Faraja ya Usichana Usichana na Ukuaji Estimated reading: 7 minutes 118 views UsichanaMaelezo Juu ya UsichanaASIKUDANGANYE mtu rafiki yangu, utoto una raha zake, ndiyo maana mara kadhaa unasikia watu wanasema wanatamani kurudi utoto. Kwanza ni kuhusu huduma, hakuna bughudha na fikiria pale baba au mama anapokufuata shuleni kukuchukua ili kukurudisha nyumbani. Au pale unaporejea kutoka shule na kukuta mama amekwisha aandaa msosi, unajichana halafu unaenda kucheza, kweli ni raha tu. Kudeka kama kazi, huku umekunja mashavu kama umenyimwa hela ya kununua pipi!Lakini miaka inasonga mbele na mambo yanabadilika na hata lile jina ‘mtoto’, taratibu linaanza kupotea na hapo unaonekana umekua. Kweli unafikia wakati unalazimika kuuaga utoto, hakuna ujanja kwa sababu kama unataka kuendelea kubaki mtoto sasa utakuwa unang’ang’ania tu. Basi tuachane na hayo kwa kuwa sasa mwenzio nimekua wacha nikupe stori za kikubwa, maana tayari nimeshaondoka kwenye huo utoto.Turudi kule darasani, shoga, hamu yangu yote ya kuwa kama Sara iliniisha siku hiyo. Akiwa amekaa ametulia tuli, mara ghafla ukelele mmoja wa kushtua ulitoka kwa mmoja wetu akisema, ‘Sara! Sara! Vipi! Damu!’ Hali hiyo ilinitoa kwenye mawazo yangu ya kuhakikisha nafanya vizuri zoezi la hisabati, nikalazimika kuinua macho kutazama kuwa kulikoni Sara, loh! Alikuwa na doa nyuma ya sketi yake.Sikuelewa, Sara kimemsibu nini, niliporudi nyumbani nilimsimulia dada yangu mkubwa, yeye akanieleza: Sara amevunja ungo, hii ni dalili ya kukua/kubalehe. Nami nikamuuliza dada anieleze mabadiliko nitakayoona mwilini kama dalili za kukaribia kuvunja ungo, walau nijiandae mapema kabisa, jambo hili nisingependa linikute bila maandalizi yoyoteMabadiliko ya mwili yanayotokeaMaelezo Juu ya Mabadiliko ya Mwili YanayotokeaMatitiHukua, yanavimba na kuuma kidogo. Mara nyingine moja huwa dogo kidogo kuliko jingine.Kwapa, UkeHuota nywele makwapani na kuzunguka uke. Wingi wa nywele ni tofauti kwa kila msichana, wengine ni chache wengine ni nyingiUso (Ngozi)Uso hupendeza zaidi, ngozi huwa na mafuta mengi yanaweza kusababisha chunusi kwa wasichana wengine. Hali ya chunusi inaweza ikasumbua hadi kwenye miaka ishirini hivi, halafu ikatoweka.NyongaHupanuka, ndiyo sababu yule rafiki yangu Sara alikuwa na kishepu cha kimama, kilichowasumbua wavulana. Mabadiliko haya hutokea ghafla kwa kipindi kifupi kabla ya kuvunja ungoUrefuUrefu huongezeka na uzito pia huongezeka. Wasichana kimaumbile hurefuka na kukua haraka kuliko wavulana tunaolingana nao umri kwenye miaka ya 15 hadi 17. Wavulana wanakuwa na kutupita miaka ya 17 hadi 19.Tezi za jashoJasho huzidi kutoka kuliko awali na kiharufu cha jasho kinaanza. Hii ni kawaida, cha msingi ni kuzingatia usafi.SautiHubadilika kuwa nyororo au kukaza kidogo. Si wote na sauti nyororo hii ni tofauti ya maumbile tu.Hatimaye…Wasichana huvunja ungo kati ya miaka 9 hadi 15 na kipindi hiki chote mwili unajiandaa kwa mabadiliko ya kuwa mtu mzima. Damu huanza kutoka ukeni kila mwezi kwa siku 3-7, inategemea na kila