Comment

Darasa Huru

Darasa Huru

Limitless Potential

Study smarter, not pricier. Access free resources now.

Topic

Ufahamu

Estimated reading: 3 minutes 68 views

Ufahamu wa Kusikiliza

Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; ni uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa mfano, mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe.

Kujibu Maswali ya Habari Uliyosikiliza

Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:

  1. Kuelewa vizuri sarufi ya lugha inayozungumzwa.
  2. Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusika anayezungumza.
  3. Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa.

Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafuatayo:

  • Kuwa makini: Elekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila anachokisema.
  • Kutilia maanani vidokezo vya maana: Kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.
  • Kuandika mambo muhimu: Andika baadhi ya mambo unayoona kuwa ni ya muhimu ili kusaidia kukumbuka hapo baadaye.
  • Kuwa makini na ishara za mwili: Ishara kama vile kurusha mikono, kutingisha kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.

Kufupisha Habari

Ili kuandika ufupisho mzuri wa habari uliyoisikiliza, yafuatayo hayana budi kuzingatiwa:

  1. Kusikiliza habari kwa makini ili kuielewa vizuri.
  2. Kuandika mawazo makuu yanayojitokeza katika kila aya.
  3. Kuyaunganisha mawazo makuu na kuiandika habari kwa maneno yako.
  4. Kuhesabu idadi ya maneno kama inazidi na kuandika idadi hiyo mwisho wa ufupisho upande wa kulia chini kidogo.

Activity 1: Soma Habari Kisha Toa Ufupisho Wake


Ufahamu wa Kusoma

Ufahamu wa kusoma ni ule mtu anaoupata kwa njia ya kusoma makala, kifungu cha habari, kitabu au gazeti.

Kujibu Maswali kutokana na Habari ndefu uliyosoma

Kuna vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:

  1. Uelewa wa msamiati: Ili kuelewa habari/matini, ni lazima msomaji awe na uwezo wa kuelewa msamiati uliotumika katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka, vilevile matini yote haitaeleweka.
  2. Uelewa wa matini: Msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
  • Kubaini mawazo makuu: Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi?
  • Kuzingatia alama za uakifishi: Hii itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatakuzingatia alama za uakifishi anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
  • Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali: Habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa, hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo.
  • Kumakinika: Msomaji anapaswa kuelewa vizuri kila kipengele anachokisoma.

Kwa kuzingatia haya yote, msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo.

Kufupisha Habari

Kufupisha habari ni kuandika upya habari uliyoisoma kwa maneno machache bila kupotosha ujumbe wa habari ya kwanza. Ufupisho wa habari huwa na sifa hizi:

  1. Mfupi kuliko habari ya mwanzo
  2. Ujumbe uleule wa habari ya mwanzo
  3. Mawazo makuu yaliyojumuishwa kutoka kwenye habari ya mwanzo
  4. Mtiririko wenye mantiki

Hatua za Kufuata katika Kuandika Ufupisho

  1. Kuisoma au kuisikiliza habari kwa makini ili kuielewa vizuri.
  2. Kutambua na kubaini mawazo makuu yanayojitokeza katika kila aya.
  3. Kuyaunganisha mawazo makuu na kuandika au kuelezea ufupisho wa habari hiyo kwa maneno yako mwenyewe bila kupotosha maana ya habari ya kwanza.
  4. Kuhesabu idadi ya maneno ya ufupisho ili kuyapunguza ikiwa yanazidi idadi iliyotakiwa.
  5. Kama muda unaruhusu, pitia tena habari ya mwanzo na ufupisho ili kujiridhisha kuwa hujaacha taarifa yoyote ya muhimu.

Kufupisha Habari Ndefu Uliyosoma

Ili kuweza kuandika ufupisho wa habari ndefu uliyoisoma, hatua zifuatazo sharti zifuatwe:

  1. Kusoma habari kwa makini na kuielewa vizuri.
  2. Kubaini mawazo makuu.
  3. Kuandika ufupisho wa habari kwa maneno yako.
  4. Kuhesabu idadi ya maneno na kupunguza yaliyozidi.
  5. Kupitia tena habari ya mwanzo na ya mwisho kama muda unaruhusu.

Kiswahili Form 4 Past Papers

Year | Questions/Answers

Leave a Comment

Share this Doc

Ufahamu

Or copy link

CONTENTS

Agricultural Development

What is Agriculture? Agriculture refers to a fundamental human activity, which i...

Population and Development

POPULATION STUDIES Is the general activities carried out for the purpose of acqu...

Study of Soil

CONCEPT OF SOIL AND SOIL PROFILE Soil appears very complex and thus differe...

Water Masses

GROUND WATER WATER CYCLE Rain falls on the earth surface in filtrates (soaks int...

Topic

The Dynamic-Earth And Consequence

THEORIES THEORY OF ISOSTASY Denudation has been going on the continents where to...

Position Behaviours And Structure Of The Earth

GLOBE Is the model of the earth Earth Is ball of rock partly covered by wat...

Photograph interpretation

Photograph are the true image pictures showing truly appearance of the earth’s...

Maps and map interpretation

What is a map? Map is a scaled conventional representation of the whole or any o...

Simple survey and mapping

INTRODUCTION TO SURVEYING Surveying is an art or a science of measuring and reco...

Field research techniques

Definitions of Research – Research is the systematic investigation into a...

Application of statistics in geography

STATISTICS Statistics is a branch that deals with every aspect of the data. Stat...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel