Topic Mjengo Wa Tungo Estimated reading: 8 minutes 84 views Maana ya TungoTungoMaana ya TungoTungo ni kipashio cha kisarufi kilichoundwa kwa kuunganisha pamoja vipashio vidogovidogo vilivyo chini yake. Kwa lugha rahisi, tungo ni neno au kikundi cha maneno ambacho hudokeza taarifa fulani, ambayo inaweza kuwa kamili au isiyo kamili.Kwa maana hii, tungo hujengwa na vipashio vidogovidogo kama vile mofimu kuunda neno, neno kuunda kirai, kirai kuunda kishazi na kishazi kuunda sentensi. Kama tulivyokwisha kuona hapo juu, tungo huanzia neno; rejea aina za tungo.Aina za TungoTungo NenoTungo neno ni tungo ambayo huundwa na vipashio vidogo zaidi ya neno ambayo ni mofimu au fonimu. Mfano: anacheza, kakimbia.Tungo KiraiKirai ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi lakini ambacho hakina muundo wa kiima-kiarifu. Mfano: mtoto mzuri, kiyama chake, bondeni.Tungo KishaziKishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho kinaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe.Kirai na Uainishaji wakeMaana ya Kirai na Uainishaji wakeDhana ya kirai itaeleweka vizuri kwa kuzingatia sifa zake zifuatazo:Kirai huwa ni kipashio cha kimuundo kisichokamilika; yaani ni kipashio kisichokuwa na muundo wa kiima – kiarifu kama zilivyo sentensi ambazo zinahusisha mtendaji wa tendo na tendo linalotendwa.Kirai huainishwa kimuundo kulingana na neno kuu la kirai husika.Kirai ni tungo, yaani ni aina moja wapo ya tungo, aina nyingine za tungo ni neno, kishazi, na sentensi.Kirai hudokeza maana, lakini maana hiyo si kamili.Maneno katika kirai lazima yapangwe kimantiki kwa mpangilio unaokubalika katika sarufi ya lugha husika.Japo virai huainishwa kimuundo, huweza kutumika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi. Kirai huweza kutokea upande wowote, wa kiima au kiarifu katika sentensi. Kirai ni kikubwa kuliko neno.Kama tulivyobainisha hapo juu, aina ya virai hukitwa katika aina za maneno ambazo ndizo chimbuko la mahusiano maalumu ndani ya vipashio hivyo.Aina za ViraiKirai Nomino (KN): Ni kirai ambapo neno lake kuu ni nomino. Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa kwenye nomino au mahusiano ya nomino na neno au mafungu ya maneno.Kirai Kitenzi (KT): Kirai-kitenzi ni kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi au katika mahusiano ya Kitenzi na neno au mafungu mengine ya maneno. Hii ina maana kuwa neno kuu katika aina hii ya virai huwa ni kitenzi.Kirai Kivumishi (KV): Kirai-kivumishi ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika kivumishi. Kwa kawaida muundo huu huwa ni wa kivumishi na neno au fungu la maneno linaloandamana nacho.Kirai Kielezi (KE): Tofauti na aina nyingine ya virai, miundo ya virai vielezi haielekei kukitwa kwenye mahusiano ya lazima baina ya neno kuu (yaani kielezi) na neno au fungu la maneno linaloandamana nalo. Badala yake, miundo inayohusika hapa ni ya maneno ambayo hufanya kazi pamoja katika lugha kama misemo, neno au maneno yanayofuata neno lililotangulia yakifafanua zaidi neno hilo.Virai Viunganishi (KV): Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina ya kwa na katika, au kwenye na fungu la maneno linaloandamana nacho. Kwa maneno mengine, kirai hicho ni kile ambacho neno kuu ni kiunganishi.Tungo KishaziMaana ya Kishazi na Uainishaji wakeKishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho kinaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe.Sifa za KishaziKishazi hupatikana ndani ya sentensi.Lazima kishazi kiwe na kitenzi, sehemu yoyote ya sentensi isiyo na