Faraja ya Usichana Msichana na Jamii Estimated reading: 4 minutes 98 views Ukuaji wangu na JamiiMaelezo ya ukuaji wangu KijamiiKijamiiNilionekana ghafla mtu mzima na kutoeleweka pale nilipoendelea na michezo ya utotoni.Majukumu yangu nyumbani yalibadilika pia kwani sasa nilianza hata kuwapikia chakula tofauti na ilivyokuwa hapo awali.Niliachiwa wadogo zangu kuwaangalia, kuwafulia, kuwapeleka shuleBibi yangu kila mara alinikanya kuhusu nguo zangu tena alisema “Umekua sasa, Si vizuri kuvaa nguo fupi na zinazoonyesha maumbile yako”Nilifokewa kuhusu kuongea mara kwa mara na kucheza na wavulanaKatika kukua nikatambua haya:Hakuna mtu asiyejua kuwa wewe bado ni mtoto, jitahidi kuweka ratiba ya kila kitu ili hata muda wako wa kucheza ubaki palepale, shoga ndio ukubwa huo. Ujue, kucheza ni mazoezi ambayo ni muhimu kwa afya yakoMama au bibi anafurahia sana kumuona bintiye amekuwa mtu mzima, naomba uwaelewe, hivyo basi hupenda kukuandaa kuwa mwanamke au mama bora. Ni vyema akina mama na akina bibi wawe wazi kwa wasichana. Ukweli ni kwamba nyumba nzuri huwa na msingi mzuri pengine hata wewe ukijaliwa kuwa mama utafanya hivyo-hivyo kwa bintiyoKisaikolojiaNilikuwa njia panda, utoto naupenda na ukubwa nautaka, kote kulinivuta na sikuelewa nikimbilie upande upi hasa.Hata kama nimekuwa mkubwa sikujua nifanyeje, kwani wakubwa wakoje? Lakini mbona mimi ni mdogo?Mpenzi wangu hata wewe yanakukuta haya hata kama ni mfumo tofauti kidogo, haya basi tusaidiane:Hata yule anayepandishwa cheo akiwa na miaka 40 anakuwa na hali hiyo hiyo ya kuogopa kuvuka hatua nyingine kutokana na mazoea aliyojenga sehemu aliyopo. Utakutana na hii hali mara nyingi maishani, uizoee na kuwa jasiri.Hakuna tabia ya mtu iliyo rahisi kuiga. Kitu kizuri ingawa kigumu maishani ni kuwa wewe mwenyewe na uhalisia wako, inapendeza na ni bora zaidi kama ukihakikisha hauigi mambo ya mtu fulani. Unatakiwa ujikubali, ujipende na pia ujivunie kuwa wewe. Uwe mdadisi wa kuelewa mambo na kujifunza yaliyo ya manufaa kwako.Uhusiano na wengineMh, Adam siku hizi anavutia sana yaani ni mtanashati ile mbaya halafu mcheshi na tulimchagua kuwa kiranja darasani kutokana na jinsi alivyo. Akisimama mbele ya darasa mikono yangu inatoa jasho.Nawaonea aibu wavulana, wakikaa kwenye kundi njiani, niko radhi nibadilishe njia kuwaepukaBasi bwana, siku moja Adam alitumwa na mwalimu kuniita. Akaja kunichukua kwa kunishika mkono, siwezi kukueleza nilivyojisikia mpaka kesho sikumbuki alichonieleza mwalimu siku hiyo manake mawazo yote yalikuwa mkononiRafiki yangu huu ni wakati ambao hisia juu ya jinsi ya kiume huanza kujitokeza kwa nguvu sana.Huo, mpenzi wangu, ni mvuto wa kawaida si tamaa. Usiruhusu ukutawale.Usiwaogope wavulana, wachukulie kama marafiki wa jinsia moja hii itakusaidia kujenga kujiamini ndani yako.Tafuta unachopendelea (hobby), michezo au masomo utakayoweza kuzingatia ili kupoteza hizo fikra.Ongea na mama au dada juu ya hali hiyo kwa sababu wanakupenda na hawawezi kukupotosha kamwe.Siyo kila kitu utakachosikia ni cha kweli kuhusu uhusiano na afya ya uzazi, tukiwa shuleni kila mtu ana tabia zake; kuigaiga mambo, hicho si kitu kizuri, jifunze kuiamini dhamira yako.Ukuaji wangu KiuchumiMaelezo ya ukuaji wangu KiuchumuKiuchumi:Ukigeuka kushoto Rehema anaringa na saa yake mpya, kanunuliwa na mpenzi wake. Jana alikuja na mkebe (kompasi) mpya kabisa alisema kanunuliwa pia.Kuna anko kila nikitoka shule namkuta kwenye kona ndani ya gari ananisubiri. Siku ya kwanza alivyoniita alinipa 10,000/= nilifurahi kwa sababu nilihitaji kununua vitu vingi lakini baadaye nikaogopa.Maisha hayana njia ya mkato, tamaa ikiendekezwa tutayakatisha maisha yetu mazuri tena kwa mwisho mbaya.Kila kitu kina wakati wake, pesa zipo na zinakungoja iwapo utakuwa na bidii shuleni na kuweza kutumia akili yako utazipata.Ukizoea kupewa hela za bure hautaweza kukaa na kujifunza kuzitafuta mwenyewe kwa kufanya kazi. Na kama hizo za bure zitaacha kuja kwa njia hiyo basi utataabika mno na hata kuingia kwenye vishawishi ambavyo ni hatari zaidi kwa afya na maisha yako kwa ujumla.Mtu anayetoa hela ili umpende maana yake hakuthamini na amekuchukulia kama ng’ombe kwenye mnada, dau la mnunuzi linapanda muuzaji anapozidi kukataa.Usiuze utu wako kwa vilifti, viji-chipsi kuku, simu, ice cream, urembo na kadhalika. Jipende na kuwa jasiri hayo ni majaribu tu ya nafsi unayoweza kuyaepukaTagged:ExtracurricularMsichana na JamiiNotes Faraja ya Usichana - Previous Usichana na Ukuaji Next - Faraja ya Usichana Msichana na Mahusiano