Topic Maendeleo Ya Kiswahili Estimated reading: 6 minutes 106 views Asili ya KiswahiliUshahidi wa Kimsamiati na Kimuundo unaothibitisha Ubantu wa KiswahiliAsili ya Kiswahili ni mada yenye mjadala mrefu, ambapo wataalamu mbalimbali wanahitilafiana juu ya chimbuko lake. Wapo wanaodai kuwa Kiswahili ni cha Kiarabu, wakati wengine wanashikilia kuwa ni lugha ya Kibantu kwa kutumia hoja za kiisimu na kihistoria.Nadharia Kuhusu Asili ya KiswahiliKiswahili ni KiarabuWanaoshikilia mtazamo huu wanadai kuwa Kiswahili kina maneno mengi ya Kiarabu na kwamba uislamu ulioletwa na Waarabu ndio chanzo cha Kiswahili. Hata hivyo, vigezo hivi vina udhaifu kwa sababu havikukitwa katika misingi ya kitaalamu ya uainishaji lugha.Kiswahili ni Lugha ChotaraMtazamo huu unadai kuwa Kiswahili kimetokana na mchanganyiko wa lugha ya Kiarabu na lugha za Kibantu. Wanaofasili Kiswahili kama lugha chotara wanadai kuwa Waswahili walitokana na wanaume wa Kiarabu na wanawake wa Kibantu.Kiswahili ni Lugha ya VizaliaWaumini wa mtazamo huu wanadai kuwa Kiswahili kilianza kama pijini ya Kiarabu na baadaye kukomaa na kuwa kreoli.Kiswahili ni KikongoNadharia hii inafafanua kuwa Kiswahili ilianzia Kongo na kusambaa katika pwani ya Afrika Mashariki.Kiswahili ni KibantuMtazamo huu unadai kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu na kwamba lugha za Kibantu zilikuwepo hata kabla ya majilio ya wageni kutoka Ajemi, Arabuni, India, China na kwingineko. Huu ndio mtazamo uliopata mashiko zaidi katika karne ya ishirini kutokana na tafiti mbalimbali za isimu, historia, akiolojia, na ethnografia.Ushahidi wa Kiisimu Unaothibitisha Ubantu wa KiswahiliMsamiatiMizizi ya msamiati wa msingi wa lugha za Kibantu na Kiswahili hufanana kwa kiasi kikubwa. Mfano:Kiswahili: Maji, JichoKikurya: Amanche, IrisoKinyiha: Aminzi, IryinsoKijita: Amanji, ElisoMofolojiaMfumo wa maumbo ya maneno ya Kiswahili na lugha za Kibantu hufanana, kama vile namna viambishi vinavyopachikwa katika mzizi wa maneno. Mfano:Kiswahili: A-na-lim-a (analima)Kisukuma: A-le-lem-a (analima)Kisimbiti: A-ra-rem-a (analima)Kinyiha: I-nku-lim-a (analima)SintaksiaMpangilio wa maneno katika sentensi za Kiswahili na lugha za Kibantu hufanana. Mfano:Kiswahili: Mama anakulaKijita: Mai kalyaKihehe: Mama ilyaKihaya: Mama nalyaFonolojiaMfumo wa sauti wa lugha za Kibantu hufanana na ule wa Kiswahili, ambapo silabi huishia na irabu na si konsonanti. Mfano:Kiswahili: BabaKikurya: TataKiha: DataKijita: RataKipare: VavaNgeli za MajinaMfumo wa ngeli za majina katika Kiswahili hufanana sana na ule wa Kibantu, hasa katika upachikaji wa maumbo ya umoja na wingi. Mfano:Kiswahili: M-tu, Wa-tuKikurya: Mo-nto, Abha-ntoKiha: Umu-ntu, Abha-ntuKikwaya: Mu-nu, Abha-nuUshahidi wa Kihistoria, Kiakiolojia na KiethinolojiaUshahidi wa kihistoria unachunguza masimulizi na vitabu vya kale ambavyo huelezea asili na chimbuko la wakazi wa pwani ya Afrika Mashariki. Ugunduzi wa kiakiolojia unaonesha kuwa kulikuwa na wakazi wa asili wa pwani ya Afrika Mashariki wenye utamaduni wao na maendeleo yao hata kabla ya kuja kwa wageni. Ushahidi wa kiethinolojia huchunguza tarihi mbalimbali zinazojaribu kutoa historia ya watu wa pwani na lugha yao.Kwa ujumla, vyanzo hivi vyote huonesha kuwa pwani ya Afrika Mashariki ilikuwa na wakazi wa asili ambao walikuwa na lugha yao, utamaduni wao na pia maendeleo yao. Vyanzo hivi vinahitimisha kwa kusema kuwa lugha ya wakazi hawa ilikuwa ni Kiswahili.Jinsi Miundo ya Kiswahili Inavyofanana na Miundo ya Lugha Nyingine za KibantuMuundo wa SilabiSilabi za Kiswahili na lugha za Kibantu huishia na irabu na siyo konsonanti. Mfano:Kiswahili: BabaKikurya: TataKiha: DataKijita: RataKipare: VavaMuundo wa SentensiMpangilio wa vipashio katika sentensi za Kiswahili na lugha za Kibantu hufanana, ambapo nomino hukaa upande wa kiima na kitenzi upande wa kiarifu. Mfano:Kiswahili: Mama anakulaKijita: Mai kalyaKihehe: Mama ilyaKihaya: Mama nalyaMfumo wa NgeliKiswahili na lugha za Kibantu zina mfumo unaofanana wa upachikaji wa maumbo ya umoja na wingi na maumbo ya upatanisho wa kisarufi. Mfano:Kiswahili: M-tu, Wa-tuKikurya: Mo-nto, Abha-ntoKiha: Umu-ntu, Abha-ntuKikwaya: Mu-nu, Abha-nuKwa ushahidi huu wote, ni dhahiri kuwa Kiswahili kina uhusiano mkubwa na lugha za Kibantu, hivyo kuthibitisha asili yake ya Kibantu.Kukua na Kuenea kwa Kiswahili nchini Tanzania katika Enzi ya Waarabu na WajerumaniEnzi ya WaarabuMahusiano ya Kibiashara na Mataifa MengineKatika karne ya kumi na tisa, Afrika Mashariki iliingia kwenye mahusiano na mataifa mengine kama vile Marekani, Ujerumani, na Uingereza. Hii ilitokana na uhusiano wa muda mrefu wa kibiashara na Waarabu, ambao waliweka athari kubwa katika kukua na kuenea kwa lugha ya Kiswahili. Wageni kutoka Ulaya walipoingia Afrika Mashariki walifanya biashara, shughuli za kidini (mishenari), elimu, na utawala. Kama ilivyokuwa katika kipindi cha Waarabu, uwepo wao pia ulikuwa na athari katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki na kwingineko.Ukuaji wa Kiswahili Kimsamiati nchini Tanzania katika Enzi ya WaarabuBiasharaWaarabu walifanya biashara kati ya pwani na sehemu za bara. Katika biashara yao, walichangia kwa kiasi kikubwa uenezaji wa lugha ya Kiswahili. Lugha kuu ya mawasiliano na ya kibiashara iliyotumiwa na wafanya biashara wa Kiarabu ilikuwa ni Kiswahili. Hii iliwezesha Kiswahili kuenea kutoka pwani hadi maeneo ya bara kama vile Tabora, Kigoma, hadi mashariki mwa Kongo.DiniDini pia ilichangia ueneaji wa lugha ya Kiswahili enzi za Waarabu. Waarabu walipokuja walitaka kueneza dini yao kwa undani kabisa. Kwa hivyo, iliwabidi kuanzisha madarasa ambayo walitumia kufundishia, na lugha iliyokuwa ikitumiwa ni lugha ya Kiswahili. Hii ilisaidia kuenea kwa lugha ya Kiswahili.Maandishi ya KiarabuWaarabu walileta hati zilizotumiwa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili. Kwa kupitia hati za Kiarabu, maandishi mbalimbali ya lugha ya Kiswahili yaliweza kuhifadhiwa. Hivyo, Kiswahili kiliweza kukua kwa vile kingeweza kuhifadhiwa katika maandishi na kusomwa wakati wowote.KuoanaWaarabu waliofika pwani waliweza kuoana na Wabantu. Hii ilisababisha kizazi kipya kutokea. Watoto walichukua maneno mengi kutoka kwa baba na mama yao, hivyo kuongeza msamiati katika lugha ya Kiswahili.Ueneaji wa Kiswahili nchini Tanzania katika Enzi ya WaarabuWaarabu walieneza Kiswahili nchini Tanzania kupitia biashara, kuoana na Wabantu au wenyeji wa pwani, dini, na maandishi ya hati za Kiarabu ambayo yalitumika kuhifadhi maandishi mbalimbali ya lugha ya Kiswahili.Enzi ya WajerumaniUkuaji wa Kiswahili nchini Tanzania katika Enzi za WajerumaniMafunzo ya Lugha ya Kiswahili kwa Wafanyakazi wa SerikaliWajerumani walilazimisha wafanyakazi wote wa serikali kujifunza Kiswahili, kwani sheria ilikuwa ni kwamba pasipojua Kiswahili huwezi kuajiriwa katika serikali ya Mjerumani. Hii ilisababisha watu kujifunza lugha ya Kiswahili ili waweze kuajiriwa. Wajerumani wenyewe walilazimika kujifunza Kiswahili ili waweze kuwasiliana na wenyeji kwa urahisi na hivyo kurahisisha shughuli zao za kiutawala.Ujenzi wa ShuleWajerumani walifungua shule kufundisha watu weusi ili wawe wasaidizi wao katika utawala wa Wajerumani. Lugha iliyotumika kufundisha masomo ilikuwa ni lugha ya Kiswahili.Kuenea kwa Utawala wa Wajerumani Nchi NzimaUtawala wa Wajerumani ulikuwa kwenye kila kona ya nchi. Kwa kuwa wafanyakazi wa serikali walilazimika kufahamu Kiswahili, kila sehemu palipokuwa na ofisi za serikali kulizungumzwa Kiswahili.Shughuli za KiuchumiKatika shughuli za mashamba, Wajerumani walichukua vibarua kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Kwa kuwa kila mmoja alikuwa na lugha yake tofauti, lugha pekee iliyowaunganisha katika mawasiliano kwenye eneo la kazi ilikuwa ni Kiswahili. Hii ilisaidia sana kuenea kwa lugha ya Kiswahili.Ueneaji wa Kiswahili nchini Tanzania katika Enzi za WajerumaniWajerumani walichangia kwa sehemu kubwa kuenea kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania enzi za utawala wao. Mambo yaliyochangia ni pamoja na dini, elimu, shughuli za utawala, na shughuli za kiuchumi kama vile kilimo.Tagged:Form 3kidato cha tatuKiswahili Topic - Previous Mjengo Wa Tungo Next - Topic Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi