Comment

Darasa Huru

Darasa Huru

Limitless Potential

A smarter way to study—free, fast, and comprehensive.

Topic

Ufahamu

Estimated reading: 4 minutes 67 views

Summary: Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma.

Kiswahili Kidato cha Kwanza

Jedwali la Yaliyomo

  1. Kusikiliza
  2. Kusoma kwa Sauti
  3. Kusoma Kimya
  4. Kusoma kwa Burudani

Kusikiliza

Ufahamu wa Kusikiliza

Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa mfano, mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe.

Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa Kusikiliza

Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha:

  • Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa.
  • Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusika anayezungumza.
  • Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa.

Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafuatayo:

  • Kuwa makini: Elekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila anachokisema.
  • Vidokezo vya maana: Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji anaongeza jambo jipya, anatofautisha, anafafanua au anahitimisha hoja.
  • Kuandika mambo muhimu: Andika baadhi ya mambo anayoona kuwa ni ya muhimu ili kumasidia kukumbuka hapo baadaye.
  • Ishara za mwili: Kuwa makini na ishara mbambali za mwili kama vile kurusha mikono, kutingisha kichwa, kutingisha mabega au hata kupepesa macho. Ishara hizi huwa zinachangia kwa kiasi kikubwa kupata maana katika mazungumzo.

Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyosikiliza

Jibu maswali kutokana na habari uliyosikiliza.

Activity 1

Jibu maswali kutokana na habari uliyosikiliza.


Kusoma kwa Sauti

Kusoma kwa sauti ni namna ya kuyaangalia maandishi na kuyatamka kwa sauti inayosikika.

Mambo ya Kuzingatia katika Ufahamu wa Kusoma

Kuna vipengele viwili vinavyounda mchakato wa ufahamu wa kusoma:

  • Uelewa wa msamiati: Uwezo wa kuelewa msamiati uliotumika katika matini hiyo. Endapo maneno yaliyotumika hayataeleweka, matini yote haitaeleweka.
  • Uelewa wa matini: Ili kuelewa habari/matini, msomaji anatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
    • Mawazo makuu: Kubaini mawazo makuu; msomaji anaposoma habari fulani au kitabu, inatakiwa ajiulize, “Je, kinachoongelewa hapa ni nini? Ni jambo gani hasa analolizungumzia mwandishi?” Maswali haya akilini mwake yatamsaidia kuelewa habari hiyo.
    • Alama za uakifishi: Kuzingatia alama za uakifishi; kwa kufanya hivyo, itamsaidia kuelewa ujumbe wa habari hiyo na endapo hatazingatia alama za uakifishi, anaweza kupotosha maana ya mwandishi.
    • Maana ya maneno na misemo: Kubaini maana ya maneno na misemo mbalimbali; habari nyingine huwa zina maneno ya kisanaa, hivyo ni muhimu msomaji kubaini maana ya maneno hayo katika muktadha wa habari hiyo, itamsaidia kuelewa vyema maana ya mwandishi.
    • Kumakinikia: Msomaji anatakiwa kumakinikia kile anachokisoma, kila kipengele anachokisoma inampasa akielewe vizuri.

Kwa kuzingatia haya yote, msomaji atakuwa na uelewa mzuri juu ya habari aliyoisoma na pia anaweza kufupisha habari hiyo aliyoisoma.

Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyosoma

Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma.

Activity 2

Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma.


Kusoma Kimya

Katika usomaji huu, msomaji hufumba kinywa na kupitisha macho katika kila mstari haraka haraka. Macho hayo huunganisha neno lililotangulia na lile linalofuata. Ubongo wake huchambua mambo muhimu yanayojitokeza, huku akiyahifadhi kichwani. Mtu akijizoeza kusoma kimya, ananufaika ifuatavyo:

  • Hupata nafasi ya kupima mwendo wake na kiasi cha welewa.
  • Hujiepusha na lawama ya kusumbua wengine.
  • Hukwepa kuzingatia kanuni za matamshi.
  • Huweza kusoma maandishi mengi kuliko ambavyo angesoma kwa sauti.

Kujibu Maswali kutokana na Habari uliyoisoma

Jibu maswali kutokana na habari uliyosoma.


Kusoma kwa Burudani

Huu ni usomaji ambao lengo lake kuu huwa ni kujiburudisha tu. Katika usomaji wa aina hii, msomaji hujisomea zaidi magazeti, majarida, na vitabu tofauti na vile vinavyotumika darasani.

Mambo ya Kuzingatiwa katika Ufahamu wa Kusoma kwa Burudani

Wakati mwingine sio lazima msomaji awe na vitabu vyote ambavyo anahitaji kuvisoma au magazeti na majarida. Inapotokea hivyo, msomaji anaweza kwenda maktaba kuazima kitabu anachokihitaji.

Ingawa lengo la msomaji huwa ni kujiburudisha tu, lakini pia hujiongezea maarifa. Hii ni kwa sababu, magazeti, majarida, na vitabu, sambamba na kutumia lugha sanifu, huelezea mambo mbalimbali yanayoihusu jamii. Hivyo msomaji kutokana na kusoma vitabu na majarida mbalimbali hujiongezea kiwango cha welewa wa lugha na mambo mengine ya kijamii yanayojadiliwa humo.

Ni jambo zuri kwa msomaji kujijengea tabia ya kujipima ili aweze kuelewa kiwango cha maarifa aliyopata katika kujisomea. Kujipima huku kunaweza kufanywa kwa kujiundia utaratibu wa kuweka kumbukumbu ya vitu au makala zilizosomwa na kufanya ufupisho wa kila makala.

Utaratibu wa Kujipima na Kuweka Kumbukumbu

  • Tarehe: …
  • Jina la kitabu/makala/gazeti: …
  • Mchapishaji: …
  • Mwaka/tarehe ya uchapishaji: …
  • Ufupisho wa habari: (yasizidi maneno 20)
  • Fundisho/ujumbe mkuu ni: …
  • Jambo lililokuvutia sana: …
  • Maoni kwa ujumla kama yapo: …

Leave a Comment

Share this Doc

Ufahamu

Or copy link

CONTENTS

Agricultural Development

What is Agriculture? Agriculture refers to a fundamental human activity, which i...

Population and Development

POPULATION STUDIES Is the general activities carried out for the purpose of acqu...

Study of Soil

CONCEPT OF SOIL AND SOIL PROFILE Soil appears very complex and thus differe...

Water Masses

GROUND WATER WATER CYCLE Rain falls on the earth surface in filtrates (soaks int...

Topic

The Dynamic-Earth And Consequence

THEORIES THEORY OF ISOSTASY Denudation has been going on the continents where to...

Position Behaviours And Structure Of The Earth

GLOBE Is the model of the earth Earth Is ball of rock partly covered by wat...

Photograph interpretation

Photograph are the true image pictures showing truly appearance of the earth’s...

Maps and map interpretation

What is a map? Map is a scaled conventional representation of the whole or any o...

Simple survey and mapping

INTRODUCTION TO SURVEYING Surveying is an art or a science of measuring and reco...

Field research techniques

Definitions of Research – Research is the systematic investigation into a...

Application of statistics in geography

STATISTICS Statistics is a branch that deals with every aspect of the data. Stat...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel