Kiswahili KE Semi Estimated reading: 5 minutes 123 views Semi ni nini?– Tungo fupi zinazowasilisha ujumbe kwa kufumba au kuchora picha.SifaHuwa fupi kwa kuwasilisha ujumbe mrefu kwa maneno machacheNi tanzu tegemezi kwa hutegemea tanzu nyingine kama vile hadithi, mazungumzo, n.k.Hazibadiliki vivi hiviBaadhi ni kielelezo cha maadili k.v. methaliHutumia lugha ya kimafumboHuibua taswiraHuwa na mchezo wa manenoBaadhi huwa na muundo maalum k.v. methali na vitendawiliNyingine ikikosa kutumika hutoweka k.v. misimuUmuhimuKuonya k.m methali, ‘Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.’Kukuza uwezo wa kufikiri k.m. vitendawili na chemsha bongoKutafsidi lugha au kupunguza ukali wa maneno k.m. nahau ‘jifungua’ badala ya ‘zaa’Kuburudisha k.m. vitendawili, chemsha bongo na vitanza ndimiKuhifadhi siri k.m. nahau, misemo, misimuKuelimisha k.m. kutofanya mambo kwa pupa-mla kwa pupa hadiriki kula tamuKuongeza utamu katika lughaKuboresha matamshi k.m. vitanza ndimiKukuza lugha k.m misimuKukuza utangamano katika jamii kwa kuleta watu pamoja wakati zinawasilishwaVipera vya Semia) Methali– Semi fupi ambazo hueleza kwa muhtasari au mafumbo ukweli fulani wa kimaisha.SifaHuwa fupi k.m. ‘Msafiri kafiri.’Hutumia tamathali za usemi.Hutumkia lugha ya kimafumbo.Huwa na maana ya ndani na nje.Kunazo hufanana kimaana k.m. ‘Haraka haraka haina baraka’ na ‘Polepole ndio mwendo.’Hupingana zenyewe k.m ‘Polepole ndio mwendo’ na ‘Chelewa chelewa utamkuta mwana si wako.’Huwa na sifa za kishairi k.v. ukwapi, utao na vina -Haba na haba, hujaza kibaba.Sifa za utegemezi kwa kuingiliana na tanzu nyingine za fasihiHuwa na muundo maalum wa sehemu mbili:i) Wazo k.m ‘Haba na haba…’ii) Kukamilisha wazo ‘…hujaza kibaba.’UmuhimuKukuza uwezo wa kufikiri kwani mpokezi hufikiri ili kupata maana ya ndaniKuonya dhidi ya matendo yasiyofaa k.m. Mchimba kisima huingia mwenyewe na Ukiambiwa jiambie usijeishia kumbe.Kufariji walio katika hali ngumu, k.m Baada ya dhiki faraja, Hakuna marefu yasiyo na ncha, Liandikwalo ndilo liwalo, Ajaliwalo ndilo apataloKuhimiza watu kujitahidi maishani/kuonyesha jambo jema huja kwa kufanyiwa kazi k.m. Mtaka cha mvunguni sharti ainame, Chumia juani ulie kivuliniKupamba lugha iwe na mvuto kwani huwa na usanii mkubwaKuhimiza ushirikiano k.m. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, Jifya moja haliijiki chunguKuelimisha mtu ajue jambo muhimu k.m. Usione kwenda mbele kurudi nyuma si kazi, Pema usijapo pema ukipema si pema tenaKushauri k.m. Enga kabla ya kujenga na Mchama ago hanyeliKufupisha maadili katika nganoKubuni lakabu k.m. kikulachoKufunza maadili k.m. kuwa na subira – Subira huvuta heri.Kuhimiza kutokata tama k.m. Bandu bandu huisha gogo, Papo kwa papo kamba hukata njiweKuonyesha umuhimu wa kuthamini jamaa zako kuliko marafiki k.m. Damu ni nzito kuliko maji, Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa naweKuonyesha umuhimu wa kuthamini vitu vyako – Usiache mbachao kwa msala upitao na Afadhali dooteni kama ambari kutandaKukashifu ubinafsi k.m. Mwamba ngoma huvutia kwake, Kila mchukuzi husifu mzigo