Topic Kutunga Kazi Za Fasihi Andishi Estimated reading: 4 minutes 81 views Utungaji wa MashairiMambo ya Kuzingatia katika Utungaji wa Mashairi [1] Ushairi ni utungo wa kisanaa ulio na madhumuni ya kutumbuiza au kuelimisha. Tena, ushairi ni tawi mojawapo la fasihi andishi.-https://sw.wikipedia.org/wiki/Ushairi Utungaji au uandishi wa kubuni ni ule unaotokana na hisia ambazo zinamsukuma mtunzi ili atunge kazi yake. Hisia zinaungana na wazo ambapo vitu hivyo vinamsumbua akilini na kumkosesha raha. Mwandishi wa kubuni anataka kuwasilisha wazo lake ili hadhira ifahamu kilichopo moyoni mwake. Mwandishi hukosa usingizi na hivyo hulazimika kuamka na kuandika kile kinachomsukuma akilini mwake.Milango ya FahamuUandishi wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu kinagaubaga. Kuna milango ya fahamu mitano ambayo ni pamoja na:Kuona: Je, mhusika unayemfikiria kichwani mwako unamwonaje? Umbo lake ni la kuvutia au kuchusha? Je, macho yake yakoje – ni ya golori au la? Ni makubwa au madogo? Je, ni mlemavu wa macho?Kunusa: Pua zako zinakufanya usikie harufu gani? Je, ni harufu mbaya au nzuri? Je, ni uvundo au marashi? Je, mhusika wako ananuka kikwapa au uturi? Je, ananuka mdomo?Kuhisi: Je, unapokaa karibu naye unajihisi nini? Je, unapata mhemko wowote au huhisi chochote? Je, akikupapasa mwilini mwako unajisikia nini? Akikugusa bega unajisikia nini?Kuonja: Je, ukiweka kitu hicho mdomoni unaonjaje – ni chungu au tamu? Je, ina pilipili au masala? Je, kuna chumvi au sukari? Je, kitu hicho kina ukakasi au uchachu?Kusikia: Je, sauti unayoisikia ikoje? Inamtoa nyoka pangoni? Inakufanya ukose usingizi? Je, ni sauti nzuri au mbaya? Ni nyororo au nzito? Kama ni sauti ya muziki – je, iko chini au juu (kelele)?Uzoefu wa MwandishiUzoefu ni hali ya kukaa au kujishughulisha na jambo au kitu kwa muda mrefu.Maswali ya Kujitathmini:Mwandishi ana uzoefu gani wa kukabiliana na maisha?Je, ni matatizo gani ambayo umekutana nayo katika maisha yako?Je, ni mafanikio gani umekutana nayo katika maisha yako?Uchunguzi/UtafitiUchunguzi unapaswa ufanywe na mwandishi ili aweze kuandika jambo au tukio bila kuongopa. Uchunguzi unahusisha:Kutambua Tabia za Mhusika au Tukio:Anatembeaje, anakulaje, analalaje, anaishije, anachekaje, analiaje, anazaaje, anahusianaje na wenzake na mazingira yake?Haya ni maswali muhimu katika kumwezesha mtunzi kufanya utafiti wa kina ili ajue kitu anachotaka kukiandika akiandikaje na akiwasilishaje ili aweze kuikamata hadhira yake.Dhana ya ShairiShairi ni kipande cha maandishi kilichopangwa kwa utaratibu katika mistari. Sauti za silabi hufanana zikiwa kati au mwisho mwa mstari. Maandishi hayo yakisomwa huleta ujumbe na hisia fulani ya kimaisha.Mpangilio wa Maneno ya Shairi: Maneno ya shairi huweza kuimbwa na hutoa picha wazi, maana halisi na burudani ya kimuziki. Nyimbo nyingi za makabila zimepangiliwa kishairi ijapokuwa hazikuandikwa.Umbo la Shairi: Mashairi yana umbo ambalo huonekana kwa mpangilio wa sauti na idadi ya maneno katika mistari. Umbo hili hutofautisha shairi na tenzi.Mambo Muhimu Katika ShairiBeti: Kifungu kimoja cha shairi ambacho kina uzani sawa.Vina: Ni mwisho wa mistari ambayo huwa na silabi zenye sauti ileile mwishoni mwa sentensi.Mizani: Ni idadi zilizo sawa za silabi katika kila mstari, ubeti hadi ubeti.Kituo: Mstari wa mwisho wa ubeti. Kuna vituo vya aina tatu:Kituo cha Bahari: Mstari unaotoka mwanzo hadi mwisho bila kubadilika katika kila ubeti.Kituo cha Kimalizio: Mstari wa mwisho maneno yake hubadilika ubeti hadi ubeti.Kituo Nusu Bahari: Mstari wa mwisho ambao maneno yake nusu hubadilika na nusu hubaki kama ulivyo ubeti hadi ubeti.Vipengele vya Fani katika MashairiJina / AnwaniMandhariWahusikaMuundo: Tathnia, tathlitha, tarbia, tathamisa, sabilia n.kMtindo: Pindu, msisitizo, beti kubadilishana vina, kurudiwa kipande kizima cha mstari wa mwisho kikiwa ni chanzo cha ubeti unaofuatia.Vipengele vya Maudhui katika MashairiVipengele vya maudhui ni pamoja na:MigogoroUjumbeFalsafaMsimamoMtazamoDhamira za mwandishiMatumizi ya UshairiKuombolezaKubembelezaKuliwazaKufundishaKuburudishaKukosoa n.k.Hatua za Utungaji wa ShairiBaada ya kuzingatia mambo haya, sasa unaweza kuanza kutunga shairi lako la kwanza.Chagua Wazo Kuu: Wazo hili ni lile linalokusukuma zaidi.Tumia Milango ya Fahamu: Fikiria unavyomuona, kumnusa, kumsikia, kumhisi na kumwonja mhusika au tukio linalohusu shairi lako.Fanya Utafiti: Ikiwa kuna jambo au tukio ambalo unataka kuandika kuhusu, fanya utafiti ili kuhakikisha unaelewa kwa undani.Andika Rasimu ya Kwanza: Andika mawazo yako bila kujali sana ufasaha wa lugha.Fanyia Marekebisho: Soma tena rasimu yako, rekebisha vina, mizani na vituo ili shairi lako liwe na mtiririko mzuri.Kwa kufuata hatua hizi, utaweza kuandika mashairi yanayovutia na kuwasilisha mawazo na hisia zako kwa hadhira kwa njia bora. Footnotes ( 1 ) Tagged:form 4kidato cha nneKiswahili Topic - Previous Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi Next - Topic Uandishi