Kiswahili KE Fasihi Simulizi Estimated reading: 12 minutes 107 views Fasihi Simulizi ni nini?Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kuwasilisha ujumbe unaomhusu binadamu.Sanaa ni ufundi wa kuwasilisha fikra na hisia za binadamu kama vile maneno, maandishi, uchoraji, uchongaji, ufinyanzi n.k.Fasihi simulizi ni sanaa kwa vile:Huwasilisha ujumbe kuhusu binadamu kuhusu utamaduni na uchumiHuwa na umbo mahsusi k.m. hadithi huwa na mwanzo, kati na mwisho na mashairi huwa na beti, mishororo, n.k.Hutumia lugha kwa ufundi k.v. ya kitamathaliHusawiri mandhari/mazingira mahsusi kwa ufundi mkubwaHujenga wahusika kwa ustadi mkuu ili kusawiri tabia za watu katika jamiiTofauti Kati ya Fasihi na Sanaa NyingineFasihiSanaa NyingineKutumia lughaKutotumia lughaSanaa tendiSi tendiKutumia wahusika kuwasilisha maudhuiHutumia maumbo kumithilisha watuKutumia maudhui na fani kuwasilisha ujumbeKutumia maumbo na sura za vituKujikita katika mazingira na wakati maalumHazijikiti katika muktadha na wakati maalumMakundi Ya FasihiFasihi simulizi – Fasihi inayowasiolishwa kwa njia ya mdomo.Fasihi andishi – Fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi.Tofauti Kati Ya Fasihi Simulizi Na Fasihi AndishiFasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo ilhali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishiFasihi simulizi huhifadhiwa akilini ilhali fasihi aandishi huhifadhiwa kwa maandishiFasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/mwandishiFasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyama na ndege, mazimwi na majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwaFasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishiUwasilishaji wa fasihi simulizi huweza kuandamana na utendaji k.v matumizi ya ishara, nyimbo, makofi, kuimba, kubeba zana katika majigambo n.k ilhali ule wa fasihi andishi hauandamani na utendaji isipokuwa inapowasilishwa mbele ya hadhiraFasihi simulizi huwasilishwa mbele ya hadhira ilhali fasihi andishi si lazima iwasilishwe mbele ya hadhiraFasihi simulizi huwasilishwa mahali maalum k.v jandoni, matangani, arusini, n.k ilhali fasihi andishi haina mahali maalumFasihi simulizi huandamana na shughuli fulani ya kitamaduni ilhali fasihi andishi haiandamani na shughuli ya kitamaduniFasihi andishi huhitaji muda kutunga ilhali baadhi ya fasihi simulizi huzuka papo hapo k.m. semi, maigamboFasihi simulizi ina uwezo mkubwa wa kubadilishwa na fanani anapowasilisha ufaraguzi) bali fasihi andishi haibadiliki isipokuwa mwandishi aiandike upyaFasihi simulizi ina historia ndefu kuliko fasihi andishi kwa kuwepo tangu mwanzo wa maisha ya binadamuFasihi simulizi huwasilishwa wakati maalum k.v. usiku, kipindi fulani cha mwaka ilhali andishi haina wakati maalumJinsi Fasihi Simulizi na Andishi ZinavyofananaZote mbili hushughulikia masuala yanayohusu maisha maisha ya binadamuZote mbili Huhumia lugha kwa ubunifu kuwasilisha maudhuiZote mbili huwa na vipengele viwili vikuu, maudhui na fani (jumla ya mbinu msanii alizotumia kuwasilisha maudhui)Zote mbili majukumu sawa k.v. kuburudisha, kuadilisha, kuhifadhi na kuendeleza utamaduni, n.kZote mbili zina utendaji-pale tamthilia na riwaya zinapoigizwaZote mbili huzaliwa, hukua na hufa kutegemea mabadiliko ya wakatiZote mbili huwa na wawasilishaji-fanani k.m. mtambaji/mganaji au manju/yeli katika fasihi simulizi na mwandishi upande wa fasihi andishiFasihi simulizi imekopa tanzu za fasihi simulizi k.v. methali, mashairi, n.kMajukumu ya Fasihi SimuliziKuburudisha-kustarehesha, kufurahisha, kuchangamsha, kutuliza, kusisimua na kupumbaza akili na kiwiliwili – nyimbo, hadithi, vitendawiliKufunza maadili kwa wanajamii kwa kuwahimiza kuiga sifa chanya na kukataa sifa hasi za wahusikaKukuza uwezo wa kufikiri/kudadisi k.m vitendawili na chemshabongoKufariji k.m mbolezi na methali k.m. ‘Baada ya dhiki faraja’Vipengele vya fasihi simulizi k.v mashairi, nyimbo, nahau, hutumiwa katika uandishi wa fasihi andishiKuhifadhi historia ya jamii k.m. mighani, visaviini, mapisi, tarihi n.k.Kukejeli tabia zinazokiuka matarajio ya jamii k.v soga, methali, n.k.Kuendeleza tamaduni za jamii kwani husawiri imani na desturi za jamii. k.v kitendawili ‘Nyumbani mwetu mna papai lililoiva lakini siwezi kulichuma.’ – Mtu hawezi kumwoa dadakeKuunganisha watu pamoja kwa kuwajumuisha pamoja wakati wa ngoma, kuimba, utambaji, n.k.Kukuza lugha k.v. misimu inapokita kimatumizi na kujumuishwa katika lugha sanifuKukuza uwezo wa kutumia lugha kadiri mtu anapoendelea kuwasilisha k.v. hotuba, vitanza ndimi husaidia kuboresha matamshi na kutofautisha maana za manenoKuza uwezo wa kubuni k.v. malumano ya utani, vitanza, ndimi ngonjera, n.k.Kukuza uzalendo kwa kufanya wanajamii kuonea fahari jamii zao na kuiga mashujaa au watu waliotendea jamii makuuKuonya na kutahadharisha wanajamii dhidi ya tabia hasi k.v. ulafi, uchoyo, n.k.Sababu za Ufaraguzi / Kubadilika kwa Fasihi SimuliziKuwasilishwa vibayaFanani kusahau na kubadilisha yaliyomo na mtiririkoKubadilisha ili kukidhi mahitaji ya hadhira k.m. umri na uelewa wao- kutumia lugha nyepesi kwa watoto na pevu kwa watu wazimaMabadiliko ya mandhari/mazingira-vitu vilivyo katika mazingira halisi kukosekana katika mazingira ya usimulizi na msimulizi kutumia vitu katika mazingira yake vinavyokaribiana navyoKutoeleweka na hivyo kuhifadhiwa vibayaMabadiliko ya wakati k.m kitendawili cha wakati wa mkoloni kutumia mzungu na cha wakati wa mwarabu kutumia mwarabu na maana ni ile ile-Mzungu/mwarabu amesimama kwa mguu mmoja-mwavuliMabadiliko ya falsafa ya vizazi na maingiliano katika jamii kusababisha kurithisha tu yale ambayo ni muhimu na kuacha mengineKila fanani huwa na mtindo wake wa kuwasilisha/kisaniiUbunifu wa fanani ili uwasilishaji uweze kuvutia saidi na uwezo wake wa lughaTeknolojia kusababisha kuhifadhiwa na hivyo kuiuaWahusika katika Fasihi SimuliziWahusika ni viumbe wa sanaa ambao hutumiwa katika kazi ya fasihi kuwasilisha maswala mbalimbali.Fanani – anayetunga na kuwasilisha fasihi simuliziHadhira – kusikiliza, kutazama, kushiriki wa kuimba, kuuliza maswali, kutegua vitendawili, kupiga makofi, n.k. kuna aina mbili za hadhira:Hadhira tendi/haiHadhira tuliWanyama – wanaofanya kama binadamu na kuwakilisha sifa kama vile ujanja, ulaghai, tamaa na ujinga na wanaobakia wanyama tuBinadamuMazimwi na majitu – viumbe vyenye matendo na maumbile ya kutisha kama vile jicho moja, vichwa viwili au zaidi, nusu mtu na nusu myama, wenye tamaa iliyokithiri ya kuweza kumeza kila kitu, kuhifadhi na kutunza binadamu ananyoyapendezaWahusika vitu (visivyo na uhai) k.m. mawe, miti, vijaluba, vibuyu-hutumiwa kuibua imani za kidiniMizimu – roho za waliokufa – hutembea, hula na huathiri binadamuMiungu – viumbe vyenye uwezo mkubwa dhidi ya binadamu k.m. katika mighani na visasiliNjia za Kukusanya Fasihi Simulizia)Kuchunza / Utazamaji– Kutazama kwa makini yanayotokea na kuandika.UmuhimuKupata habari za kutegemewa na kuaminikaNi rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.Ni njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandikaKuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.Kuweza kupata hisia halisi za uwasilishajiUdhaifuShida ya mawasilianoUgeni wa mtafiti kusababisha washiriki kumshuku na kusitisha uwasilishajiGhali kwa kumbidi mtafiti kusafirihuhitaji muda mrefub) Kusikiliza Wasanii Wakiwasilisha Tungo ZaoUmuhimuKuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.Kupata habari za kutegemewa na kuaminikaNi rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.Kikwazo cha mawasiliano-Si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandikaKuweza kupata hisia halisi za uwasilishajiUdhaifuShida ya mawasiliano-Si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandikaHuhitaji muda mrefu-kusafiri na kusikilizaUgeni wa mtafiti kusababisha washiriki kutowasilisha ipasavyoGhali kwa gharama ya usafiric) Mahojiano– Kuhoji wanaofahamu mengi kuhusu fasihi simulizi.UmuhimuKuweza kung’amua wakati mhojiwa anatoa habari zisizo za kweliKuweza kufafanulia mhojiwa maswali ili kuweza kupata habari sahihi zaidiKuweza kupata sifa za uwasilishaji k.v. toni/kiimbo, ishara n.k.Ni rahisi kurekodi k.v. kwa vinasa sauti, video, n.k.Kupata habari za kutegewa na kuaminikaUdhaifuHuhitaji muda mrefuMhojiwa kutotoa habari kwa kutomwamini mtafiti kwa ugeni wakeKikwazo cha mawasiliano-si njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandikaGhali kwa gharama ya usafiri.d) Kurekodi Katika Kanda za Sauti / TepurekodaUmuhimuKuweza kudumu na kufikia vizazi vingiSifa za uwasilishaji/uhai kama vile toni na kiimbo kuhifadhiwaMkusunyanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewaKupata habari za kutegewa na kuaminikaKuweza kupata hisia halisi za uwasilishajiUdhaifuChaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirikaHakiwezi kunasa uigizajiFanani huenda asiwasilishe vyema akijua anarekodiwaGhali kwa kuhitaji kununua kifaa na kumbidi mtafiti kusafirie) Kurekodi kwa Filamu na Video– Hunasa picha zenye miondoko na sauti.UmuhimuVideo huhifadhi uigizaji, ishara na kiimbo/toniKuonyesha uhalisi wa mandhariMkusunyanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewaKazi iliyokusanywa hivi hudumu kwa muda mrefuNjia bora kwa wasiojua kusoma na kuandikaKupata habari za kutegewa na kuaminikaUdhaifuChombo chaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirikaFanani huenda asiwasilishe vyema akijua anarekodiwaNjia ghaliFanani huenda asiwasilishe vyema akijua anarekodiwaGhali kwa gharama ya ya usafiri na kununua filamu na kamera ya videoData yaweza kufisidiwa na hivyo kutowafikia walengwaf) Kupiga Picha kwa Kamera– Hunasa picha zisizo na miondoko na sauti.UmuhimuHuonyesha uhalisi wa mandhariHuweza kuhifadhi isharaMkusunyanyaji aweza kurudia uwasilishaji ikiwa hakuelewaKupata habari za kuaminiwa na kutegemekaUdhaifuGhali kwa gharama ya ya usafiri na kununua kameraSifa za uhai kama vile kiimbo haziwezi kuhifadhiwaYaweza kukosa nguvu za umeme na utafiti kuathirikaData yaweza kufisidiwa na hivyo kutowafikia walengwag) Kushiriki Katika Kazi ya Fasihi Simulizi k.v. ngoma, soga, n.kUmuhimuKuweza kupata hisia halisi za uwasilishajiKupata habari za kutegewa na kuaminikaNjia bora kwa wasiojua kusoma na kuandikaKukuza utangamano wa mtafiti na wanajamiiKuweza kunasa na kuhifadhi sifa za kiimbo, toni na isharaUdhaifuKuchukua muda mrefuUgeni wa msanii kusababisha washiriki kuwa na wasiwasi na kutotenda kama kawaidaNjia ghali kwa kuhitaji mtafiti kusafiri mbaliMtafiti aweza kusahau kwa kuhifadhi akilinih) Kutumia HojajiUmuhimuGharama ya chiniYaweza kutumika katika mahojianoHuokoa muda kwani mtafiti aweza kuituma na kuachia mhojiwa kujazaUdhaifuUtata wa maswali kusababisha majibu yasiyo sahihiSi nzuri kwa wasiojua kusoma na kuandikaKutopata sifa za uwasilishaji kama vile kiimbo, toni na isharaWahojiwa kukataa kuijaza kutokana na mwelekeo hasi dhidhi ya hojaji na hivyo kukwamiza utafitiVifaa vya Kukusanya Fasihi Simulizi na Udhaifu WakeVinasa sauti/tepu rekodaKameraFilamu na videoDiski za kompyutaKalamu na karatasiUmuhimuKuweza kudumu na kufikia vizazi vingiSi rahisi kusahaulika-hubakia vile vileSi njia ghali kama vile videoUdhaifuSifa za uwasilishaji kama vile toni, kiimbo/toni na ishara haziwezi kuhifadhika hivyo kupoteaHupunguza hadhira kwa kulenga tu wanaojua kusoma na kuandika na hivyo kuathiri usambazaji wakeMbinu za Kuhifadhi Fasihi Simulizia) Huhifadhiwa na binadamu akilini k.m. ngano hupokewa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.b) Katika maumbile au mazingira k.m. fisi daima huchechemea , kinyonga naye hutembea pole pole.c) Katika vifaa meme k.m. nyimbo, hadithi, maigizo n.k. huweza kuhifadhiwa katika kanda za sauti, video, sidi na diski za kompyuta.d) Katika michoro k.m. picha huhifadhi matukio maalum k.v. za kabila fulani likiwinda au likisherehekea.Umuhimu wa Kukusanya / Kuhifadhi Fasihi SimuliziIli isipotee k.m. kwa kusahaulikaKuirekodi ili kuiendeleza kwa kuirithisha kwa vizazi vijavyoIli kulinganisha fasihi simulizi za jamii mbalimbali na kuonyesha tofauti zakeIli kuhakikisha mtiririko katika uwasilishajiKutunza historia ya jamii ili vizazi vijavyo viijueIli kuziba mapengo ya utafiti