Topic Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi Estimated reading: 4 minutes 79 views Uhakiki wa Ushairi, Tamthiliya na RiwayaDhana ya UhakikiUhakiki ni kitendo cha kutathmini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Kwa kiwango cha elimu ya sekondari, mhakiki hufanya kazi ya uhakiki ili kuonesha mambo yanayojitokeza kama vile dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, na msimamo.Dhima ya Mhakiki na Nafasi ya MhakikiDhima ya UhakikiUhakiki una mchango mkubwa sana katika kazi za fasihi na una dhima zifuatazo:Kusaidia Wasomaji: Husaidia wasomaji kuelewa kazi ya fasihi kwa urahisi. Watunzi wa kazi za fasihi hutofautiana katika matumizi ya lugha na taswira, hivyo mhakiki anapofanya kazi ya uhakiki, anamsaidia msomaji kuelewa vipengele hivi kwa kuvifafanua kwa lugha rahisi.Kukuza Fasihi: Mhakiki anapoonesha ubora na udhaifu wa kazi ya mtunzi fulani, watunzi wengine pia watafunguka kifikra na kutunga kazi bora zaidi.Kukuza Uelewa wa Mhakiki: Kwa kuhakiki kazi mbalimbali za fasihi, mhakiki hujiongezea maarifa ya lugha pamoja na mambo yanayotokea katika jamii.Nafasi ya MhakikiMhakiki ana nafasi kubwa katika kazi za fasihi. Mhakiki ndiye anafafanua kazi ya fasihi ili hadhira iweze kumwelewa vizuri mtunzi wa kazi hiyo, hivyo kusaidia kurahisisha mawasiliano kati ya hadhira na mtunzi. Pia, mhakiki huwaonyesha watunzi ubora na udhaifu wa kazi zao, na kwa kufanya hivyo huwawezesha watunzi kufanya kazi bora zaidi.Hatua za Kufanya UhakikiKusoma Kazi ya Fasihi: Mhakiki anatakiwa kuisoma kazi husika ya fasihi kwa kina na kuielewa vizuri.Kuchambua Vipengele Muhimu: Mhakiki anapaswa kuainisha na kuchambua mambo muhimu yanayojitokeza katika kazi hiyo katika vipengele vya fani na maudhui.Kutoa Tathmini: Mhakiki anapaswa kutoa tathmini au kuelezea ubora na udhaifu wa kazi inayohusika.Uhakiki wa MashairiShairiShairi ni utungo wa kisanaa wenye mpangilio maalum wa lugha ya mkato unaowasilisha mawazo au ujumbe kuhusu mwanadamu au mazingira yake na hufuata utaratibu fulani.Aina za MashairiMashairi ya Arudhi: Haya ni mashairi yanayofuata kanuni za kimapokeo au arudhi za utunzi wa mashairi. Kanuni hizi ni pamoja na:Kugawika kwa shairi katika betiBeti kuwa na idadi maalum ya mishororoMishororo ya ubeti kugawika katika vipandeMishororo kuwa na ulinganifu wa mizaniShairi kuwa na urari wa vinaShairi kuweza kuimbika au kuwa na mahadhi au mapigoKuwepo kwa kipokeo katika shairiKuwa na mtiririko wa mantiki na mawazo au muwalaShairi kuwa na utoshelezo wa beti au kujisimamia kimaanaMashairi Huru: Pia hujulikana kama mashairi ya kimapinduzi. Haya ni mashairi yasiyozingatia lazima ya arudhi na hivyo huwa na muundo huru. Sifa zake kuu ni:Lugha ya muhtasariLugha yenye mahadhiLugha ya kisanii iliyo na mafumbo na taswiraMara nyingine hugawika katika betiMishororo kamilifu (inayojitosheleza) na ile isiyo kamilifu (mishata)Sifa za MashairiHutumia lugha ya mkato au muhtasariNi sanaa au kazi iliyobuniwa kwa ufundiHuwa na mpangilio maalum kuanzia mistari hadi betiHutumia lugha teule na msamiati teule uliosheheni tamathali, taswira na jazandaHuwa na sifa ya kuweza kuimbika, hivyo shairi ni wimbo na wimbo ni shairiDhima ya MashairiKupasha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya upole na mvutoKuelimisha na kuzindua jamiiKuendeleza na kukuza kipawa cha utunziKuhifadhi msamiati wa lugha ya Kiswahili na sanaa ya fasihiKuburudisha hadhira na wasomajiKuwasilisha hisia za ndani za mtu na mawazoHatua za Uhakiki wa MashairiSoma shairi polepole na kwa makini kupata maana ya jumlaSoma shairi tena kwa utaratibu ukizingatia maneno na vipande mbalimbali na kuchunguza maana ya kila mojawapoPitia maswali yote kwa makini ukitilia maanani aina ya majibu yanayotarajiwaSoma shairi tena ukipigia mstari kwa penseli sehemu zinazoelekea kujibu maswaliToa majibu kamilifu kulingana na swali kwa lugha ya mtiririkoVipengee vya Uchambuzi wa MashairiAnwani/Kichwa cha Shairi: Huwa ni muhtasari wa shairi katika neno au sentensi moja. Anwani ni kidokezo muhimu cha kinachozungumziwa katika shairi na huweza kuwa ya moja kwa moja, fumbo, kinaya, kibwagizo au sehemu ya kibwagizo. Ikiwa shairi halina anwani, basi lipewe anwani inayoafikiana na maudhui au dhamira kwa sentensi isiyozidi maneno sita.Maudhui: Haya ni masuala makuu au mambo muhimu yanayohusu mwanadamu au mazingira yake yanayozungumziwa katika shairi kama vile malezi, siasa, usalama, unyanyasaji, ufisadi n.k.Dhamira/Shabaha: Ni lengo kuu la mshairi katika kusanifu utungo wake. Dhamira ya mtunzi huwa ni ujumbe kwa kifupi anaoutambua msomaji kutokana na mwelekeo wa usemaji wa mtunzi katika shairi.Mbinu na Tamathali za Lugha: Ni mbinu za uandishi na tamathali za usemi zilizotumiwa na mshairi katika shairi. Mfano: Mazda/ziada/zidi – kurefusha maneno; enda kuwa enenda. Inksari/muhtasari – kufupisha maneno; aliyefika kuwa alofika. Utohozi – mbinu ya kugeuza msamiati/maneno ya lugha geni ili yaandikike na kutamkika kana kwamba ni ya Kiswahili.Taarifa Muhimu za Mwandishi wa Kila KitabuUnaposoma kazi za fasihi ni lazima ujue taarifa muhimu za mwandishi wa kazi hiyo, kama vile jina la mwandishi, falsafa na utamaduni wake, msimamo wake, muundo wa kazi zake, mtindo wake na matumizi ya lugha.Tagged:form 4kidato cha nneKiswahili Topic - Previous Ukuaji Na Ueneaji Wa Kiswahili Enzi Ya Waingereza Na Baada Ya Uhuru Next - Topic Kutunga Kazi Za Fasihi Andishi