msichana. Kama tulivyoona katika yale mabadiliko yanatokea mwilini. Msichana anapofikia hapa ana uwezo wa kupata mimba.MIMI NA MWILI WANGU ULIVYO: KABLA NA BAADA YA KUBALEHEMzunguko wangu wa MweziMaelezo Juu ya Mzunguko wangu wa MweziNeno mzunguko humaanisha vitu/matukio yanayojirudia-rudia ki mduara. Hapa nina maana ya mwanzo wa hedhi katika mwezi mmoja mpaka inapoanza tena mwezi unaofuata.Tuchukue mifano hii:Mzunguko huu kwa wanawake walio wengi ni wa siku 28, unahesabu siku ya kwanza uliyoanza hedhi mwezi huu hadi siku moja kabla ya kuanza hedhi mwezi unaofuata. Wachache wana mzunguko wa siku 21 na wengine wa siku 35. Hii ni aina tofauti ya maumbile wala si ugonjwa. Hata hivyo ili kupata wastani kamili na wa uhakika wa mzunguko wako, unatengeneza kikalenda chako cha siri utakachoweza kurekodi vizuri siku za hedhi za kila mwezi kwa miezi sita (6).Utahesabu kila mwezi mzunguko wake, utajumlisha mizunguko ya miezi yote sita (6) na kuigawa kwa sita (6). Kwa mfano:Januari siku 26, Februari siku 28, Machi siku 31, Aprili siku 33, Mei siku 29, Juni siku 28.Jumla siku 175 ÷ miezi 6 = siku 29Kwa hiyo mzunguko wa uhakika ni siku 29Vile vile tukichukulia alama za barabarani:NYEKUNDU- Daima huashiria hatariKIJANI- Ni rangi ya usalamaNJANO- Huweka tayari rangi ya maandaliziMfano wa mzunguko wa mwezi:Nyekundu:Hizi ni siku ambazo yai limeshakua, na mji wa mimba umeanza kujengeka ili kukaribisha mimba. Yai husafiri kutoka kwenye kokwa hadi kwenye mji wa mimba kupitia kwenye mirija ya kupitishia mayai. Iwapo litakutana na kuungana na mbegu ya kiume, mimba itatungwa, kisha husafiri kukaa kwenye mji wa mimbaIshara ya mwili:Maji maji yenye kuteleza hutoka na kukufanya ujisikie kama umelowa. Maji maji haya ni kama ute unaovutika mithili ya yai bichi au mlenda.Kijani:Siku hizi huitwa siku salama, pengine zilipata jina hili kwa sababu huwezi kushika mimba kwenye siku hizi. Huwa ni baada ya hedhi ambapo yai halijapevuka kwenye kokwa.Baada ya siku hatari, uke huwa mkavu na hizi pia huwa ni siku salama kwani baada ya siku kadhaa yai husinyaa na litatoka na damu ya hedhi.Njano:Njano iliyo karibu na nyekundu inaashiria uwezekanao wa yai kuwa tayari kurutubishwa. Njano iliyo karibu na hedhi, ni kipindi ambacho mwili upo katika maandalizi, kiuno na mgongo unaweza kuuma, chunusi hutokea, kichwa kuuma.UsafiUsafi ni MazoeaMojawapo ya sifa kubwa za mwanamke ni usafi, ni muhimu tuelewe kuwa usafi ni mazoea unayojijengea. Kipindi hiki tuzingatie usafi, viharufu vya ajabu-ajabu vitatuumbua.Jasho:Jasho kali au kikwapa ni kutokana na kemikali zilizoko mwilini zinazobadili mfumo mzima wa via vya uzazi. Humo mwilini, vitu vipo kazini kama kiwanda.Uoge walau mara moja kwa siku lakini ni bora ikawa mara mbili hasa siku za hedhi au angalau nawa sehemu zako za siri walau mara mbili kwa kutwa.Nyoa nywele za kwapani mara kwa mara na kusafisha vizuri na sabuni wakati unapooga. Tumia “deodarant’ mafuta ya kukausha jasho na kuondoa harufu kwapani.Yanapatikana kwa wingi kwenye maduka mbalimbali hata yale ya mtaani kwako.Ogea sabuni ya magadi inakata jasho na harufu kwapani zinapatikana kwa wingi kwenye maduka mbalimbali hasa yale ya magerezaPEDI/ KITAMBAA (SODO)/ PAMBA:Hivi vitu hatupaswi kuviweka hovyo hovyo hasa tukiwa shuleni, kama mnavyojua wavulana hupenda sana kututania hasa kama watabahatika kuviona na pia si vizuri ili kulinda hadhi na heshima ya mwanamke.Damu ya mwezi ikutanapo na hewa hubadilika harufu na kunuka kama kitu kilichooza , hivyo basi, badilisha pedi/kitambaa(sodo)/ pamba kila baada ya saa nne (4) kupita ukizingatia hedhi yako na wingi wake. Kama unatumia kitambaa (sodo) kifue hadi kitakate, kitoke doa la damu. Kama unatumia pamba au pedi usitupe kwenye choo cha kuvuta, huweza kusababisha choo kuziba.Usitupe nje jalalani, maana mbwa na paka huweza kuviburuzia kwa watu. Unaweza kuchimbia chini au kuchoma moto.Hakikisha nguo zako za ndani ni safi kwa kubadili mara mbili au tatu kwa siku kwa uhakika zaidi.Tembea na pedi/ kitambaa/ pamba ukaribiapo siku zako ili kuepuka fedheha ya kuanza hedhi na kuchafuka hadharani.Usafi, usafi, usafi ni mazoea unayoweza kuyajenga iwapo utajipenda,nawa sehemu zako za siri kila unapobadilisha pedi/ pamba/ kitambaa chako. Vile vile usiache kunawa vizuri mikono yako.Njia PandaWASICHANA wengi katika kipindi chetu cha ukuaji hasa miaka michache baada ya kuvunja ungo, hatuna utaratibu maalumu wa mzunguko wa hedhi, mwezi huu inaweza ikawepo na mwezi ujao isiwepo. Mara kwa mara, mzunguko hubadili siku zake kiasi kwamba huwezi kujua siku zipi yai linarutubishwa na siku zipi unakaribia kuanza tena hedhi. Hali hii si ugonjwa bali ni hali ya kawaida, via vya uzazi huwa havijakomaa sawasawa. Cha msingi, ni kuwa makini na mwangalifu bila kuiwekea asilimia 100 kalenda yako. Mimi nikikaribia hedhi nasononeka sana kwa sababu ya maumivu makali ya tumbo.Maumivu hayo nayapunguza kwa kufanya yafuatayo:Kunywa maji moto kwa wingi siku mbili kabla ya kuanza hedhi.Kufanya mazoezi ya viungo kuwezesha mvutano wa misuli katika tumbo la uzazi kutokuwa mkubwaWachache hunywa dawa na husema zinawasaidia kupunguza maumivu ambazo ni Panadol na Buscopan ingawa si vyema kujenga mazoea ya kutumia dawa kila maraPia…1. Ninamfahamu msichana mmoja aliyekuwa akitoka damu ya hedhi hata wiki mbili mfululizo, hili ni tatizo la homoni huwa zinazidiana mwilini na ni vizuri kwenda mapema kwa daktari wa magonjwa ya wanawake kwa msaada wa kitaalamu2. Miezi mingine inapita bila kuwa na hedhi, usiogope, usiingiwe na hofu na hali hiyo kwa kuwa husababishwa na:Mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa.Kama uliugua sana kwa muda mrefu, au kwa maumivu makali sana.Mwanzoni mwa kuvunja ungo, mzunguko huwa hauko sawa mpaka baada ya mwaka hata zaidi.Habari zilizo kushtua hasa za huzuni.3. Wasichana wengine wanafikia miaka 18 bila kuvunja ungo. Hawa ni muhimu kumuona daktari wa magonjwa ya wanawake mapema.YOTE HAYA NI KENDA LA KUMI NAJIVUNIA KUWA MWANAMKETagged:ExtracurricularNotesUsichana Next - Faraja ya Usichana Msichana na Jamii