Comment

Darasa Huru

Darasa Huru

Limitless Potential

Learn, grow, succeed — with free resources at your fingertips.

Topic

Uandishi

Estimated reading: 8 minutes 77 views

Uandishi wa Insha za Kiada

Insha ni kifungu cha maandishi kinachoandikwa kutokana na mtazamo wa mwandishi katika kujadili mada fulani. Mwandishi anaweza kuandika kuipinga au kuishadidia mada hiyo. Kuna aina mbili za insha: insha za kaida (zisizo za kisanaa) na insha za kisanaa. Insha za kaida hutumia lugha ya kawaida kuelezea mambo mbalimbali katika jamii, kama vile mazingira, uchumi, biashara, na historia.

Muundo wa Insha za Kaida

Muundo wa insha za kaida unajumuisha vipengele vifuatavyo:

  1. Kichwa cha Insha:
  • Hudokeza kile unachokijadili katika insha. Kwa mfano, “Madhara ya Matumizi ya Madawa ya Kulevya”.
  1. Utangulizi:
  • Hutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utajadili katika insha.
  1. Kiini cha Insha:
  • Ndipo kuna maelezo ya kina juu ya mada unayojadili. Maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala.
  1. Hitimisho:
  • Muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au msimamo juu ya mada.

Mambo ya Kuzingatia Katika Uandishi wa Insha

  1. Epuka kutumia vifupisho visivyo rasmi:
  • Uandishi wa insha ni suala rasmi, hivyo epuka kutumia vifupisho visivyo rasmi kama “xamahani” (badala ya “samahani”) au “ckatai” (badala ya “sikatai”).
  1. Andika utangulizi unaovuta umakini wa msomaji:
  • Hii ni muhimu sana ili kumvutia msomaji kuendelea kusoma insha yako.
  1. Andika kiini cha insha kwa mpangilio mzuri:
  • Kila wazo kuu lipewe aya yake na kuwe na mtiririko mzuri wa mawazo.
  1. Andika hitimisho ambalo linahitimisha mawazo yaliyokwishajadiliwa:
  • Epuka kudokeza wazo jipya ambalo litaleta mjadala mpya.

Uandishi wa Hotuba

Hotuba ni insha inayotoa maneno halisi ya mzungumzaji/kiongozi anapozungumza na hadhira kuhusu jambo fulani. Hotuba huandikwa katika hali ya usemi halisi bila alama za kunukuu.

Muundo wa Hotuba

  1. Anwani:
  • Kichwa cha hotuba kinarejelea mada ya hotuba au kutaja hadhira.
  1. Utangulizi:
  • Tambua waliohudhuria mkutano (hadhira) kwa majina/vyeo vyao, kutoka wa cheo cha juu hadi wa chini.
  • Jitambulishe kwa hadhira yako.
  • Tanguliza mada yako.
  1. Kiini:
  • Hakikisha kuna mtiririko wa hoja kuanzia mwanzo hadi mwisho, na ujumbe wako uwe katika usemi halisia.
  1. Tamati:
  • Maliza kwa shukurani au hitimisho la ujumbe wako.

Uandishi wa Risala

Risala ni hotuba fupi inayosomwa mbele ya kiongozi kwa niaba ya kundi fulani la watu ili kutoa maelezo ya haja zao au kuonyesha msimamo wa kundi hilo kwa kiongozi.

Muundo wa Risala

  1. Utangulizi:
  • Cheo cha kiongozi anayehusika.
  • Kundi linalowakilishwa.
  1. Kiini:
  • Maelezo ya hali halisi ya maswala na msimamo wa kundi.
  • Mapendekezo na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa.
  1. Hitimisho:
  • Shukrani.

Mfano wa Risala

Ndugu Mgeni rasmi, Walimu, Wanafunzi wenzetu, Wazazi, Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana.

Kwa niaba ya wanafunzi wa kidato cha nne, tunayo heshima na furaha kubwa kukukaribisha ili ushiriki nasi katika siku hii muhimu na kusikia mafanikio mbalimbali kwa kipindi chote cha masomo yetu hapa shuleni.

Shukrani zetu za pekee ziende kwa uongozi mzima wa Shule na walimu wetu wote kwa jinsi walivyojitoa kwa moyo wa kutufundisha, hivyo tumefundishika vyema. Kweli, tupo tofauti sana na tulivyokuja hapa mwezi Januari 2009.

Ndugu mgeni rasmi, tulianza kidato cha kwanza tukiwa wanafunzi 120; wasichana 60 na wavulana 60. Mpaka leo tunapohitimu tupo wanafunzi 90; kati yao wavulana ni 43, na wasichana 47. Wengine wameshindwa kuhitimu nasi siku ya leo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ujauzito, na kuhama shule. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwa ulinzi wake kwetu hadi leo hii tunahitimu kidato cha nne.

Ndugu mgeni rasmi, elimu hii ya kidato cha nne imetupatia msingi mzuri wa kujiunga na Elimu ya juu, pia imetujengea uwezo mzuri wa kujitambua, kufikiri, kufanya kazi vizuri, na kufanya maamuzi sahihi. Pia imetuwezesha kupata elimu ya mambo mbalimbali kupitia masomo tunayo fundishwa hapa shuleni, kama vile elimu ya uraia, historia, afya, usalama, kilimo, maumbile ya nchi, na viwanda. Vilevile tumeelewa umuhimu wa kusoma vitabu mbalimbali kwa lengo la kuinua uchumi wa taifa letu.

Ndugu mgeni rasmi, mafanikio hayo yamepatikana kutokana na ushirikiano mzuri kati yetu na walimu wetu. Tangu tujiunge na shule hii, tumefanya majaribio na mitihani mara kwa mara jambo lililotusaidia kuinua taaluma yetu. Tunawashukuru sana walimu wetu na tunawaahidi kufanya vizuri katika mitihani yetu ya Taifa ya kidato cha nne mwaka huu. Mungu awabariki sana.

Ndugu mgeni rasmi, tumepata changamoto mbalimbali wakati wa maisha yetu ya kielimu hapa shuleni, kama ifuatavyo:

1. Upungufu wa vitabu vya kiada na ziada, jambo lililosababisha kushindwa kujisomea vizuri.
2. Upungufu wa vifaa vya maabara, hivyo tunatumia muda mwingi sana kujifunza.
3. Upungufu wa walimu, hasa wa masomo ya sayansi.
4. Upungufu wa samani za shule kama madawati, viti, na meza kwa walimu.
5. Ukosefu wa maji ya kutosha, jambo ambalo linaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko.
6. Upungufu wa vifaa vya michezo, kama mipira ya miguu, pete na mikono, na milingoti ya chuma kwa ajili ya magoli ya viwanja vya michezo.

Ndugu mgeni rasmi, tunashukuru uongozi wa shule hii, walimu na wazazi kwa kuchangia maendeleo ya shule yetu. Tuna matumaini kwamba maombi yetu umeyasikiliza na utayaatekeleza kupitia Halmashauri unayosimamia. Asante sana.

Mwisho, tunaomba msamaha wa dhati kwa walimu, wanafunzi wenzetu, na wazazi pale tulipoenda kinyume na matarajio yenu. Tunatumaini mtapokea msamaha wetu, nasi hatuna jambo lolote baya kwenu.

Ndugu mgeni rasmi, tunakushukuru sana kwa kufika katika mahafali yetu. Tunatambua kuwa una majukumu mengi, lakini umeyaacha ili uwe hapa kwa ajili yetu. Asante sana.

Hitimisho

Kwa kuzingatia muundo na vipengele vya msingi vya uandishi wa insha, hotuba, na risala, unaweza kuwasilisha mawazo yako kwa usahihi na kwa namna inayovutia. Kila aina ya maandishi ina muundo wake maalum unaopaswa kufuatwa ili kuwasilisha ujumbe kwa ufanisi.

Uandishi wa Kumbukumbu za Mikutano

Kumbukumbu za mikutano ni rekodi zinazowekwa na katibu wa mkutano wakati mkutano unapoendelea ili kuhifadhi yanayojadiliwa na kukubaliana katika mkutano huo. Katibu anapaswa kufuatilia mtindo maalum wa kuandika kumbukumbu hizo kulingana na mpangilio katika mkutano.

Mambo ya Kuzingatia katika Uchukuaji wa Kumbukumbu za Mikutano

Katika uchukuaji wa kumbukumbu za mikutano, mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:

Kichwa cha Kumbukumbu

Kichwa cha kumbukumbu kinapaswa kutaja mambo yafuatayo:

  • Ni mkutano wa akina nani?
  • Unaandaliwa wapi?
  • Unaandaliwa lini?
  • Unaanza saa ngapi?

Mfano wa Kichwa cha Kumbukumbu:

Kumbukumbu za Mkutano wa Shirika la Msalaba Mwekundu Shuleni ulioandaliwa tarehe saba Agosti 2001 katika Ukumbi wa Mikutano kuanzia saa Tisa alasiri.

Waliohudhuria

Andika orodha ya wote waliofika kwenye mkutano huku ukianzia na yule mwenye cheo cha juu zaidi hadi kwa wanachama. Pia onyesha vyeo vyao.

Waliotoa Udhuru

Hawa ni wale walioomba ruhusa kutohudhuria mkutano.

Waliokosa Kuhudhuria

Hawa ni wale waliokosa kuhudhuria mkutano bila kutoa udhuru.

Waalikwa

Hawa ni wageni walioalikwa katika mkutano, kama vile mlezi wa chama, afisa wa kiutawala, n.k.

Ajenda

Orodhesha hoja zitakazorejelewa katika mkutano huo.

Kuandika Kumbukumbu

KUMB 1: Kumbukumbu ya kwanza huwa ni kufunguliwa kwa mkutano na ujumbe kutoka kwa mwenyekiti.

KUMB 2: Kusomwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia na kuthibitishwa kwa kumbukumbu hizo kwa kutiwa saini.

KUMB 3: Maswala yanayoibuka kutokana na kumbukumbu zilizosomwa. (Kumbuka kutaja nambari ya kumbukumbu hizo.)

KUMB kuendelea: Maswala katika ajenda.

KUMB ya Mwisho: Maswala mengineyo yasiyokuwa kwenye orodha ya ajenda.

Tamati

Kufungwa kwa mkutano. Taja mkutano ulifungwa saa ngapi; mkutano ujao utakuwa tarehe ngapi; kisha acha nafasi ya kuthibitishwa kwa kumbukumbu hizo katika mkutano utakaofuatia.

Mfano wa Kumbukumbu za Mkutano

KUMBUKUMBU ZA MKUTANO WA CHAMA CHA KISWAHILI ULIOANDALIWA KATIKA CHUMBA CHA MIJADALA TAREHE 24 JUNI 2013 KUANZIA SAA TATU ASUBUHI

Waliohudhuria

  • Teddy Mbogela – Mwenyekiti
  • Vaileth Matiko – Mweka hazina
  • Iliashibu Masatu – Mkuu wa utafiti
  • Funk Kiduku – Mwanachama
  • Meta Mkorofi – Katibu

Waliotuma Udhuru

  • Bahatika Mashauri – Naibu Mwenyekiti
  • Ponea Kamgazi – Msimamizi wa Mijadala

Waliokosa Kuhudhuria

  • Zebedayo Chisege – Spika
  • John Kumbikumbi – Mwanachama

Waalikwa

  • Mnoko Nokwe – Mwanahabari
  • Dkt. Fikirini – Mlezi wa Chama

Ajenda

  1. Uchapishaji wa jarida la Kiswahili
  2. Shindano la kuandika insha
  3. Kusajili wanachama wapya

KUMB 3/04/14 – KUFUNGULIWA KWA MKUTANO

Mwenyekiti aliwakaribisha wanachama wote na baada ya kuwatambulisha wageni, akawaomba washiriki wawe huru kuchangia katika ajenda mkutano huu ili kuboresha chama.

