Comment

Topic

Utungaji Wa Kazi Za Fasihi Andishi

Estimated reading: 4 minutes 161 views

Utungaji wa Hadithi

Mikondo ya Hadithi

Pambanua Mikondo ya Uandishi wa Hadithi

Kazi za fasihi andishi ni sanaa inayohitaji ubunifu wa mwandishi ili ziweze kuwa na mwonekano wa kisanaa. Fasihi andishi hutumia lugha ya kisanaa, ambayo ni kipengele muhimu sana katika fasihi. Ili kazi ya kifasihi iwe nzuri na ya kuvutia, msanii lazima awe na ubunifu wa hali ya juu katika kutumia lugha, na awe na uwezo wa kupangilia maneno na kuteua maneno yanayobeba ujumbe unaogusa hadhira yake.

Kwa maana hii, mwandishi wa kazi za kifasihi, iwe riwaya au tamthiliya, lazima azingatie sana lugha, kwani lugha ndiyo nyenzo kuu ya usanii wa fasihi kwa ujumla.

Hatua za Kuandika Kazi ya Kisanaa

  1. Kuwa na Kisa/Wazo:
  • Katika jamii kuna mambo mengi yanayotendeka, na msanii anaweza kupata wazo la kiubunifu kutokana na mambo hayo.
  • Fasihi andishi inaonesha yale yanayotendeka katika jamii, hivyo msanii anaweza kutumia fursa hiyo kuweka wazi mambo yanayoendelea.
  • Mfano wa mada ni ufisadi, umasikini, mapenzi, ndoa, maisha binafsi, ushirikina, au falsafa yoyote.
  • Katika hatua hii, msanii pia anaweza kubuni jina la hadithi yake, ambalo litamsaidia katika upangaji wa visa na matukio.
  1. Kuchagua Umbo la Kazi ya Fasihi:
  • Baada ya kupata wazo, msanii anahitaji kuchagua jinsi atakavyoliwasilisha wazo lake: hadithi fupi, riwaya, tamthiliya, ushairi, au utenzi.
  • Uchaguzi wa umbo unategemea uwezo wa msanii katika tanzu hizo. Kila tanzu ina changamoto na urahisi wake.
  1. Kubaini Hadhira:
  • Kujua ni nani anayemwandikia ni suala la msingi sana kwa mwandishi.
  • Hadhira inaweza kuwa watoto, watu wazima, wasomi, wenye elimu ndogo, wakulima, wanasiasa, nk.
  • Hii inamsaidia mwandishi kuteua lugha ya kuandikia, kulingana na hadhira yake.
  1. Kubuni Wahusika na Mandhari:
  • Mwandishi anahitaji kubuni wahusika wa hadithi yake, ambao wanaweza kuwa watu, wanyama, mimea, mazimwi, malaika, nk.
  • Pia ni lazima kubaini mazingira ambamo visa vyote vya hadithi na matukio yatakapofanyika. Mandhari yanaweza kuwa baharini, kijijini, mjini, mbinguni, kuzimu, nk.
  1. Kupanga Msuko wa Visa na Matukio:
  • Msuko wa visa na matukio ni muhimu sana katika usimulizi wa hadithi.
  • Maswali yafuatayo yanaweza kuwa muongozo mzuri katika kupanga ploti: Hadithi itaanzaje? Mgogoro utaanzaje? Ni kati ya nani na nani? Kilele cha mgogoro ni nini? Hadithi inaishaje? Mhusia mkuu atapata ushindi, kushindwa, kufungwa, au kubadilika?
  1. Kuanza Kuandika:
  • Baada ya kupitia hatua zote, mwandishi anaweza kuanza kuandika.
  • Mchakato wa kuandika huwa mrefu, na mwandishi anaweza kujikuta anafuta mara nyingi kile alichokiandika.
  • Hii inasaidia kuwa na zao bora la fasihi.

