Topic Ufahamu Estimated reading: 4 minutes 67 views Summary: Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma.Kiswahili Kidato cha KwanzaJedwali la YaliyomoKusikilizaUfahamu wa KusikilizaMambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa KusikilizaKujibu Maswali kutokana na Habari uliyosikilizaActivity 1Kusoma kwa SautiMambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa KusomaKujibu Maswali kutokana na Habari uliyosomaActivity 2Kusoma KimyaKujibu Maswali kutokana na Habari uliyoisomaKusoma kwa BurudaniMambo ya Kuzingatiwa katika Ufahamu wa Kusoma kwa BurudaniKusikilizaUfahamu wa KusikilizaUfahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa mfano, mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe.Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa KusikilizaUfahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa.Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusika anayezungumza.Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa.Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafuatayo:Kuwa makini: Elekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila anachokisema.Vidokezo vya maana: Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.Kuandika mambo muhimu: Andika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya muhimu ili kumasidia kukumbuka hapo baadaye.Ishara za mwili: Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono, kutingisha kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi huwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyosikilizaJibu maswali kutokana na habari uliyosikiliza.Activity 1Jibu maswali kutokana na habari uliyosikiliza.Kusoma kwa SautiKusoma kwa sauti ni namna ya kuyaangalia maandishi na kuyatamka kwa sauti inayosikika.Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa KusomaKuna vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:Uelewa wa msamiati: Uwezo wa kuelewa msamiati uliotumika katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka, matini yote haitaeleweka.Uelewa wa matini: Ili kuelewa habari/matini, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:Mawazo makuu: Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu, inatakiwa ajiulize, “Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi?” Maswali haya akilini mwake yatamsaidia kuelewa habari hiyo.Alama za uakifishi: Kuzingatia alama za uakifishi; kwa kufanya hivyo, itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatazingatia alama za uakifishi, anaweza kupotosha maana ya mwandishi.Maana ya maneno na misemo: Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa, hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, itamsaidia kuelewa vyema maana ya mwandishi.Kumakinikia: Msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele anachokisoma inampasa akielewe vizuri.Kwa kuzingatia haya yote, msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyosomaJibu maswali kutokana na habari uliyosoma.Activity 2Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma.Kusoma KimyaKatika usomaji huu, msomaji hufumba kinywa na kupitisha macho katika kila mstari haraka haraka. Macho hayo huunganisha neno lililotangulia na lile linalofuata. Ubongo wake huchambua mambo muhimu yanayojitokeza, huku akiyahifadhi kichwani. Mtu akijizoeza kusoma kimya, ananufaika ifuatavyo:Hupata nafasi ya kupima mwendo wake na kiasi cha welewa.Hujiepusha na lawama ya kusumbua wengine.Hukwepa kuzingatia kanuni za matamshi.Huweza kusoma maandishi mengi kuliko ambavyo angesoma kwa sauti.Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyoisomaJibu maswali kutokana na habari uliyosoma.Kusoma kwa BurudaniHuu ni usomaji ambao lengo lake kuu huwa ni kujiburudisha tu. Katika usomaji wa aina hii, msomaji hujisomea zaidi magazeti, majarida, na vitabu tofauti na vile vinavyotumika darasani.Mambo ya Kuzingatiwa katika Ufahamu wa Kusoma kwa BurudaniWakati mwingine sio lazima msomaji awe na vitabu vyote ambavyo anahitaji kuvisoma au magazeti na majarida. Inapotokea hivyo, msomaji anaweza kwenda maktaba kuazima kitabu anachokihitaji.Ingawa lengo la msomaji huwa ni kujiburudisha tu, lakini pia hujiongezea maarifa. Hii ni kwa sababu, magazeti, majarida, na vitabu, sambamba na kutumia lugha sanifu, huelezea mambo mbalimbali yanayoihusu jamii. Hivyo msomaji kutokana na kusoma vitabu na majarida mbalimbali hujiongezea kiwango cha welewa wa lugha na mambo mengine ya kijamii yanayojadiliwa humo.Ni jambo zuri kwa msomaji kujijengea tabia ya kujipima ili aweze kuelewa kiwango cha maarifa aliyopata katika kujisomea. Kujipima huku kunaweza kufanywa kwa kujiundia utaratibu wa kuweka kumbukumbu ya vitu au makala zilizosomwa na kufanya ufupisho wa kila makala.Utaratibu wa Kujipima na Kuweka KumbukumbuTarehe: …Jina la kitabu/makala/gazeti: …Mchapishaji: …Mwaka/tarehe ya uchapishaji: …Ufupisho wa habari: (yasizidi maneno 20)Fundisho/ujumbe mkuu ni: …Jambo lililokuvutia sana: …Maoni kwa ujumla kama yapo: … Topic - Previous Uandishi Wa Barua