wakeKukashifu kiburi k.m. Maskini akipata matako hulia mbwata, Zingwi zingwi lipe nguo utaona mashauoMbinu za Lugha/Fani /Tamathali za Usemi katika Fasihi– Maneno au vifungu vya maneno vinavyotumiwa kutia fasihi urembo ili kufanya ujumbe ueleweke vyema zaidi.Tashbihi – Ulinganishi kwa kutumia viunganishi kama, mithili, mfano na sawa k.m Kawaida ni kama sheriaSitiari/ Istiara – Ulinganishi usio wa moja kwa moja k.m Mgeni ni kuku mweupeTashhisi/Uhaishaji – Kukipa kitu sifa ya uhai k.m Siri ya mtungi muulize kataTaashira/ Ishara – Kitu kuwakilisha kingine k.m Kimya kingi kina mshindo mkubwaChuku/udamisi – Kutia chumvi au kufanya kitu kionekane kikubwa sana au kidogo sana k.m Usipoziba ufa utajenga ukutaTakriri – Urudiaji wa neno au mafungu ya maneno k.m Haba na haba hujaza kibabaTanakuzi – Maneno yaliyo kinyume k.m Mpanda ngazi hushukaTabaini – Msisitizo kwa njia ya kinyume kwa kutumia kikanushio ‘si’Ritifaa – Kusemesha asiyekuwapo kama yupoTaharuki – Kuacha msomaji akiwa na hamu ya kutaka kujua kipi kitakachojiri halafuMbinu rejeshi – Kukumbusha mambo yaliyopita k.mBalagha – Maswali yasiyohitaji majibu k.m Pilipili usiyoila yakuwashiani?Taswira – Ujenzi wa picha akilini k.m Mpanda farasi wawili hupasuka msambaKinaya – Mhusika kutumia maneno au matendo yaliyo kinyume cha inavyotarajiwa k.m Asante ya punda ni matekeKejeli – Kudharau au kubeza k.m Ucha Mungu si kilemba cheupeJazanda – Kufananisha vitu kwa mafumbo k.m. katika biblia k.m Kupanda mchongoma kushuka ndio ngomaKweli kinzani – Hoja mbili zinazopingana/kutowezekana k.m Wagombanao ndio wapatanaoVigezo vya Kuainishia Methali / Kuziweka Pamoja na kuzichambuaMandhari/mazingira k.m. kilimo. k.m Ukipanda pantosha utavuna pankwishaMaudhui k.m. ulezi k.m Samaki mkunje angali mbichiFani/tamathali k.m Haba na haba hujaza kibabaJukumu k.m. kuonye k.m Asiyesikia la mkuu huvunjika guuMaana k.m. sawa k.m Haraka haraka haina barakaii) Vitendawili– Semi ambazo hutolewa kwa mtu kwa mfano wa swali ili azifumbue.SifaHuwa vifupi kimaelezo.Hutumia lugha ya kimafumbo.Hutolewa mbele ya hadhira.Hutumia ufananisho wa kijazanda.Kunazo huhusiana na methali k.m. mzee amekufa vyombo vimevunjikavunjika.Huwa na wakati maalum wa kutolewa yaani jioni.Huwa na mchezo wa maneno k.m. Ukiona njigi utadhani njegeHujisimamia vyenyeweKunavyo huwa na jibu zaidi ya mojaHutumia tamathali za lugha kwa ufanifu mkubwaHuweza kuwa na fomyula/muundo maalumk.m. Mteguaji: KitendawiliMteguaji: TegaUmuhimuKuburudisha jioni baada ya kaziKukuza ubunifu wa kuvitunga kwa kulinganisha vitu katika mazingira ili kuviundaKuimarisha uwezo wa kukumbukaKukuza uwezo wa kufikiri kwani mfumbiwa huhitaji kufikiri sana ili kupata jibuKuleta umoja na ushirikiano katika jamii kwa kuleta watu pamoja wakati vinategwaKuimarisha ujuzi wa kujieleza kwa lughaKupanua ujuzi wa mazingira wa mtotoKuendeleza utamaduni wa jamii k.m. Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini. siwezi kulichumaKukejeli au kudharau tabia mbaya k.m. Wazungu wawili wanachungulia dirishaniTagged:Kiswahili KENotesSemi Kiswahili KE - Previous Hadithi