Utungaji wa Hadithi Fupi

Hadithi fupi ni masimulizi ya kubuni yaliyoandikwa kinathari. Inaweza kuwa na wahusika wachache, matukio machache, na mandhari finyu. Kuna aina mbili kuu za hadithi kulingana na kigezo cha urefu au maudhui:

  • Hadithi Fupi: Inayo wahusika wachache, matukio machache, na mandhari finyu.
  • Riwaya: Ina wahusika wengi, matukio mengi, na mandhari mapana.

Mikondo ya Uandishi wa Hadithi

Mkondo wa hadithi ni mwelekeo ambao mwandishi anaufuata katika utunzi wa kazi yake. Baadhi ya mikondo ni:

  1. Mkondo wa Kiwasifu: Huhusisha hadithi zinazohusu maisha ya watu.
  2. Mkondo wa Kitawasifu: Hadithi zinazohusu maisha ya mwandishi mwenyewe.
  3. Mkondo wa Kihistoria: Hadithi zinazohusu matukio ya kweli ya kihistoria.
  4. Mkondo wa Kipelelezi: Hadithi zinazohusu upelelezi wa uhalifu.
  5. Mkondo wa Kimapenzi: Hadithi zinazozungumzia masuala ya mapenzi.

Utungaji wa Tamthiliya

Dhima ya Tamthiliya

Tamthiliya ni kazi ya fasihi iliyoandikwa kwa lengo la kuonyeshwa jukwaani, ambapo wahusika huzungumza na kutenda vitendo mbalimbali. Tamthiliya huigiza maisha ya kila siku na huwa na maelezo ya jukwaani yanayoonesha nini kifanywe na nani na kwa namna gani.

Aina za Tamthiliya

  1. Tanzia: Mhusika mkuu anapata anguko kubwa au kifo kinachosababisha huzuni.
  2. Ramsani: Hufundisha kwa njia ya kuchekesha ili kuleta ujumbe mzito.
  3. Vichekesho/Futuhini: Hufanya hadhira kucheka kwa kutumia mbinu za kudhihaki na kukejeli.

Utungaji wa Tamthiliya

Katika utunzi wa tamthiliya, mambo kadhaa yanapaswa kuzingatiwa:

  1. Chagua jambo unalotaka kuandikia.
  2. Panga msuko wa visa na matukio.
  3. Buni wahusika wako kulingana na kile unachotaka kuandika.
  4. Chagua mandhari yanayofaa kulingana na visa vyako.
  5. Tumia mtindo wa majibizano kati ya wahusika.
  6. Gawa tamthiliya katika maonyesho.
  7. Weka maelekezo ya jukwaa, ambayo huelezea kile kinachotendeka kwa wakati huo. Maelezo ya jukwaa huwa katika maandishi ya italiki.

Leave a Comment


Share this Doc

Utungaji Wa Kazi Za Fasihi Andishi

Or copy link

CONTENTS

Translation And Interpretation | English Form 5 & 6

Translation is a process by which ideas that are written in one language ar...

Writing Skills | English Form 5 & 6

Are the abilities that allow you to write effectively and concisely. A competent...

Reading Skills | English Form 5 & 6

Reading is the process of going through written information or piece of wor...

Speaking Skills | English Form 5 & 6

What is Speaking? SPEAKING SKILLS: Speaking is simply the act of talking wh...

Listening Skills | English Form 5 & 6

Listening is ability to accurately receive and interpret messages in the communi...

Word Formation | English Form 5 & 6

This is the field or branch of morphology which studies different principles or ...

Introduction To Language | English Form 5 & 6

Language is a symbol system based on pure or arbitrary  conventions…...

Topic

Form Five and Form Six

Ecology

Ecology is the study of the interactions between living things, such as humans, ...

Evolution

EVOLUTION Evolution is  a change in the genetic composition of a population...

Genetics

Genetics is the study of heredity and variationHeredity- is the passage of chara...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel