Topic Kuongeza Msamiati Wa Kiswahili Estimated reading: 3 minutes 87 views Uundaji wa ManenoLugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili msamiati uongezeke katika lugha, sharti maneno mapya yaundwe.Njia za Uundaji ManenoNjia za Uundaji Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo:Kubadili mpangilio wa herufiKuambatanisha manenoKutohoa maneno ya lugha nyingineUambishaji wa manenoKufananisha sauti, umbo, mlio na suraKuunda Msamiati kwa Kubadili Mpangilio wa HerufiNeno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno lingine.Mfano 1:Neno “lima” lina herufi l, i, m, a. Herufi hizi huweza kujenga maneno kama mali, kumi, imla, mila.Neno “tua” lina herufi t, u, a. Herufi hizi zinaweza kujenga maneno kama tatu, tua, viatu, tatua.Njia ya Kuambatanisha ManenoKuna njia tatu za kuambatanisha maneno:Njia ya kurudufisha au kukariri nenoMfano: barabara, sawasawa, polepole, katikati, vilevile.Njia ya uundaji wa msamiati kwa kuunganisha maneno mawili tofautiNomino na Nomino:Punda + mlia = PundamiliaBibi + Shamba = BibishambaAfisa + Elimu = AfisaelimuMwana + Siasa = MwanasiasaBata + maji = BatamajiKitenzi na Nomino/Jina:Changa + moto = ChangamotoChemsha + bongo = ChemshabongoPiga + mbizi = PigambiziZima + moto = ZimamotoKuunganisha maneno mawili na kudondosha baadhi ya herufiMfano 2:Baraza la Kiswahili Tanzania = BAKITAMzaliwa wa mahali Fulani = MZAWAChama cha Mapinduzi = CCMNyamamfu = NYAMAFUKutohoa Maneno Kutoka Lugha NyingineKila lugha ina tabia ya kuchukua maneno kutoka lugha nyingine ili kukidhi mahitaji ya msamiati. Maneno yanapotoholewa kutoka lugha nyingine hubadilishwa kimatamshi ili yafuate kanuni za Kiswahili. Maneno haya husanifishwa na asasi za lugha ya Kiswahili kabla ya kutumiwa rasmi.Mfano 3:Neno la Kiswahili – Lugha ya Mwanzo – Neno LililotoholewaShule – Kijerumani – SchuleSalama – Kiarabu – SalaamDuka – Kihindi – DukanKaroti – Kiingereza – CarrotShati – Kiingereza – ShirtPicha – Kiingereza – PicturePapai – Kihispania – PapayaMeza – Kireno – MeziShukrani – Kiarabu – ShukranNgeli – Kihaya – EngeliIkulu – Kinyamwezi – IkuluNg’atuka – Kizanaki – Ng’atukaNdafu – Kichaga – NdafuKuunda Maneno kwa Njia ya Uambishaji wa ManenoHii ni njia ya kubandika viambishi awali na tamati kwenye kiini cha neno. Ujenzi wa maneno hutokana na mzizi mmoja kuonesha maana tofauti ingawa maana hizo zina husiana.Mfano:Mzizi: -lim-Lima, analima, walilima, kilimo, limiana, halitalimwa, ukulima.Kufananisha Sauti, Sura, au TabiaMfano 4:Kengele – hutokana na sauti ya kengele inapopigwa.Pikipiki – hutokana na muungurumo wa pikipiki.Ndizi mkono wa tembo – Ndizi inayo fananishwa na mkono wa mnyama tembo.Chubwi – Jiwe au chura atumbukiapo katika kina cha maji.Mazingira Yanayoelezea Kuhitaji Maneno MapyaMabadiliko mengi yanatokea kila siku katika nyanja mbalimbali za kimaisha, kama vile mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa, kisayansi, na kiteknolojia. Katika mazingira kama haya, watu watahitaji kuwasiliana na hivyo lugha itahitaji kuunda maneno mapya ili kuwasilisha dhana mpya zilizoibuka.Mfano:Maneno kama vile nywila, kisakuzi, udukuzi, puku, talakirishi yameundwa ili kuwasilisha dhana za kiteknolojia kwa Kiswahili.Undaji wa Maneno katika Miktadha MbalimbaliMabadiliko ya kimaendeleo yanafanya lugha ihitaji maneno ya kuyafikisha na kutumiwa na jamii. Ili kukidhi mahitaji hayo, maneno mapya yanazuka. Maneno hayo yanaweza kuwa katika fani mbalimbali kama vile sayansi na teknolojia, siasa, utamaduni, na uchumi kulingana na mkondo wa maendeleo.Mfano wa Msamiati:Fedha, ushuru, kumpyuta, ukoloni, hospitali, suruali, n.k.Activity 1: Unda Maneno katika Miktadha MbalimbaliTafadhali unda maneno mapya kulingana na mazingira yako. Fikiria maendeleo ya kiteknolojia, kisayansi, kiuchumi, na kisiasa na jinsi unavyoweza kuwasilisha dhana mpya kupitia maneno mapya ya Kiswahili.Tagged:form 4kidato cha nneKiswahili Next - Topic Ukuaji Na Ueneaji Wa Kiswahili Enzi Ya Waingereza Na Baada Ya Uhuru