemea kama sentensi ikiwa vitaondoshwa katika muktadha wa sentensi kuu.
  • Vishazi vingi, hata vishazi huru, huwa na kiima dhahiri.
  • Kishazi kwa kawaida, hasa kishazi huru, huwa na kitenzi kimoja kikuu.
  • Kitenzi hicho huweza kuandamana na kitenzi kisaidizi. Pia, kitenzi katika kishazi huweza kuwa kitenzi kishirikishi.
  • Kishazi hutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi.

Tofauti ya kishazi na sentensi ni kwamba kishazi hupatikana ndani ya sentensi lakini sentensi hujisimamia kimuundo na kimaana. Kishazi huwa na kiarifu kimoja na kiima kimoja, lakini sentensi huweza kuwa na kiima kimoja.

Aina za Vishazi

  • Vishazi Huru: Kishazi huru ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kikuu, ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe kamili usiohitaji maelezo zaidi ya kukamilisha maana. Ni kishazi ambacho hata kikiondolewa katika muktadha wa sentensi ambamo vimejikita, huweza kujitegemea kama sentensi.
  • Vishazi Tegemezi: Kishazi tegemezi ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kisaidizi, ambacho muundo wake hukifanya kutegemea kitenzi cha kishazi huru ili kuweza kutoa ujumbe uliokusudiwa. Kishazi tegemezi peke yake hakitoi ujumbe unaojitosheleza.

Sifa za Kishazi Tegemezi

  • Kishazi tegemezi hutoa maana kamili kinapoandamana na kishazi huru.
  • Kishazi tegemezi kinaweza kufutwa katika sentensi bila kuharibu maana ya sentensi nzima.
  • Kishazi tegemezi hutambulishwa na viambishi vya utegemezi vinavyoambatanishwa kwenye kitenzi.
  • Kishazi tegemezi vile vile kinaweza kutambuliwa kwa kuwepo vishazi kama vile ingawa, kwamba, ili, kwa sababu, mzizi wa amba, mofimu ya masharti n.k.

Aina za Vishazi Tegemezi

  • Vishazi tegemezi vivumishi
  • Vishazi tegemezi vinavyotokea pamoja na nomino inayovumishwa
  • Vishazi tegemezi visivyoambatana na nomino inayovumishwa
  • Vishazi tegemezi vielezi
  • Vishazi tegemezi vya mahali
  • Vishazi tegemezi vya wakati
  • Vishazi tegemezi vya namna au jinsi
  • Vishazi tegemezi vya masharti
  • Vishazi tegemezi vya hali, hitilafu au kasoro iliyoko katika tendo
  • Vishazi tegemezi vya sababu/chanzo

Dhima na Hadhi ya Vishazi

Kishazi chaweza kuwa huru kikajitegemea chenyewe kwa kuwa na maana kamili inayojitosheleza. Lakini kuna vishazi ambavyo havijitoshelezi vyenyewe, bali hutegemea vishazi vingine. Kishazi huru kina hadhi ya sentensi (sahili). Kishazi tegemezi hakina hadhi hii; vishazi tegemezi ambavyo hutegemea vishazi vingine hushuka daraja na kuchukua dhima ya kikundi. Baadhi ya vishazi tegemezi huchukua dhima (hufanya kazi) ya kivumishi katika tungo ambayo kwa kawaida ni dhima ya kikundi au neno. Vishazi hivi huvumisha nomino katika tungo hiyo.

Ufafanuzi wa Aina za Tungo

Sentensi

Maana ya Sentensi

Sentensi ni kifungu cha maneno kuanzia neno moja na kuendelea chenye muundo wa kiima na kiarifu na kinacholeta maana kamili.

Sifa za Sentensi

  1. Mpangilio wa Maneno: Sentensi lazima iwe na mpangilio wa maneno unaokubalika na wazungumzaji wa lugha husika.
  2. Ukamilifu: Sentensi lazima ikamilike kimaana, kimuundo, na kisarufi.
  3. Muundo: Sentensi huwa na muundo wa kiima na kiarifu, ikiwa na kirai nomino na kirai kitenzi.
  4. Kitenzi Kikuu: Sentensi inaweza kuwa na kitenzi kikuu kimoja au zaidi.
  5. Kishazi: Sentensi inaweza kuundwa na kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi.
  6. Hali Mbalimbali: Sentensi huonyesha hali mbalimbali kama vile amri, ombi, mshangao, na swali.

Muundo wa Sentensi

Kimapokeo/Kikazi/Kidhima

  1. Kiima: Sehemu inayojaza nafasi ya mtenda au mtendwa wa jambo.
  2. Kiarifu: Sehemu inayojaza maneno yanayoarifu tendo lililofanywa, linapofanywa, au litakapofanywa.

Vipashio vya Kiima

  • Nomino peke yake
  • Nomino na kiunganishi
  • Nomino na kivumishi
  • Kivumishi na nomino
  • Kiwakilishi peke yake
  • Kiwakilishi na kivumishi
  • Nomino na kishazi tegemezi vumishi
  • Kitenzi jina
  • Nomino na vivumishi zaidi ya kimoja
  • Kitenzi jina na nomino
  • Umbo kapa

Taarifa zitolewazo na Kiarifu kuhusu Kiima

  • Kiima ni nani
  • Kiima kina nini
  • Kiima hufanya nini
  • Kiima kinahisi nini

Sifa za Kiarifu

  • Huwa na kitenzi na pengine huambatana na maneno mengine.
  • Kwa kawaida huja baada ya kiima.

Vipashio vya Kiarifu

  • Kitenzi kikuu peke yake
  • Kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu
  • Kitenzi kishirikishi na kijalizo

Aina za Sentensi

Sentensi Sahili

  • Maana: Huundwa na kishazi huru kimoja na inaelezea taarifa moja tu.
  • Mfano: Wanafuzi wanafanya mtihani.
Miundo ya Sentensi Sahili
  1. Kitenzi kikuu peke yake. Mfano: Gari limeanguka.
  2. Kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi. Mfano: Mgosiyuda alitaka nisipate utajiri.
  3. Vira-vitenzi vilivyokitwa katika kitenzi ‘kuwa’. Mfano: John amekuwa akiangalia TV kwa muda mrefu sana.
  4. Kitenzi shirikishi. Mfano: Kiswahili ni tunu ya Taifa.

Sifa za Sentensi Sahili

  • Ina kiima ambacho kimetajwa wazi au kimeachwa kutajwa.
  • Ina kiarifu chenye kitenzi kikuu kimoja, kitenzi kisaidizi, kitenzi kishirikishi, kijalizo na chagizo.
  • Inajitosheleza kimuundo na kimaana.

Sentensi Changamano

  • Maana: Ina kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi.
  • Mfano: Gari lililopinduka jana jioni halikuharibika hata kidogo.

Sentensi Ambatano

  • Maana: Inajengwa na sentensi mbili au zaidi zilizounganishwa kwa viunganishi kama vile lakini, wala, au, na.
  • Mfano: Mwalimu anafundisha wakati wanafunzi wanapiga kelele.
Miundo ya Sentensi Ambatano
  1. Sentensi sahili tu. Mfano: Mwalimu anafundisha wakati wanafunzi wanapiga kelele.
  2. Sentensi sahili na changamano. Mfano: Walinzi waliposhindwa, polisi waliwasaidia lakini hawakuweza kuwakamata majambazi.
  3. Sentensi changamano tu. Mfano: Barabara zilizojengwa na wakoloni zimedumu hadi leo wakati zile zilizojengwa na Wachina hata mwezi hazifikishi.
  4. Vishazi visivyounganishwa kwa viunganishi.

Uchanganuzi wa Sentensi

Hatua za Uchanganuzi

  1. Kutaja aina ya sentensi: sahili, changamano, au ambatano.
  2. Kutaja sehemu zake kuu: kiima na kiarifu, au kirai nomino na kirai kitenzi.
  3. Kutaja sehemu kuu za kiima na kiarifu au sehemu kuu za kirai nomino na kirai kitenzi.
  4. Kutaja sehemu zote za maneno yaliyomo katika sentensi hiyo.

Njia za uchanganuzi wa sentensi

Njia ya mishale/mistari

Example 1

Uchanganuzi wa sentensi kwa njia ya mishale

Njia ya visanduku/jedwali

Example 2

Mfano

S.S
KNKT
NKHTKN
HKNNKV
NVKE
E
MtuMwenyeUlemavuanachezampiramzurisana

Njia ya matawi

Example 3

Uchaganuzi wa sentensi kwa njia ya matawi

Mifano mingine ya uchanganuzi wa sentensi ambatano;(Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti)

Njia ya jedwali

Example 4

Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti

S.A
S1US2
KNKTKNKT
NKVTKEWT
VE
WatuwengiwalimwaminiSanaLakiniYeyealiwasaliti

Kwa njia ya matawi

Example 5

Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti

Kwa njia ya mishale

Example 6

Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti

Leave a Comment

Share this Doc

Mjengo Wa Tungo

Or copy link

CONTENTS

Agricultural Development

What is Agriculture? Agriculture refers to a fundamental human activity, which i...

Population and Development

POPULATION STUDIES Is the general activities carried out for the purpose of acqu...

Study of Soil

CONCEPT OF SOIL AND SOIL PROFILE Soil appears very complex and thus differe...

Water Masses

GROUND WATER WATER CYCLE Rain falls on the earth surface in filtrates (soaks int...

Topic

The Dynamic-Earth And Consequence

THEORIES THEORY OF ISOSTASY Denudation has been going on the continents where to...

Position Behaviours And Structure Of The Earth

GLOBE Is the model of the earth Earth Is ball of rock partly covered by wat...

Photograph interpretation

Photograph are the true image pictures showing truly appearance of the earth’s...

Maps and map interpretation

What is a map? Map is a scaled conventional representation of the whole or any o...

Simple survey and mapping

INTRODUCTION TO SURVEYING Surveying is an art or a science of measuring and reco...

Field research techniques

Definitions of Research – Research is the systematic investigation into a...

Application of statistics in geography

STATISTICS Statistics is a branch that deals with every aspect of the data. Stat...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel