Kiswahili KE Hadithi Estimated reading: 11 minutes 123 views Hadithi ni nini?– Hadithi ni masimulizi yanayotumia lugha ya mtiririko au nathariSifaHutumia ya lugha ya mtiririko au nathari- kueleza matukio moja kwa mojaHurithishwa jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingineHuwasilishwa mbele ya hadhiraHutambwa mahali maalum k.v. ndani ya nyumba, chini ya mti, uwanjani, n.k.Huweza kutokana na matukio halisi (kihistoria) au ya kubuniHuwa na mafunzo fulani kwa jamii/hadhiraHutumia wahusika wa aina tofauti k.v. nyumbani, wanyama, ndege, mazimwi, n.k.Hutumia aina nyingine za sanaa k.v nyimbo, methali, ushairi, n.k.Huwa na utendaji k.v. mtambaji kuiga fisi anavyokulaAghalabu hutambwa jioniMajukumu ya HadithiKufunza maadili yaliyo nguzo kuu kwa wanajamiiKukuza ujasiri wa kuzungumza hadharaniKuburudisha baada ya kazi ya kutwaKukuza uwezo wa watoto wa kukumbuka ili kutamba baadayeKueleza asili ya mambo k.m visaviini, visasili na ngano za usuliKutahadharisha wanajamii dhidi ya kufanya mambo yasitofaaKuunganisha watu katika jamii wanapojumuika pamoja kusikiliza utambajiNgano za mtanziko hukuza uwezo wa kutathmini na kutoa uamuzi ufaaoKukuza lugha hasa kwa hadhira ya watotoKuhifadhi na kuendeleza historia ya jamii k.v. mighani, tarihi, n.k.Kuelimisha hadhira kuhusu utamaduni waoNjia ya kupokeza kizazi historia na utamaduni wa jamiiSifa za Mtambaji / Mganaji BoraAsiwe mwoga ili kuweza kuzungumza hadharani.Asiwe na haya ili kuweza kuzungumzia mambo ya aibu inapobidiAwe na uelewa wa mazingira na masuala ibuka katika jamii ili kuweza kuwasilisha dhana zisizopatikana katika mazingira yake k.m. kutumia rais kuelezea dhana ya mfalmeAwe na ufahamu mpana wa lugha ili aweze kuitumia kwa uhodari na kuwasilisha kwa wepesiAwe mchanganfu na mcheshi ili kunasa makini ya hadhira na kuzuia isikinaiAwe na ufahamu mpana wa utamaduni husika ili kuzuia kutumia maneno na ishara zinazoweza kuwaudhi au kupingana na imani za hadhiraAwe na uwezo wa kushirikisha hadhira k.v. kuimba, maswali ya balagha ili isikinai, n.k.Aweze kujua, matarajio, kiwango cha elimu na tajriba ya hadhira ili kuweza kubadilisha kwa kiwango kinachofaaAwe na uwezo wa kuingiliana vizuri na hadhira ili aivutieAwe na kumbukumbu nzuri ili usimulizi wake utiririke vizuriAwe na uwezo wa kudramatisha ili kuonyesha picha fulani k.v. kuiga toni, sauti, na kiimbo kulingana na swala analowasilishaKubadilisha toni au kiimbo ili hadhira isikinaiAwe na ujuzi wa kutumia ishara za uso, mwili na miondoko kulingana na hali anayoigizaAwe na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka na inayovutiaAweze kubadilisha toni na kiimbo kulingana na hali tofauti anazoigiza k.v. huzuniAwe na uwezo wa kushirikisha hadhira kwa nyimbo na maswali ya balagha ili kuondoa uchovu wa kutazama na kusikilizaAwe na uwezo wa ufaraguzi/ kubadilisha utambaji wake papo hapo kutegemea hadhira yake na kutoa mifano inayofahamika kutoka katika mazingira ya hadhiraAwe na uwezo wa kutumia mtuo wa kidrama ili kuongeza taharuki, kusisitiza ujumbe na kuteka makini ya hadhiraAina za Hadithi– Kuna aina mbili za hadithiHadithi za Kubuni / Ngano – Hazisimulii matukio ya kweli bali ya kutungwaHadithi za Kisalua/Kihistoria – Zinazosimulia matukio yaliyowahi kutendwa na wahusika waliowahi kuishi. Huongezewa ubunifu ili kuvutia zaidi.Hadithi za Kubuni / Ngano– Hadithi zinazosimulia kisa chenye funzo na zenye wahusika aina ya binadamu, viumbe na vitu visivyo na uhai.Sifa za NganoZina fomyula ya kuanzia/mwanzo maalumZina fomyula ya kumalizia/mwisho maalumZina wahusika aina mbalimbaliZina matumizi ya nyimboHutumia takriri (usambamba) ili kusisitiza k.m. zimwi likakimbia, likakimbiaHuwa na na maadili/mafunzoHutumia maswali ya balagha kuongeza taharukiHutumia tanakali za sautiZina matumizi ya fantasia au matukio yanayokiuka uhalisi/mambo ya ajabu k.v. binadamuAina za Fomyula za Kuanzia/Mianzo MaalumPaukwa, Pakawa. Sahani. Ya mchele. Giza. La mwizi. Na kiboko je? Cha mtoto mkorofi…Hapo zamani za kale/za kongamawe…Ilitokea…Hadithi! Hadithi! Hadithi njoo…Kaondokea chenjangaa, kajenga nyumba kakaa, mwanangu mwanasiti, kijino kama chikichi, cha kujengea kikuta, na vilango vya kupita…Hapo jadi na jadudi…Umuhimu wa Fomyula ya Kuanzia/Mwanzo maalumi) Kuvuta makini ya hadhiraii) Kumtambulisha mtambaji kwa hadhiraiii) Kuashiria mwanzo wa hadithiiv) Kutoa hadhira kutoka ulimwengu halisi hadi ule wa hadithiAina za Fomyula za Kumalizia/Miishio MaalumHadithi inaishia hapo.Tangu siku hiyo…Wakaishi raha mustarehe.MaadiliUmuhimu wa Fomyula ya Kumalizia/Mwisho Maalumi) Kuashiria mwisho wa hadithi.ii) Kutoa hadhira katika ulimwengu wa hadithi hadi ule halisi.iii) Kumpisha/kumpa fursa mtambaji anayefuata.iv) Kupisha shughuli inayofuata.v) Kutoa funzo la hadithi kwa muhtasari.vi) Kupa hadhira nafasi ya kupumzika baada ya kuwa makini kwa mudaUmuhimu wa Nyimbo katika Nganoi) Kushirikisha hadhira.ii) Kusisimua hadhira na kuondoa ukinaifuiii) Kuteka makini yao.iv) Kuwasilisha mafunzo/maadili.v) Kutenganisha matukio katika hadithi.vi) Kuburudisha hadhira.vii) Kupunguzia hadhira mwemeo.Umuhimu wa Tanakali za Sauti/Onomatopeya katika Nganoi) Kuongeza utamu.ii) Kusaidia msomaji kupata picha kamili.iii) Kusaidia kupata hisia halisiAina za Ngano (Hadithi za Kubuni)i) Hurafa– Hadithi zenye wahusika wanyama na ndege.– Hurafa za kijanja ni hadithi ambapo wanyama wadogo hutumia ujanja wa hali ya juu ili kujinasua na hali ngumu au mitego wanayotegewaSifaWahusika ni wanyama au na au ndegeWanyama na ndege hupewa sifa za binadamuNi kazi ya ubunifuHutoa mafunzo kwa njia ya kuchekesha na isiyoumizaHuwa na ucheshi mwingiHutumia mbinu ya uhuishiHuwa na sifa zinazohimizwa na zinazoshutumiwaUjanja au uongo hujitokeza katika hurafa za kijanjaUshindi hujitokeza katika hurafa za kijanjaUmuhimuKutahadharisha watu dhidi ya kuwa wa danganyifu/kudanganyika kwa urahisiKuonyesha jinsi tabia ya udanganyifu inavyoweza kujitokeza na kuathiri watuHurafa za kijanja hufunza jinsi ya kupampana na hali ngumuii) Hekaya/Ngano za Kiayari– Hadithi zinazomsawiri mhusika anayetumia ulaghai kupata matilaba yake kutoka kwa wengine (kwa mfano: Abunuwasi).SifaWahusika wakuu ni binadamuHuwa na ubunifu mkubwaHustaajabisha na kuchekeshaUjanja na uongo hujitokezaUshindi hujitokezaNi za kubuniUmuhimuHutahadharisha watu dhidi ya kuhadaika kwa wepesiHuonya dhidi ya matokeo yanayoweza kuwapata wanaojinyakulia mali kwa udanganyifuKuonya dhidi ya usalitiKukashifu viongozi dhalimu na matendo maovuKukejeli wanaotumia nguvu badala ya akili/hekimaiii) Visasili– Hadithi zinazoeleza asili ya matukio fulani katika jamii k.m. kifo, jua, lugha, zilizala n.k.SifaHusimulia mambo ya kiimani na kidiniHuwa na misingi ya kihistoriaHueleza asili ya matukio katika jamiiWahusika ni wanyama na binadamuHuwa na maadiliHurithishwa kizazi hadi kingineUmuhimuKueleza asili ya mambo kama vile kifo, utamaduni n.k.Kueleza utaratibu wa kutekeleza desturi k.v. mahariKuhalalisha baadhi ya mila na desturi za jamii k.v. ulipaji mahari, uabudu miti, n.k.Kukitisha mizizi imani fulani ya watuKupunguza athari za majanga kama vile kuhalalisha kifoKutambulisha jamii kwani kila jamii ina aina yake ya visasiliKuhifadhi historia na utamaduni wa jamiiiv) Ngano za usuli– Hadithi zinazoeleza asili ya hali, tabia, mahusiano au wasifu. k.v. asili ya kuku kuchakura, asili ya kinyonga kwenda kwa tahadhari, n.k.SifaWahusika ni wanyama na binadamuNi kazi ya kubuniHueleza kuhusu asili ya sifa, tabia au hali.Hutumia mbinu ya uhuishiHuwa na maadiliUmuhimuKueleza sababu ya tabia, hali au sifa FulaniKuonya dhidi ya tabia hasi kama vile ulafiv) Ngano za mazimwi– Hadithi ambazo wahusika ni mazimwi.SifaWahusika ni mazimwiMazimwi huwakilisha sifa hasi za binadamu k.m ulafi, ukatili, uovu n.k.Hujaa uharibifuHuwa na matumizi mengi ya fantasiaKipengele cha safari hujitokeza k.v. kwenda nchi za mbali kutafuta suluhisho.Ushindi hujitokeza (mazimwi hushindwa)Ni kazi ya kubuniHuwa na maadiliMazimwi huwa na sifa zinazokiuka mipaka ya binadamu k.m. kinywa kisogoni, jicho moja kubwa, n.k.UmuhimuKukashifu tabia ya uovu, ulafi, na ukatiliKutahadharisha dhidi ya kuwa na ulafi, ukatili n.k.Kutia moyo waliodhulumiwa kuwa waliowanyanyasa wataadhibiwa siku mojavi) Ngano za Mashujaa– Ambazo zinazohusu watu waliotenda matendo ya kishujaa katika jamii zao kama vile kuokoa jamii.– Ngano za mashujaa ni za kubuni ilhali katika mighani, mashujaa wanaaminiwa waliishi.SifaKipengele cha motifu au kusafiri nchi za mbali, kupigana na mazimwi kuokoa jamiiHusawiri mapigano kati ya wema (lila) na ubaya (fira)Uovu huwakilishwa na mazimwi au viongozi dhalimuHatimaye wema hushinda uovu kwa juhudi za mashujaaUmuhimuKuhimiza uzalendo na ujasiri miongoni mwa vijanaKuhimiza ujasiri miongoni mwa vijanaKusifu mashujaa katika jamiiKuelimisha jamii kwa kuwapa maarifa ya kukabiliana na changamoto, inda na ilaKuhimiza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga mashujaa na kupigania jamiiKuonya dhidi ya matendo hasi k.v. ukatiliKuhimiza watu kutokata tamaavii) Ngano za mtanziko– Hadithi ambapo mhusika hukabiliwa hali ngumu ya kuamua baina ya mambo wawili au zaidi yanayomkabili.SifaWahusika ni wanyama au binadamuNi kazi ya kubuniMhusika hulazimika kufanya uteuzi mgumuHali mbili au zaidi zinazotatanisha huwepoUmuhimuHutuerevusha jinsi ya kupambana na hali ngumuKuonya/kutahadharisha dhidi ya kujiponzaKukuza uwezo wa kupima mambo na kuteua lililo muhimuKuonya dhidi ya kutenda bila kuwaza kwa kinaviii) Ngano za Kimafumbo– Ambazo huwa na maana ya ndani/iliyofichika.Istiara – Hadithi ambayo maana yake huwakilisha maana nyingine iliyofichika k.v. hurafa ambapo wanyama huwakilisha binadamuMbazi – Hadithi fupi inayotolewa inayotolewa kama mfano kumkanya au kumwelekeza mtu k.v. katika bibliaHadithi za Kisalua/Kihistoriai) Mighani– Hadithi za mashujaa/majagina wa jamii fulani k.m. Rwanda Magere wa Waluo, Fumo Liyongo wa Wapate, Koome Njue wa Wameru, Wangu wa Makeri wa Wakikuyu na Syokimau wa Wakamba.SifaHuhusu mashujaa wa jamii fulaniWahusika hupambana na hali ngumu inayosababishwa na maaduiWahusika hupewa sifa na uwezo usiokuwa wa kawaida k.v. ukubwa wa ajabu, nguvu katika kivuli, nguvu katika nywele, kutoulika n.k.Wahusika