KUMB 7/04/14 – KUREJELEA KUMBUKUMBU ZA MKUTANO ULIOPITA

Katibu alisoma kumbukumbu za mkutano wa mwezi Machi. Kumbukumbu zilikubaliwa na wanachama wote na kuthibitishwa na mwenyekiti pamoja na katibu kwa kutia saini.

KUMB 10/04/14 – MASWALA IBUKA KUTOKANA NA KUMBUKUMBU ZILIZOSOMWA

Mweka hazina alifahamisha mkutano kwamba aliongea na mkuu wa idara ya Kiswahili kuhusu ufadhili kama tulivyokuwa tumekubaliana katika KUMB 9/03/10 ya mkutano uliopita.

KUMB 12/04/14 – HAFLA YA KISWAHILI

Iliripotiwa kwamba hafla ya Kiswahili ambayo wanachama walikuwa wamealikwa kuhudhuria katika Shule ya Sakata Academy haingeweza kufanyika kutokana na tamasha la muziki lilizokuwa linaendelea katika shule hiyo. Wanachama waliokuwa wamejitayarisha kwa mashairi waliombwa kuendelea kujifunza ili wayawasilishe muhula wa pili.

KUMB 15/04/14 – UCHAPISHAJI WA JARIDA LA KISWAHILI

Wanachama walikubaliana:

  1. Kwamba chama kitaanza kuchapisha jarida la Kiswahili.
  2. Kwamba jarida litakuwa likichapishwa mara moja kila muhula na kuuzwa shuleni.
  3. Kwamba kila mwanachama atachangia katika kuandika makala na kuuza nakala za jarida hilo.
  4. Kwamba paneli ya wahariri ingeundwa ili kuongoza idara ya uchapishaji.
  5. Kwamba hazina ya chama ina fedha za kutosha kuzindua uchapishaji huo.

KUMB 17/04/14 – SHINDANO LA KUANDIKA INSHA

Kila muhula wa pili, chama huandaa shindano la kuandika insha ambalo wanafunzi wote hushiriki. Insha zilizopendekezwa mwaka huu ni:

  1. “Jadili chanzo cha migomo shuleni na namna ya kusuluhisha.”
  2. … (endelea na insha nyingine kama zilivyopendekezwa)

KUFUNGWA KWA MKUTANO

Mkutano ulifungwa saa kumi na nusu, baada ya maswala yote kujadiliwa. Mkutano unaofuatia ulipangwa kuwa tarehe ishirini mwezi Mei, katika Ukumbi wa Muziki.

KUTHIBITISHWA KWA KUMBU KUMBU

_________ _________
Mwenyekiti Katibu
Tarehe: Tarehe:

Leave a Comment

Share this Doc

Uandishi

Or copy link

CONTENTS

Agricultural Development

What is Agriculture? Agriculture refers to a fundamental human activity, which i...

Population and Development

POPULATION STUDIES Is the general activities carried out for the purpose of acqu...

Study of Soil

CONCEPT OF SOIL AND SOIL PROFILE Soil appears very complex and thus differe...

Water Masses

GROUND WATER WATER CYCLE Rain falls on the earth surface in filtrates (soaks int...

Topic

The Dynamic-Earth And Consequence

THEORIES THEORY OF ISOSTASY Denudation has been going on the continents where to...

Position Behaviours And Structure Of The Earth

GLOBE Is the model of the earth Earth Is ball of rock partly covered by wat...

Photograph interpretation

Photograph are the true image pictures showing truly appearance of the earth’s...

Maps and map interpretation

What is a map? Map is a scaled conventional representation of the whole or any o...

Simple survey and mapping

INTRODUCTION TO SURVEYING Surveying is an art or a science of measuring and reco...

Field research techniques

Definitions of Research – Research is the systematic investigation into a...

Application of statistics in geography

STATISTICS Statistics is a branch that deals with every aspect of the data. Stat...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel