Comment

Darasa Huru

Darasa Huru

Limitless Potential

Your academic success starts here — free notes, books, and more.

Topic

Matumizi Ya Lugha Katika Miktadha Mablimbali

Estimated reading: 13 minutes 59 views

Summary: Matumizi ya lugha ni namna ambavyo wazungumzaji wa lugha hutumia lugha kwa kuzingatia mila, desturi na kaida mbalimbali za jamii inayohusika.

Rejesta

Kwa ujumla, tunaweza kufasili rejesta kama mtindo wa lugha unaotegemea kazi fulani, muktadha wa matumizi, lengo, na uhusiano wa wanaowasiliana. Katika muktadha rasmi, rejesta hurejelea upande mmoja kama vile msamiati wa kiufundi, adabu maalum, na matumizi ya lugha fasaha, mfano katika elimu, mahakamani, na kadhalika.

Kuwasiliana kwa Kutumia Rejesta

Rejesta za Mitaani

Haya ni mazungumzo yanayozungumzwa magengeni na hueleweka na wazungumzaji wenyewe. Ni lugha ambayo huchipuka kutokana na kikundi kidogo cha watu. Mfano wa maneno yanayotumika sana mitaani ni kama vile “mshikaji” (rafiki) na “demu” (mwanamke). Kwa ujumla, lugha ya mitaani ni lugha isiyo sanifu, iliyojaa maneno ya mitaani ambayo yanaeleweka kwa wazungumzaji wenyewe.

Mazungumzo ya Kwenye Shughuli Maalum (Rejesta za Mahali)

Mazungumzo ya kwenye shughuli maalum hayafanywi kiholela, bali yanafuata taratibu na kanuni maalum zinazojitokeza katika mazingira haya kutokana na kutumiwa kwake kwa muda mrefu kwenye mazingira yale yale.

Mazungumzo ya kwenye shughuli maalum ni kama vile mazungumzo ya:

  • Maofisini au mahali popote pa kazi
  • Mahakamani
  • Hotelini
  • Hospitalini
  • Msikitini
  • Kanisani, n.k.

Mazungumzo ya mahotelini yana utaratibu wake ambao katika hali ya kawaida unaweza usieleweke. Kwa mfano:

A: Nani wali kuku?
B: Mimi
A: Chai moja wapi?
B: Hapa

Katika mazungumzo haya, A anapouliza “Nani wali kuku?”, ana maana ya nani anahitaji kula wali na nyama ya kuku. Hapa hana maana ya kumwita mtu aitwaaye “wali kuku”.

Kwa upande wa lugha ya mahakamani, ni tofauti na lugha ya hotelini. Lugha ya mahakamani inasisitiza usahihi ili kuondoa migongano miongoni mwa wanaohusika.

Mfano:
Wakili wa Utetezi: Nakuuliza, jaribio la kutaka kupindua serikali litakuwa kosa la namna gani katika sheria za Tanzania?
Kamishna Msaidizi: (Baada ya kupewa kitabu cha sheria za Tanzania na kukisoma) Ni kosa la uhaini.
Wakili wa Utetezi: Ulichukua muda mrefu kufikia jibu hili. Washitakiwa wawili hawahusiani na makosa haya?
Kamishna Msaidizi: Sijui.

Kimsingi, hii ni hali ya kawaida kabisa katika mahojiano ya mahakamani. Mara nyingi mahojiano hayaendi haraka sana. Kila mtu anayehusika – hakimu, mwendesha mashtaka, wakili, mdaiwa, shahidi, n.k. hujieleza kwa uwazi bila kujali urefu wa maelezo.

Rejesta Zinazohusu Watu

Rejesta zinazohusu watu ni yale mawasiliano yasiyo rasmi, ni maongezi ya kawaida ya kila siku au mazungumzo rasmi; kwa mfano, mazungumzo kati ya:

  • Vijana wenye rika moja
  • Wazee wenyewe
  • Wanawake wenyewe
  • Wanaume wenyewe
  • Mwalimu na mwanafunzi
  • Meneja na wafanyakazi wake
  • Mtu na mpenzi wake, n.k.

Mazungumzo miongoni mwa marafiki wa rika moja huzungumza lugha ambayo wao wenyewe wanaielewa na sio rahisi kwa mtu wa rika lingine kuielewa lugha hiyo.