yaliyomo kwa vile kuna tungo ambazo hazijatafitiwa kwa kinaKuendeleza elimu ya jadi ya jamiiKuingiliana na jamii iliyo chanzo cha fasihi humwezesha kuelewa na utamaduni na fasihi yake kwa ujumlaHumwezesha mwanafunzi kuona vipengele hai vya fasihi k.v. uigizaji, toni na kiimbo ambavyo husaidia kuielewa kwa kinaHusaidia kuhifadhi tamaduni za jamii kwa nia ya kuzipitisha kwa vizazi vijavyoHusaidia kuelewa utamaduni wa jamii nyingineHumwezesha mwanafunzi kupata maarifa ya kufanya utafiti katika taaluma nyingine k.v. sosholojiaKujua fasihi simulizi za jamii nyingine humfanya mtafiti kuzielewa na kuzikubali jamii hizo na hivyo kuendeleza amani katika nchiIli kusahihisha mawazo mapotovu kuhusu baadhi ya tanzu na vipera vya fasihi simuliziMatatizo Yanayomkabili Mkusanyaji wa Fasihi SimuliziGharama ya utafiti kuwa kubwa kiasi cha mtafiti kutoimudu k.v. kusafiria, kununulia vifaaKutojaziwa hojaji kutokana na mtazamo hasi wa jamii dhidi ya ujazaji wakeWanajamii kukataa kutoa habari wakishuku mtafiti anawapeleleza au kwa kuona hayaWanajamii wengine kudai walipwe kabla ya kutoa habari na hivyo kukwamiza utafitiMbinu nyingine k.v. hojaji huhitaji watu wanaojua kusoma na kuandika na ikiwa mhojiwa hajui utafiti utakwamizwaUchache wa wazee na wataalamu wa fasihi simulizi kusababisha kukosekana au kupatikana kwa data isiyo ya kutegemewaUtawala kukataa kutoa idhini ya kufanya utafitiKukosa ufadhili na utafiti kutofanywa kwa kutomudu gharamaMuda wa utafiti kutotosha na hivyo kutopata habari za kutosha kuhusiana na mada yakeKikwazo cha mawasiliano ikiwa mtafiti na mhojiwa hawatumii lugha moja na mhojiwa hajui lugha nyingine na kumbidi mtafiti kukodi mkalimani na gharama kuongezekaUkosefu wa vyombo vya usafiri kunakochelewesha utafiti na kutomalizika katika muda uliopangwaUkosefu wa usalama k.v. kuvamiwa kwa kushukiwa anapeleleza na kuibiwa vifaaChangamoto Zinazokabili Ukusanyaji wa Fasihi SimuliziUkosefu wa utafiti wa kutosha kwani kuna vipera ambavyo bado havijaandikwaUchache wa wataalamu wa kutafitia na kuendeleza utafitiWatu kuhamia mijini na kuingiliana na wa jamii nyingine na kufanya uhifadhi na urithishaji wa fasihi kutowezekanaMtaala wa elimu kupuuza lugha ya kiasili inayotumiwa kuhifadhia na kurithisha fasihi simulizi na hivyo kukatiza ukuaji wakeFasihi simulizi kuhusishwa na ukale na hivyo kutoona haja ya kuirithisha na kuihifadhiKuhifadhiwa kwa fasihi simulizi akilini kusababisha kusahaulika, kubadilika hata kufa kwakeJinsi Jamii ya Sasa Inavyojaribu Kuhifadhi Fasihi SimuliziTamasha za muziziki kunakokaririwa na kuimbwa mashairiSherehe za arusi, jando, mazishi mawaidaUtegaji na uteguaji wa vitendawili kupitia redio na runingaSarakasi za wasanii huhifadhi kipera cha vichekeshoNgoma za kienyeji kama isukuti katika hafla za kisiasa na harusiUtambaji wa hadithi hasa katika sehemu za mashambaniTanzu za Fasihi Simulizi– Tanzu ni aina za tungo zenye muundo uliokaribia kufanana.HadithiSemiUshairiMazungumzoMaigizoTagged:FasihiFasihi SimuliziKiswahili KENotes Next - Kiswahili KE Hadithi