kitenzi haiwezi kuwa kishazi.Kishazi huru hutawaliwa na kishazi kikuu na kishazi tegemezi hutawaliwa na kishazi tegemezi.Baadhi ya vishazi huweza kujitegemea kama sentensi hata vikiondoshwa katika muktadha wa sentensi kuu. Kishazi kinachoweza kujisimamia kama sentensi huitwa kishazi huru kikiwa ndani ya sentensi kuu na huitwa “sentensi sahili” kikiwa sentensi inayojitegemea.Baadhi ya vishazi haviwezi kujitegemea kama sentensi ikiwa vitaondoshwa katika muktadha wa sentensi kuu.Vishazi vingi, hata vishazi huru, huwa na kiima dhahiri.Kishazi kwa kawaida, hasa kishazi huru, huwa na kitenzi kimoja kikuu.Kitenzi hicho huweza kuandamana na kitenzi kisaidizi. Pia, kitenzi katika kishazi huweza kuwa kitenzi kishirikishi.Kishazi hutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi.Tofauti ya kishazi na sentensi ni kwamba kishazi hupatikana ndani ya sentensi lakini sentensi hujisimamia kimuundo na kimaana. Kishazi huwa na kiarifu kimoja na kiima kimoja, lakini sentensi huweza kuwa na kiima kimoja.Aina za VishaziVishazi Huru: Kishazi huru ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kikuu, ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe kamili usiohitaji maelezo zaidi ya kukamilisha maana. Ni kishazi ambacho hata kikiondolewa katika muktadha wa sentensi ambamo vimejikita, huweza kujitegemea kama sentensi.Vishazi Tegemezi: Kishazi tegemezi ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kisaidizi, ambacho muundo wake hukifanya kutegemea kitenzi cha kishazi huru ili kuweza kutoa ujumbe uliokusudiwa. Kishazi tegemezi peke yake hakitoi ujumbe unaojitosheleza.Sifa za Kishazi TegemeziKishazi tegemezi hutoa maana kamili kinapoandamana na kishazi huru.Kishazi tegemezi kinaweza kufutwa katika sentensi bila kuharibu maana ya sentensi nzima.Kishazi tegemezi hutambulishwa na viambishi vya utegemezi vinavyoambatanishwa kwenye kitenzi.Kishazi tegemezi vile vile kinaweza kutambuliwa kwa kuwepo vishazi kama vile ingawa, kwamba, ili, kwa sababu, mzizi wa amba, mofimu ya masharti n.k.Aina za Vishazi TegemeziVishazi tegemezi vivumishiVishazi tegemezi vinavyotokea pamoja na nomino inayovumishwaVishazi tegemezi visivyoambatana na nomino inayovumishwaVishazi tegemezi vieleziVishazi tegemezi vya mahaliVishazi tegemezi vya wakatiVishazi tegemezi vya namna au jinsiVishazi tegemezi vya mashartiVishazi tegemezi vya hali, hitilafu au kasoro iliyoko katika tendoVishazi tegemezi vya sababu/chanzoDhima na Hadhi ya VishaziKishazi chaweza kuwa huru kikajitegemea chenyewe kwa kuwa na maana kamili inayojitosheleza. Lakini kuna vishazi ambavyo havijitoshelezi vyenyewe, bali hutegemea vishazi vingine. Kishazi huru kina hadhi ya sentensi (sahili). Kishazi tegemezi hakina hadhi hii; vishazi tegemezi ambavyo hutegemea vishazi vingine hushuka daraja na kuchukua dhima ya kikundi. Baadhi ya vishazi tegemezi huchukua dhima (hufanya kazi) ya kivumishi katika tungo ambayo kwa kawaida ni dhima ya kikundi au neno. Vishazi hivi huvumisha nomino katika tungo hiyo.Ufafanuzi wa Aina za TungoSentensiMaana ya SentensiSentensi ni kifungu cha maneno kuanzia neno moja na kuendelea chenye muundo wa kiima na kiarifu na kinacholeta maana kamili.Sifa za SentensiMpangilio wa Maneno: Sentensi lazima iwe na mpangilio wa maneno unaokubalika na wazungumzaji wa lugha husika.Ukamilifu: Sentensi lazima ikamilike kimaana, kimuundo, na kisarufi.Muundo: Sentensi huwa na muundo wa kiima na kiarifu, ikiwa na kirai nomino na kirai kitenzi.Kitenzi Kikuu: Sentensi inaweza kuwa na kitenzi kikuu kimoja au zaidi.Kishazi: Sentensi inaweza kuundwa na kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi.Hali Mbalimbali: Sentensi huonyesha hali mbalimbali kama vile amri, ombi, mshangao, na swali.Muundo wa SentensiKimapokeo/Kikazi/KidhimaKiima: Sehemu inayojaza nafasi ya mtenda au mtendwa wa jambo.Kiarifu: Sehemu inayojaza maneno yanayoarifu tendo lililofanywa, linapofanywa, au litakapofanywa.Vipashio vya KiimaNomino peke yakeNomino na kiunganishiNomino na kivumishiKivumishi na nominoKiwakilishi peke yakeKiwakilishi na kivumishiNomino na kishazi tegemezi vumishiKitenzi jinaNomino na vivumishi zaidi ya kimojaKitenzi jina na nominoUmbo kapaTaarifa zitolewazo na Kiarifu kuhusu KiimaKiima ni naniKiima kina niniKiima hufanya niniKiima kinahisi niniSifa za KiarifuHuwa na kitenzi na pengine huambatana na maneno mengine.Kwa kawaida huja baada ya kiima.Vipashio vya KiarifuKitenzi kikuu peke yakeKitenzi kisaidizi na kitenzi kikuuKitenzi kishirikishi na kijalizoAina za SentensiSentensi SahiliMaana: Huundwa na kishazi huru kimoja na inaelezea taarifa moja tu.Mfano: Wanafuzi wanafanya mtihani.Miundo ya Sentensi SahiliKitenzi kikuu peke yake. Mfano: Gari limeanguka.Kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi. Mfano: Mgosiyuda alitaka nisipate utajiri.Vira-vitenzi vilivyokitwa katika kitenzi ‘kuwa’. Mfano: John amekuwa akiangalia TV kwa muda mrefu sana.Kitenzi shirikishi. Mfano: Kiswahili ni tunu ya Taifa.Sifa za Sentensi SahiliIna kiima ambacho kimetajwa wazi au kimeachwa kutajwa.Ina kiarifu chenye kitenzi kikuu kimoja, kitenzi kisaidizi, kitenzi kishirikishi, kijalizo na chagizo.Inajitosheleza kimuundo na kimaana.Sentensi ChangamanoMaana: Ina kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi.Mfano: Gari lililopinduka jana jioni halikuharibika hata kidogo.Sentensi AmbatanoMaana: Inajengwa na sentensi mbili au zaidi zilizounganishwa kwa viunganishi kama vile lakini, wala, au, na.Mfano: Mwalimu anafundisha wakati wanafunzi wanapiga kelele.Miundo ya Sentensi AmbatanoSentensi sahili tu. Mfano: Mwalimu anafundisha wakati wanafunzi wanapiga kelele.Sentensi sahili na changamano. Mfano: Walinzi waliposhindwa, polisi waliwasaidia lakini hawakuweza kuwakamata majambazi.Sentensi changamano tu. Mfano: Barabara zilizojengwa na wakoloni zimedumu hadi leo wakati zile zilizojengwa na Wachina hata mwezi hazifikishi.Vishazi visivyounganishwa kwa viunganishi.Uchanganuzi wa SentensiHatua za UchanganuziKutaja aina ya sentensi: sahili, changamano, au ambatano.Kutaja sehemu zake kuu: kiima na kiarifu, au kirai nomino na kirai kitenzi.Kutaja sehemu kuu za kiima na kiarifu au sehemu kuu za kirai nomino na kirai kitenzi.Kutaja sehemu zote za maneno yaliyomo katika sentensi hiyo.Njia za uchanganuzi wa sentensiNjia ya mishale/mistariExample 1Uchanganuzi wa sentensi kwa njia ya mishaleNjia ya visanduku/jedwaliExample 2MfanoS.SKNKTNKHTKNHKNNKVNVKEEMtuMwenyeUlemavuanachezampiramzurisanaNjia ya matawiExample 3Uchaganuzi wa sentensi kwa njia ya matawiMifano mingine ya uchanganuzi wa sentensi ambatano;(Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasaliti)Njia ya jedwaliExample 4Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasalitiS.AS1US2KNKTKNKTNKVTKEWTVEWatuwengiwalimwaminiSanaLakiniYeyealiwasalitiKwa njia ya matawiExample 5Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasalitiKwa njia ya mishaleExample 6Watu wengi walimuamini sana lakini yeye aliwasalitiTagged:Form 3Kiswahili Topic - Previous Ngeli Za Nomino Next - Topic Maendeleo Ya Kiswahili