Mfano:
Kijana 1: Niaje? Nakuona umechili.
Kijana 2: Mzuka jembe. Kama kawa… kama dawa!

Maana ya Maneno:

  • Wikiendi – Mwisho wa wiki
  • Kibaridi – Tulivu
  • Kuzamia infoo – Kuingia mahali bila kualikwa
  • Zinga la mnuso – Sherehe kubwa
  • Saiti – Sehemu
  • Baunsa limenyuti chedro – Ni mlinzi wa mlangoni ametulia pembeni
  • Noma – Hatari
  • Mnoko kishenzi – Kinaa sana
  • Mkwara mbuzi – Vitisho dhaifu

Mtu anaposoma maelezo hayo, mara moja unaona jinsi vijana wa rika moja waishio mjini wanavyozungumza Kiswahili. Si rahisi kwa mzungumzaji wa Kiswahili sanifu kuielewa kirahisi lugha hiyo.

Dhima za Rejesta

Utambulisho wa Kijamii

Rejesta ina nafasi kubwa katika utambulisho wa kijamii. Namna ya lugha ya mazungumzo inaweza kujidhihirisha miongoni mwa watumiaji wake au kuwatambulisha na kuwatofautisha wanajamii husika. Pia, tunazingatia namna mtu anavyotambulika katika jamii kulingana na jinsi anavyoongea, kulingana na hadhi, tabaka, na jinsi mtu huyo anavyoweza kusababisha mshikamano au mwachano katika mazungumzo. Kwa mfano, jamii itamtambua mwanajamii kuwa ni msomi kulingana na mtindo wa lugha ya mazungumzo anaoutumia, au ni mtu wa mtaani kulingana na lugha anayotumia.

Maendeleo ya Kiuchumi

Rejesta ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya kiuchumi kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Madhumuni makuu ya mawasiliano katika biashara ni kuwavutia wateja na kuwafanya kuamini kuwa bidhaa ama huduma wanazouziwa ni za kiwango cha juu na ni thamani bora kwa pesa zao. Hivyo, lugha ya biashara (rejesta) kwa kawaida ni lugha ya kutangaza uzuri wa bidhaa au huduma, huwa na sentensi au vifungu vifupi, mfano “Okoa mapesa chungu mbovu” na huwa na lugha ya kupumbaza na kuaminisha, mfano “Kunywa XYZ kufumba na kufumbua afya yako itakurudia”.

Urahisishaji wa Mawasiliano

Rejesta inasaidia kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji katika masuala mbalimbali ya kibiashara na hata katika huduma mbalimbali za kijamii. Mfano hospitalini, “mbili mara tatu”, hotelini, “kuku wali tafadhali”, sokoni, “kata nusu”, na maeneo mengine. Baadhi ya rejesta hutumika kupunguza idadi ya maneno, hivyo kufanya mazungumzo yawe mafupi na kueleweka kwa urahisi.

Elimu ya Dini

Katika kutoa elimu ya dini kanisani na msikitini, rejesta ina nafasi kubwa katika kujenga maadili. Pia, rejesta ina nafasi ya kupamba mazungumzo; wazungumzaji wengi wanapozungumza hupenda kutumia maneno tofauti ili kufanya mazungumzo yawe ya kuvutia.

Misimu

Kuwasiliana kwa Kutumia Misimu

Misimu ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. Misimu inayodumu huweza kuingia katika methali, nahau, au misemo ya lugha ya jamii hiyo.

Chanzo cha Misimu

Misimu huzuka kulingana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii husika katika nyakati mbalimbali. Huzuka kutokana na haja ya watu kuelezea hisia zao juu ya matukio mbalimbali yaliyotokea katika vipindi fulani, kwa mfano, njaa, mafuriko, vita, n.k.

Aina za Misimu

  1. Misimu ya Pekee: Huelezea mahusiano ya kikundi kimoja kutoka katika utamaduni mmoja, na hujulikana miongoni mwao pekee.
  2. Misimu ya Kitarafa: Hujulikana na watu wengi katika eneo kubwa, yaweza kuwa ni kata, wilaya au tarafa.
  3. Misimu Zagao: Ni misimu iliyoenea nchi nzima au pengine kuvuka mipaka ya nchi, husikika redioni, magazetini na hata kwenye vitabu. Misimu iliyokita mizizi sana huweza kusanifishwa na kuwa msamiati rasmi.