hupigania haki za wanyongeMhusika hukomboa jamii yake dhidi ya maaduiMhusika hufa kifo cha huzuni (tanzia) kwa kusalitiwa na mtu wa karibu k.v. mwanamke au jamaa zaoMashujaa huuliwa kwa njia ya ajabu kama vile kunyolewa nywele, kivuli kuchomwa mkuki, kuchomwa shindano ya shaba kitovuniMighani huzungumzia matukio ya kihistoriaKuna tabia ya kupiga chuku matukio yaliyo hadithiniMighani hurithishwa jamii kutoka kizazi kimoja hadi kingineHuchukuliwa na jamii kama hadithi zenye ukweli na jamii hujinasibisha na mighani hiyoHusimulia mambo ya kiimani na kidiniUmuhimuKutambulisha jamii kwani kila jamii ina aina yake ya mighaniKuhifadhi na kumbusha historia yajamiiKusifu mashujaa katika jamiiKuhimiza ujasiri miongoni mwa vijanaKuelimisha jamii kwa kuwapa maarifa ya kukabiliana na adui au changamotoKukuza uzalendo kwa kuhimiza watu kuiga mashujaa na kupigania jamiiKuonya dhidi ya matendo hasi kama vile usalitiKuhimiza watu kutokata tamaii) Visakale– Masimulizi ya matukio yaliyotendeka zamani k.v. vita, majanga kama njaa na magonjwa na hamahama za jamii k.v. waisraeli kutoka misriiii) Visaviini– Hadithi zinazoeleza chimbuko la jamii Fulaniiv) Mapisi– Maelezo ya kihistoria yasiyo na ubunifu wowote k.v. chimbuko la kundi la wabantu kutoka Afrika ya Kati na kuenea sehemu mbalimbali za Afrikav) Tarihi– Maelezo kuhusu matukio ya kihistoria kulingana na yalivyofuatana ki wakativi) Kumbukumbu– Maelezo ya kitawasifu kuhusu mtu au jamii inayotambulika kwa kutoa mchango fulani mkubwaVipera Vingine vya Hadithii) Soga– Hadithi fupi za kuchekesha zinazolenga kutania au kudhihakiSifaWahusika ni wa kubuniHutaja ukweli unaoumizaHutumia vichekesho kupunguza ukali wa dhihakaHutumia chuku kupita kiasiHuhusu tukio mojaNi fupiUmuhimuKukashifu matendo hasi kwa njia ya ucheshiKuonya na kutahadharisha dhidi ya matendo hasi k.v. ulaghaiKufunza maadiliKuburudisha kwa kuchekeshaii) Vigano– Hadithi fupi zinazosimulia kuhusu matendo mabaya katika jamii na wakati uo huo kuonya na kuelekeza dhidi yayo.– Aghalabu huandamana na methali kwa lengo la kufafanua linalokusudiwa au kudhibitisha funzo la methali fulani.SifaHuwa vifupiHusimulia kisa kimoja tuWahusika ni binadamu na wanyamaHufunza maadili kutokana na methaliiii) Kisa– Masimulizi mafupi yenye tukio moja lenye funzo kwa njia ya kufurahishaMambo ya Kuzingatia katika Uchambuzi wa Hadithi/Ngano– Tanzu ni aina za tungo zenye muundo uliokaribia kufanana.Kueleza aina ya ngano kwa kuzingatia wahusika na maudhuia) Ngano yaweza kuwa ya mazimwi na ya mashujaa kwa wakati mmojab) Ngano yaweza kuwa hurafa, ya usuli na ya kiayariKutaja wahusikaKufafanua sifa za wahusika wakuuMaadili/mafunzo yanayojitokeza katika hadithiKubainisha sifa za ngano/hurafa/hekaya, n.k. zinazojitokeza katika hadithiKueleza umuhimu wa fomyula ya kuanzia/wimbo uliotumiwa katika hadithiKubainisha tamathali za usemi zilizotumiwa katika hadithi fulaniKuonyesha jinsi ngano inavyoshughulikia maudhui fulaniKufafanua ufaafu wa methali fulani zilizotumiwa katika hadithiKatika ngano ya mtanziko, ungekuwa mhusika mkuu ungefanya nini?Kubainisha matumizi ya mbinu ya fantasiaKufafanua maswala ibuka/maudhui yaliyoshughulikiwa k.m. usaliti, ujinga, ulaghai, n.k.Kuchanganua utungo kifani-ploti, wahusika, mbinu za lugha, fantasia, nyimbo, n.k.Kueleza majukumu ya hadithiTagged:HadithiKiswahili KENotes Kiswahili KE - Previous Fasihi Simulizi Next - Kiswahili KE Semi