Sifa za Misimu

  • Huzuka na kutoweka kufuatana na mabadiliko ya jamii
  • Ni lugha isiyo sanifu
  • Ina chuki
  • Ni lugha ya mafumbo
  • Ina maana nyingi

Dhima ya Misimu

  • Hutumika kupamba lugha
  • Hutumika kukuza lugha
  • Hutumika kutunza historia ya jamii fulani
  • Hutumika kuibua hisia mbalimbali za wazungumzaji
  • Hufurahisha na kuchekesha

Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi

Sifa ya Lugha ya Kimazungumzo

Bainisha sifa ya lugha ya kimazungumzo:

Lugha ya mazungumzo ni maongezi ya watu wawili au zaidi bila kutumia maandishi. Hii ni aina ya lugha kongwe zaidi ya lugha ya maandishi, na ina dhima kubwa ya kufanikisha mawasiliano miongoni mwa watu au kikundi fulani. Ilianza punde tu binadamu alipoanza kukabiliana na mazingira yake, hivyo kimsingi lugha ya mazungumzo ndiyo nguzo kuu ya kufanikisha shughuli zote za kibinadamu kutokana na nafasi yake kimatumizi.

Faida ya lugha ya mazungumzo:

  • Uhusiano wa karibu: Mzungumzaji anaweza kukaa ana kwa ana na msikilizaji, hivyo hukuza uhusiano.
  • Matumizi ya ishara za mwili: Mzungumzaji anaweza kutumia ishara za mwili katika kusisitiza maelezo yake.
  • Uwezo wa kuuliza maswali: Mzungumzaji anaweza kupata nafasi ya kuuliza au kuulizwa maswali.
  • Uwasilishaji wa hisia: Mzungumzaji anaweza kuonesha hisia zake kwa kulia, kupaza sauti, kupunguza sauti, kuonyesha furaha, huzuni au hasira.
  • Maingiliano ya papo kwa papo: Mzungumzaji anaweza kuuliza maswali, kuona hisia za mzungumzaji kwa kusikiliza lugha zinazotolewa na kuangalia ishara za mwili zinazotumika.
  • Urekebishaji wa maelezo: Mzungumzaji anaweza kupata nafasi ya kufuta usemi wake, kuongezea jambo au kutoa maelezo ya ziada.
  • Kubadilika kulingana na mazingira: Mzungumzaji anaweza kubadilisha lugha yake kulingana na mazingira aliyomo.
  • Uhuru wa matumizi ya lugha: Mzungumzaji anao uhuru wa kutumia lugha ya mitaani, misimu kulingana na muktadha.

Matatizo ya lugha ya mazungumzo:

  • Kumbukumbu: Maelezo lazima yahifadhiwe kichwani, hivyo kama mtu hana kumbukumbu, taarifa zilizotolewa hupotea na kusahaulika.
  • Kurudiarudia: Mtumiaji wa lugha ya mazungumzo anaweza kurudiarudia vipengele fulani na hivyo kuichosha hadhira.
  • Kelele: Ujumbe unaweza usieleweka kama unatolewa kwenye kelele nyingi.

Lugha ya Maandishi

Hii ni lugha inayowasilishwa kwa njia ya maandishi.

Lugha ya maandishi hushirikisha pande mbili: mwandishi na msomaji. Lugha ya maandishi sharti iwe fasaha ili msomaji anaposoma maandishi hayo, apate kuelewa kila kitu, yaani asibaki akijiuliza maswali. Pia huambatana na alama za uakifishaaji, hii husaidia maandishi kusomeka vizuri na kueleweka kwa urahisi.

Ubora wa lugha ya maandishi:

  • Mawasiliano ya mbali: Lugha ya maandishi huwawezesha watu walio mbali kuwasiliana.
  • Kustawisha sarufi: Lugha ya maandishi hustawisha sarufi ya lugha na misingi yake, kwa sababu mwandishi anahakikisha kwamba anazingatia vizuri kanuni za kisarufi ili msomaji wake aweze kumwelewa.
  • Uwazi: Ili kuhakikisha maelezo yake yanaeleweka, mwandishi analazimika kuandika kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni na miiko yote ya uandishi.

Udhaifu wa lugha ya maandishi:

  • Ujuzi wa kusoma na kuandika: Lugha hii hutumiwa na wale tu wanaojua kusoma na kuandika.
  • Ukosefu wa msisimko wa lafudhi: Lugha ya maandishi haina msisimko uletwao na lafudhi na matamshi.
  • Ukosefu wa vidokezo vya ziada: Msomaji hukosa vidokezo vingi ambavyo katika lugha ya mazungumzo huchangia katika mawasiliano.
  • Hakuna nafasi ya kupima welewa: Lugha ya maandshi inamnyima mwandishi nafasi ya kupima welewa wa msomaji kwa kuwa hamwoni.

Dhima ya Lugha ya Mazungumzo na Lugha ya Maandishi

Lugha ya mazungumzo na lugha ya maandshi zote zina umuhimu wa pekee katika maisha ya kila siku kwa sababu ndizo zinazowezesha watu kuwasiliana kwa namna mbalimbali. Umuhimu wa lugha ya maandshi pia hutokana na dhima yake kwa watu. Maandishi yanaweza kuhifadhiwa na kusambazwa kwa watu wengi hata walio mbali. Maandishi yanahifadhi kumbukumbu na kwa muda mrefu. Kwa hali hii, watu wa vizazi vingine wanaweza kusoma na kujua mambo yaliyofanyika karne nyingi zilizopita.

Tofauti kati ya Lugha ya Mazungumzo na Lugha ya Maandishi

Lugha ya mazungumzo huwezesha mawasiliano ya ana kwa ana lakini lugha ya maandishi haiwezeshi mawasiliano ya ana kwa ana. Lugha ya mazungumzo haihitaji maandalizi wakati lugha ya maandishi huhitaji maandalizi. Mwandishi atalazimika kupata muda wa kuandika pamoja na kuandaa vifaa kama vile kalamu, karatasi n.k. Lugha ya mazungumzo hailazimiki kuzingatia kanuni za kisarufi, lakini lugha ya maandshi hutakiwa kuzingatia kanuni za kisarufi.

Kipengele Lugha ya Mazungumzo na Lugha ya Maandishi

KipengeleMazungumzoMaandishi
MuktadhaWahusika huonanaWahusika hawaonani
Viungo vya mwili hutumikaHutumikaHavitumiki
MaandaliziHufanyika wakati mmojaHufanyika kabla ya matumizi
MadaHazina uzito mkubwaHuelekea kuwa na uzito mkubwa
Mpangilio wa mada na mawazoHautabiriki. Unaelekea kutokuwa na mtiririko.Hutabirika. Huelekea kuwa na mtiririko.
Mjadala wa madaHauelekei kuwa na kina. Hazichujwi kwa uaangalifu.Unaelekea kuwa na kina. Huchujwa.

Dhima ya Matumizi ya Lugha

Dhima kuu ya lugha ni kupashana habari, ujuzi na maarifa mbalimbali. Vilevile lugha husaidia kujenga uhusiano mwema baina ya watu. Uhusiano huo unaweza kuwa wa kijamii, kielimu, kibiashara, kihuduma, kisiasa, kiuchumi n.k. Kwa hiyo, kujua jinsi ya kuitumia lugha kama inavyotakiwa, kunasaidia kufikisha vizuri ujumbe unaotakiwa bila kuupotosha. Vilevile kunasaidia kuepuka migongano, hasa ya kijamii kwa kuwa utakuwa umetumia lugha kwa mujibu wa mila na desturi za jamii inayohusika.

Mambo ya Kuzingatia Katika Matumizi ya Lugha

  1. Mada inayozungumziwa: Mada za mazungumzo zipo nyingi. Kuna mada za kijamii, kwa mfano ndoa, unyago, mapenzi, kifo, matanga, burudani, muziki n.k. Kuna mada za kibiashara kwa mfano bidhaa, kodi, vibali, fedha, hasara, faida n.k. Kwa hiyo, ili mazungumzo yaweze kwenda vizuri, wazungumzaji wanatakiwa kuzingatia mada husika.
  2. Muktadha wa mazungumzo: Mazungumzo yanaweza kuathiriwa na miktadha tofauti. Kwa mfano kuna miktadha ya kidini, kiganga, huzuni, sherehe, kisiasa, kielimu, kibiashara n.k. Mazungumzo yanaweza kufanyika mjini, kijijini, ugenini, shuleni, dukani, hotelini n.k.
  3. Malengo ya mazungumzo hayo: Malengo ya mazungumzo nayo yanaathiri matumizi ya lugha. Kwa mfano, lengo linaweza kutoa taarifa, kuhoji, kukejeli, kutia moyo n.k. Sasa jinsi lugha itakavyotumika katika kutoa taarifa ni tofauti na itakavyotumika katika kutia moyo au kukejeli.
  4. Uhusiano uliopo baina ya wazungumzaji: Matumizi ya lugha huweza kuathiriwa pia na mahusiano ya wazungumzaji. Kuna mazungumzo baina ya watoto, wanafunzi, wazee, viongozi, marafiki n.k. Upo uhusiano wa daktari na mgonjwa, mwalimu na mwanafunzi, mnunuzi na muuzaji. Kwa hiyo mazingira baina ya pande hizi mbili yatategemea uhusiano wao, kwa hiyo kaida za uhusiano huu utapaswa kuzingatiwa.Kwa hiyo, kwa kuzingatia mambo haya manne, itawafanya wazungumzaji wawe makini katika uteuzi wa maneno, miundo, mifano na kina cha ufafanuzi wa maelezo au habari inayozungumzwa.

Dhima ya Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi

Elezea Dhima ya Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi

Lugha ya kimazungumzo na ya kimaandishi zina dhima kuu katika mawasiliano na maisha ya kila siku. Zina majukumu muhimu yafuatayo:

  1. Kupasha Habari: Lugha hizi hutumika kutoa taarifa na habari muhimu.
  2. Kufundishia Ujuzi: Lugha ni chombo cha kufundishia na kujifunzia ujuzi mbalimbali.
  3. Kujenga Uhusiano: Husaidia kujenga na kuimarisha uhusiano mwema baina ya watu.
  4. Kufikisha Ujumbe: Huwezesha kufikisha ujumbe unaotakiwa vizuri bila kupotosha.
  5. Kuchochea Maendeleo: Lugha ni kichocheo cha maendeleo katika jamii.
  6. Kuhifadhi Historia: Lugha ya maandishi hasa, inasaidia kuhifadhi historia ya jamii.
  7. Kueleza Mawazo na Hisia: Hutumika kuelezea mawazo na hisia za watu.

Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi katika Muktadha Sahihi

Matumizi ya lugha ya kimazungumzo na ya kimaandishi katika muktadha sahihi huongozwa na mambo yafuatayo:

  1. Mada Inayozungumzwa: Mada inaweza kuwa kijamii, kibiashara, kisiasa, nk.
  2. Muktadha au Mahali: Mahali pa mazungumzo yanapofanyika, kama ni mjini, shuleni, n.k.
  3. Malengo ya Mazungumzo: Malengo yanaweza kuwa kutoa taarifa, kuhoji, kukejeli, kutia moyo, n.k.
  4. Uhusiano wa Wazungumzaji: Uhusiano kama wa daktari na mgonjwa, mwalimu na mwanafunzi, n.k.

Activity 1: Tumia Lugha ya Kimazungumzo na ya Kimaandishi katika Muktadha Sahihi

Matamshi na Lafudhi ya Kiswahili

Matamshi ni namna ambavyo mtu anatamka neno au jinsi mtu anavyozungumza lugha. Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani yanayotokana na athari za kimazingira. Hii inaweza kuathiriwa na:

  1. Eneo la Kijiografia: Mahali anakotoka msemaji.
  2. Kabila: Kabila la msemaji linaweza kuathiri lafudhi.
  3. Kundi la Kijamii: Msanii, mwanasiasa, n.k.
  4. Elimu: Kiwango cha elimu cha msemaji.

Sauti za Lugha ya Kiswahili

Sauti za lugha ya Kiswahili hujumuisha irabu na konsonanti, ambazo kwa ujumla huunda sauti 24: irabu tano na konsonanti 19. Matamshi ya Kiswahili hutamkwa kama yalivyoandikwa.

Mkazo

Mkazo ni pale silabi inapotamkwa kwa kukazwa. Maneno ya Kiswahili huwa na silabi moja ambayo hutamkwa kwa nguvu zaidi kuliko silabi nyingine.

Kiimbo

Kiimbo ni utaratibu maalum wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti unaojitokeza katika utamkaji wa lugha fulani.

Aina za Viimbo
  1. Kiimbo cha Maelezo: Mawimbi ya sauti ya usemaji yanakuwa katika mstari ulionyooka.
  2. Kiimbo cha Maulizo: Mawimbi ya sauti yanapanda na kushuka kulingana na aina ya swali.
  3. Kiimbo cha Amri: Mawimbi ya sauti yanapanda zaidi kuliko katika kiimbo cha maelezo.

Lafudhi Mbalimbali za Kiswahili

Lafudhi hutofautiana kutokana na eneo au jamii mbalimbali. Kwa mfano:

  1. Wakuria: “Usiniretee maswara ya ubaguzi wa kikabira hapa.”
  2. Wakongo: “Amemupiga mutoto ya watu juu amemuibia mfaranga makumi mawili.”
  3. Wamakonde: “Ukikaa nchale, ukichimama nchale.”
  4. Wasukuma: “Wewe unakamuaga mang’ombe tu moja kwa moja.”
  5. Wahaya: “Mbona unakuwa kinganganizi, nilishakwambia sikupendi lakini wewe bado unaningangania tu!”

Utata katika Mawasiliano

Utata ni hali ya neno au sentensi kuwa na maana zaidi ya moja.

Sababu za Utata

  1. Neno kuwa na maana zaidi ya moja: Mfano, neno “mbuzi” linaweza kumaanisha mnyama au kifaa cha kukunia nazi.
  2. Kutozingatia taratibu za uandishi: Alama za uakifishaaji zinaweza kubadili maana ya sentensi.
  3. Muktadha wa Matumizi: Maneno yanaweza kuleta maana tofauti kulingana na muktadha.
  4. Utamkaji wa Maneno: Utamkaji unaweza kuleta utata tofauti na maandishi.
  5. Mjengo wa Maneno: Vitenzi kama “piga” vinaweza kumaanisha mambo tofauti.

Mifano ya Utata katika Tungo

  1. Patience amemwandikia Lilian barua: Inaweza kumaanisha Patience ameandika barua kwenda kwa Lilian au kwa niaba ya Lilian.
  2. Umefanikiwa kununua mbuzi?: Inaweza kumaanisha mnyama au kifaa cha kukunia nazi.
  3. Alimkuta amelala kwenye nyumba ya wageni: Inaweza kumaanisha nyumba ya mtu kwa ajili ya wageni au inayomilikiwa na wageni.
  4. Attu ametumwa na Aritamba: Inaweza kumaanisha Aritamba amemtuma Attu au wote wawili wametumwa pamoja.

Leave a Comment

Share this Doc

Matumizi Ya Lugha Katika Miktadha Mablimbali

Or copy link

CONTENTS

Agricultural Development

What is Agriculture? Agriculture refers to a fundamental human activity, which i...

Population and Development

POPULATION STUDIES Is the general activities carried out for the purpose of acqu...

Study of Soil

CONCEPT OF SOIL AND SOIL PROFILE Soil appears very complex and thus differe...

Water Masses

GROUND WATER WATER CYCLE Rain falls on the earth surface in filtrates (soaks int...

Topic

The Dynamic-Earth And Consequence

THEORIES THEORY OF ISOSTASY Denudation has been going on the continents where to...

Position Behaviours And Structure Of The Earth

GLOBE Is the model of the earth Earth Is ball of rock partly covered by wat...

Photograph interpretation

Photograph are the true image pictures showing truly appearance of the earth’s...

Maps and map interpretation

What is a map? Map is a scaled conventional representation of the whole or any o...

Simple survey and mapping

INTRODUCTION TO SURVEYING Surveying is an art or a science of measuring and reco...

Field research techniques

Definitions of Research – Research is the systematic investigation into a...

Application of statistics in geography

STATISTICS Statistics is a branch that deals with every aspect of the data. Stat...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel