Comment

Darasa Huru

Darasa Huru

Limitless Potential

From theory to practice—your free resource hub for success.

Faraja ya Usichana

Msichana na Mahusiano

Estimated reading: 14 minutes 98 views

Afya ya Uzazi

Maana ya afya ya Uzazi

Afya ya uzazi ni ipi?

Katika pilika zangu nilipita sehemu kadhaa na kukutana na watu mbalimbali. Miongoni mwa hao watu nilipenda kufahamu wanaelewa nini juu ya afya ya uzazi, nao walinijibu ifuatavyo:

  • Ni afya ya kupanga uzazi wa watoto kwa maana nyingine uzazi wa mpango katika familia.
  • Ni ile inayomhusu mama mjamzito mpaka anapofikia kipindi cha kujifungua mtoto wake.
  • Afya ya wanandoa hasa inayohusu tendo la kujamiiana ili kupata watoto.

Niligundua watu hawa wako gizani lakini mimi pia ilikuwa hivyo hivyo na kilichonipa utata ni neno hili la uzazi

Nini maana ya afya ya uzazi?

  • Ni afya inayohusu maungo ya uzazi yaani via vinavyohusika katika mtiririko wa kupata mtoto kuanzia kujamiiana hadi mimba inapotungwa katika mfuko wa uzazi.
  • Uzazi ni uwezo wa mbegu ya kike kurutubishwa na ya kiume ili kutungwa mimba.
  • Afya ya uzazi inahusu jinsia zote za kiume na za kike kwa sababu wanaume nao wana via vya uzazi
  • Afya ya uzazi inabidi kutiliwa maanani na kulindwa katika mzunguuko wote wa maisha: toka utotoni hadi uzeeni.

Ngono katika umri wangu

NAAMINI kuwa kila uendapo umesikia na kuambiwa juu ya matokeo ya kufanya ngono katika umri mdogo. Naona kama nisirudie, lakini nafikiri ni vyema kama nitakueleza yafuatayo ambayo mimi pia nilielezwa na yakanisaidia:

  • Uamuzi wa kufanya ngono ni wako wala mtu mwingine hana haki ya kukushawishi au kukulazimisha, nasema hivi kwa sababu asilimia 95% hufanya tendo hili si kwa hiari yao.
  • Misingi imara ya dini yako itakupa nguvu na uwezo wa kukabili vishawishi,kwa mimi mkristo,imani yangu ni nguzo yangu
  • Starehe ya muda mfupi inaweza kukuletea majuto ya muda mrefu katika maisha yako yote.
  • Uelewe kuwa wewe ni mtu muhimu sana “spesho”hapa duniani na mwili wako ni kielelezo cha undani wako hivyo basi inakupasa uulinde mwili wako.
  • Ndoto zako hazitofanikiwa bila jitihada, nguvu zako na uwezo wako. Jifunze kujipenda na kujithamini na sio kutimiza matakwa ya mtu mwingine.
  • Hata kama wote walio karibu yako au unaowafahamu wanafanya tendo hili, jivunie kuwa tofauti

Umri sahihi wa kufanya ngono ni upi?

Kuna imani za dini,mila na desturi ama maazimio binafsi yanapelekea watu kufanya ngono wakiwa kwenye ndoa, hiyo ni sahihi na bora. Pia, wengine, labda kutokana na sababu zao nyingi,muhimu na ambazo sio muhimu, wanataka kufanya ngono kabla ya ndoa.

Uamuzi wa kufanya ngono uzingatie yafuatayo:

  • Mipaka yako ya dini na maadili yenu,kuepuka kutumbukia dhambini
  • Ndoto zako na mipango yako inayohitaji kutekelezwa, mara nyingi katika umri wa wanafunzi ni mapema mno
  • Utu wako, heshima yako na kulinda nafsi yako.
  • Uhusiano madhubuti na kijana anayekupenda ambaye pengine mtaoana na haitakufanya ujutie.
  • Jitahidi kusubiri upate mchumba anayefaa. Mbele tutaona mchumba anayefaa ni yupi ili usiruke ruke huku na kule kama kuku asiyekuwa na makazi maalum  Uwe umekuwa kifikra, kimsimamo na mwenye hesabu na mipangilio madhubuti kwa maisha yako.

Unyanyasaji wa kijinsia

Maelezo juu ya Ngono ya kulazimishwa

Ngono ya kulazimisha: ubakaji

Kwanza kabisa hebu tuwekane sawa, unajua wengi kati yetu mimi nikiwa mmojawapo sikuelewa kuwa ngono ya kulazimisha ndiyo ubakaji. Ukweli ni kuwa mtu mzima anaweza kumshawishi msichana mdogo wafanye ngono bila hata kumnasa kibao. Msichana huyo akiwa chini ya miaka 18 basi huyo mtu aliyemfanyia kitendo hicho atahukumiwa kwa mujibu wa sheria ya ubakaji.

Tendo la kubaka

Ni kumlazimisha mtu kufanya nae mapenzi kinyume na ridhaa yake hali inayoweza kuleta majeraha makubwa kimwili na kisaikolojia kwa mtu aliyebakwa kwa muda mrefu sana

Hatua ya kwanza kama umebakwa

  • Ni uamuzi wako kutoa taarifa, kuripoti polisi au usiripoti. Lakini ni vema kuripoti tukio hilo polisi ama kwa mtu yeyote unayemwamini anayeweza kutoa msaada. Iwapo utaamua kutoa ripoti polisi basi nenda kwenye kituo cha karibu na tukio lilipotokea na pia nenda hospitali ya karibu kama umeumia sana na wao watakutibu na baadaye nenda polisi.

Hatua za kuelewa iwapo umeamua kwenda polisi

  • Usijisafishe wala kujifuta kwa sababu utapoteza ushahidi ambao utahitajika mahakamani.
  • Jiandae kwenda mahakamani iwapo polisi watamshika aliyekubaka
  • Daktari atachunguza kwa nia ya kutafuta ushahidi utakaosaidia kesi yako ili mbakaji aweze kuhukumiwa
  • Nilisikitika pale nilipoongea na msichana mmoja ambaye alienda kuripoti kituoni kuwa amebakwa. Polisi wale wakaanza kuongelea kwa sifa umbile lake tena ngoja ninukuu walivyosema “du! Zinga la figa, jamaa uzalendo ulimshinda ha ha ha………! Hii ilinidhihirishia jinsi wanaume walio wengi walivyo na mtazamo wa ubaguzi wa kijinsia.
  • Iwapo umeamua kutotoa ripoti polisi ni lazima utibiwe kama kuna madhara yoyote yaliyotokana na kitendo hicho. Pia kumbuka, unahitaji dawa ya kukinga maambukizo ya UKIMWI ama magonjwa mengine ya ngono.
  • Usikae kimya,itakuumiza, ongea na mama dada, bibi au mtu yeyote unayemwamini ili hilo donge lisikae tena ndani yako.

Sipendi kufikiria hili suala lakini yanatokea …

Mimba itokanayo na kubakwa

Kuzaa mtoto wa mbakaji ni wazo la kwanza litakalokujia kichwani kwako hata hivyo ni mtoto wako pia. Mimba hiyo unaweza kuamua kuzaa lakini ni muhimu baada tu ya kitendo hiki uende hospitali ili pia uweze kufahamu hali kama hii. Ukishafahamu kama huitaki, unaweza kupewa njia ya dharura ya kuzuia mimba

Magonjwa …

  • Muhimu ni kuanza dawa za kutibu magonjwa ya ngono mapema iwezekanavyo na ndio maana nasisitiza umuhimu wa kwenda hospitali kitendo hiki kitokeapo. Pigo kubwa ni kama amekuambukiza virusi vya UKIMWI ni ngumu hata kwa kufikiria tu lakini katika maisha kuna kuendelea mbele. Pata ushauri nasaha kuhusu virusi vya UKIMWI na kutokukata tamaa.

Vidonge vya dharua vya kuzuia mimba vipo katika vituo vya afya hapa nchini. Iwapo utabakwa, ili uweze kuzuia mimba, nenda katika kituo chochote cha afya na uripoti suala hilo. Inatakiwa umuone mtoa huduma ya uzazi wa mpango ambaye atakupa ushauri pamoja na huduma. Mimba inaweza kuepushwa kwa usalama na kwa ufanisi hadi siku tatu au saa 72 baada ya kubakwa. Jinsi utakavyowahi kumeza vidonge vya dharura vya kuzuia mimba, kuna uwezekano mkubwa wa kuepuka mimba

Mtoto nizae Mtoto ?

Maelezo juu ya Mtoto Kuzaa Mtoto

Nitakuwa mgeni wa nani mie…!

Katika akiba yangu nilikuwa na vijihela kidogo bila kusita nikaenda hospitali moja niliyoelekezwa na shoga yangu kwa nia ya kuyasitisha maisha ya huyo kiumbe aliyeko tumboni. Nilikuwa nimetajiwa mpaka dokta, nilimuulizia na nikaelekezwa ofisini kwake, Haukupita muda tukajikuta tukipangiana bei kama vile ukiwa unanunua nguo halafu unaomba upunguziwe bei

Baada ya makubaliano aliniuliza kama nimekula nikamwambia hapana hata hivyo nilipenda kujua maana ya hilo swali akaniambia atanichoma sindano ya usingizi inayoleta kichefuchefu hivyo basi haitakiwi niwe nimekula kwa sababu matapishi yanaweza yakapita njia ya hewa na kusababisha kifo.

Nikavaa manguo ili nipelekwe chumba cha operesheni. Licha ya kupewa dawa ya usingizi huko kwenye chumba cha operesheni nikaanza kusikia wanachokifanya kwa mwanangu.

Sitanii wala sidanganyi, wanakwangua kama nazi inavyokunwa kwenye mbuzi. Nilihisi kizunguzungu, nikalala. Eh! Nimesahau kuwaambia hizo sindano zinachomwa pale palenukeni halafu wanaingiza kama bomba ili wapanue njia. Usikie tu, inauma, Baada ya pale, walikuwa wameniwekea gozi kama pamba ndani kwa ajili ya kunyonya damu. Ilipofika jioni nikatoa gozi lakini damu ikaendelea kutoka kwa fujo ikiwa mabonge mabonge na tumbo lilianza kuuma nashindwa hata kueleza. Damu iliendelea kutoka kama bomba lililofunguliwa. Niliumwa nikahisi nakufa. Nilienda hospitali nyingine na kufikia hatua hii hata nyumbani walijua. Niliingizwa tena chumba cha operasheni nikasafishwa upya, maumivu yalipungua taratibu na tumbo likaacha kuuma. Sijajua kama nina uwezo wa kubeba mimba tena kwa sababu yaliyonikuta hata rafiki yangu wa kiume aliniacha.Yaliyonifika nisingependa yamfike msichana mwenzangu, jamani!

Njia za Kuzuia Mimba

Maelezo juu ya Njia mbali mbali za Kuzuia Mimba

Zipo katika makundi haya mawili

  • Njia za kisasa
  • Njia za asili

NJIA ZA ASILI

1.Kutokufanya ngono kabisa

Hii ni njia madhubuti na yenye uhakika kwa asilimia 100.

2. Kufanya ngono siku salama za mwezi:

  • Msichana anachunguza mabadiliko ya ute wa ukeni kila siku kwa kutumia vidole vyake, yeye na mwenzi wake wanaweza kuzuia mimba kwa kuepuka kujamiiana katika siku za kupevuka yai. Njia hii haina uhakika wa moja kwa moja na wakati mwingine ni vigumu kufuatilia ratiba ya kupevuka kwa yai hasa inapotokea mabadiliko ya ghafla yasiyotarajiwa.

NJIA ZA KISASA

1. Njia za vizuizi

  • Kondom ya kiume,Huu ni mpira laini ambao huvishwa kwenye uume uliosimama kabla ya kujamiiana. Mpira huu huzuia shahawa kuingia ukeni ili kusababisha mimba kutunga. Kondom mpya itumike kwa kila mshindo mmoja na kutupwa kwa usalama.
  • Kondom ya kike,Huu ni mpira laini ambao unaingizwa ukeni na kuushikisha kwenye mlango wa uke. Mpira mpya hutumika kwa kila tendo la kujamiiana kisha kutupwa kwa usalama

2. Dawa zenye vichocheo

  • Vidonge vya uzazi wa mpango,Vidonge hivi vina dawa maalum inayoweza kuzuia mimba.Vina maelekezo yake kwenye pakiti na ni njia ya muda, ni salama na ya kuaminika. Hivi ni vidonge ambavyo humezwa na mwanamke kila siku ili kuzuia mimba. Hupatikana katika pakiti ya vidonge 28 na 35. Vidonge hivi pia husaidia kurekebisha matatizo ya hedhi.
  • Sindano,Hii ni njia ya uzazi wa mpango inatolewa kwa kuchoma sindano kwenye msuli wa bega au takoni. Utumiaji wa njia ya sindano huzuia mimba kwa kipindi cha miezi mitatu
  • Vipandikizi,Hii ni dawa ya kuzuia mimba ambayo imo ndani ya mrija wa plastiki, wengine huviita vijiti. Mwanamke huwekewa vipandikizi (na mtaalam) chini ya ngozi, kwenye sehemu ya ndani ya mkono. Vipo vipandikizi vya aina mbili: vyenye vijiti sita na vyenye kijiti kimoja

3. Njia za muda mrefu na njia za kudumu

  • Kitanzi (copper T), Hiki ni kiplastiki kidogo kilichozungushiwa na shaba kwa sehemu chache ambacho kinawekwa na mtalamu kwenye mji wa mimba (mfuko wa kizazi) ili kuzuia mimba isitunge. Kitanzi kina uwezo wa kuzuia mimba kwa kipindi cha miaka 8 hadi 10. Kitanzi kinaweza kutolewa wakati wowote mwanamke anapohitaji kupata mimba.
  • Kufunga kizazi kwa mwanamke, Hii ni njia nyepesi ya operesheni ndogo ambayo hufanyiwa mwanamke aliyeridhika na idadi ya watoto aliowapata. Kwa kawaida operesheni hii hufanyika kwa muda usiozidi dakika ishirini . Baada ya saa 2 hadi 6 kupita, mteja anaweza kwenda nyumbani. Kufunga kizazi kwa mwanamke hakuathiri hamu yake ya kujamiiana, wala mzunguuko wa hedhi.
  • Kufunga kizazi kwa mwanaume, Hii ni njia nyepesi ya operesheni ndogo ambayo hufanyiwa kwa mwanaume aliyeridhika na idadi ya watoto aliowapata. Kwa kawaida operesheni hii hufanyika kwa muda usiozidi dakika kumi na tano. Baada ya saa 2 hadi 4 kupita, mteja anaweza kwenda nyumbani. Kufunga kizazi kwa mwanaume hakuathiri hamu yake ya kujamiiana, wala nguvu za kiume.

MAMBO YA KUKUMBUKA

  • Uzazi wa mpango hauingilii haki ya mtu binafsi au wenzi katika kuamua idadi na wakati wa kupata watoto
  • Unahitaji kuwa na taarifa kamili na sahihi ili uweze kuchagua njia ya uzazi wa mpango: Mtoa huduma atakusaidia kufanya maamuzi sahihi.
  • Kondom ndiyo njia pekee inayokinga mimba, magonjwa ya ngono na UKIMWI
  • Kondom hupatikana madukani, lakini pia zinapatikana bila ya malipo kwenye vituo vya huduma za afya.
  • Maelezo juu ya dondoo mbali mbali na mambo muhimu ya kukumbuka

DONDOO ZA UZAZI WA MPANGO, VVU/UKIMWI

  • Watu walioambukizwa VVU wanaweza kutumia njia za uzazi wa mpango
  • Uzazi wa mpango huwapunguzia adha za ujauzito wanawake walioambukizwa VVU
  • Vijana wanapoahirisha kuanza ngono huwapunguzia uwezekano wa kuambukizwa magonjwa ya ngono/VVU na kuepuka mimba katika umri mdogo. Hivyo wanaweza kufikia malengo yao ya kimaisha

UKWELI HUTUWEKA HURU

Ni dhahiri kwamba kuna njia mbali mbali za kuzuia mamba lakini tuelewe tu ya kwamba mimba iliyokwishatunga,imeshatunga.Iwe dakika moja baadae,saa moja baadae hata siku moja baadae,maisha ya binadamu huyo tayari yameshaanza.Kwa maana nyingine,huzuii mimba bali unaua kiumbe cha Mungu. Nimesema haya,lakini mwishoni wa siku uamuzi unabaki kuwa wa kwako na ndio maana nimejitahidi kuweka bayana hizo njia zote.

TOFAUTI YA NGONO NA MAPENZI

Ngono ni tendo la kujamiiana baina ya mwanaume na mwanamke kwa nia ya kuridhishana kimwili.

Mapenzi ni hisia kali za mvuto baina ya mtu na mtu. Upendo wa dhati ambapo hutaki kumwona mpenzi wako anaumia, na huu ni upendo unaojali na kuheshimu

  • Tuelewe ngono sio lazima iwe na mapenzi, tunaweza kufanya ngono na watu bila kuwa na mapenzi nao.
  • Ngono ni sehemu ndogo tu ya uhusiano wa kimapenzi na muda mwingi katika mapenzi hutumika kujenga mazoea.
  • Wasichana tuna hulka ya kuchanganya ngono tukidhani ni mapenzi, wavulana wanaelewa ngono ni ngono na mapenzi ni mapenzi matokeo yake tunaumia.

Shoga usifuate mkumbo wa kufanya ngono kwa kujionyesha ya kwamba wewe unafuata “fashion”. Heshimu mwili wako, usikubali kufanya ngono holela. Mwanaume anayetaka kukuoa ataheshimu msimamo wako wa kutotaka kufanya ngono kabla ya wakati muafaka

Unawezaje kujikinga na UKIMWI?

Njia kuu ambazo zinaweza kukusaidia usipate UKIMWI

  • Subiri; usifanye ngono kabisa mpaka wakati muafaka utakapofika: kuolewa au kuwa na mwenzi wa kudumu (Kwa lugha ya kiingereza: Abstinence”A”)
  • Kuwa na mwenzi mmoja mwaminifu ambaye hajaambukizwa Virusi Vya UKIMWI (Kwa lugha ya kiingereza: Be faithful ”B”)
  • Tumia Kondom kila mara na kwa usahihi: Mshauri mwenzi wako kutumia Kondom ya kiume au tumia mwenyewe kondom ya kike (Use Condom ”C”)

Nimechagua “A”

Muda unavyozidi kwenda mimi na mpenzi wangu tunazidi kufurahi pamoja na mpango wa kuondoka unazidi kupotea. Giza linazidi kuingia, kwenye redio unasikika muziki laini unaobembeleza. Nahisi niko karibu sana na mpenzi wangu. Kila kitu ni sawa, hisia zangu kwa kweli ni kali. Nahisi mpenzi wangu yuko tayari kufanya mapenzi na kwa namna moja mimi pia niko tayari.

Nifanyeje?

  • Wengi wetu tumepitia hali hii na wewe pia, mwenzangu, lazima katika kukua upitie hali hii inayokufanya ukabiliwe na wakati mgumu wa kufanya uamuzi. Mara nyingi unajikuta katikati ya mahaba mazito bila kufahamu nini hasa unataka,ukifikiria kama ufanye au usifanye.

La kufanya :

  • Ni vizuri kuongea mkiwa hampo kwenye mahaba mazito tayari kuhusu uamuzi wako wa kutofanya ngono. Chagua wakati ambao mmetulia na mkiongea mtaelewana na upange kabisa utakachokiongea kabla mazungumzo hayajaanza
  • Kama umeamua kutofanya ngono basi usiwe kama kinyonga unabadilika badilika. Maneno yako na matendo yako yaendane. Wote wawili mnapaswa mkubaliane mipaka yenu. Shoga tawala hisia, usiruhusu hisia ikutawale!

Ni vigumu iwapo:

  • Mtakaa peke yenu chumbani na mpenzi wako.
  • Mtakutana sehemu za giza au vichochoroni mkiwa wawili na mna uhakika hakuna anayewaona.
  • Mnakunywa pombe mpaka mnalewa kiasi unashindwa kufanya mamuzi sahihi..
  • Mnaangalia mikanda ya video ya ngono, picha, karata au magazeti ya ngono pamoja au peke yako.
  • Ukikaa na rafiki zako mazungumzo ni kufanya mapenzi, ukikaa na mpenzi wako pia mazungumzo ni hayo hayo. Inakuhamasisha zaidi kufanya ngono.

Ni rahisi iwapo

  • Mtatafuta hobi ambayo wote mnapendelea iwe michezo, masomo au sanaa.
  • Kujichanganya na rafiki zenu au watu wengine na sio kukaa peke yenu kila mara kama vile mko kwenye fungate(honeymoon)
  • Kuepuka kukaa chumbani au vichochoroni peke yenu ili msijihamasishe kufanya ngono..
  • Mimi naamini msichana ndiye mtu wa kwanza kufanya maamuzi juu ya mwili wake, juu ya mipango na ndoto zake. Maamuzi ambayo mwishoni yanalenga kumjenga na sio kumdidimiza. Fanya uamuzi ambao hautajutia siku zijazo, mwezi mmoja au mwaka mmoja baadaye

Kwa nini usubiri?

  • Nilivyokuwa shule nilielezwa kuwa tendo la ndoa ni kwa wanandoa na ndio maana limeitwa tendo la ndoa. Hata wakati nakua, nilisisitizwa jambo hilo, hasa kwa sababu za kidini na imani zetu na hii ndiyo sababu yenye nguvu zaidi. Pale sababu hii inapovunjwa tunajihisi kujisaliti wenyewe na Mungu wetu,hata kuchanganyikiwa kwa kuhisi umepoteza muelekeo.
  • Maazimio binafsi yasiyohusishwa na dini wala mila hufanya watu wengine kusubiri,unaweza kuwa mmoja kati ya wa watu hawa.
  • Sababu ya iliyo wazi kwa wengi kuliko zote ni ile ya kuzuia mimba na magonjwa ya ngono hasa UKIMWI.
  • Wasichana tuna tabia moja ya kihisia tena yenye kutuumiza. Tuingiapo katika hali ya mapenzi na mtu inakuwa sio tu kimwili bali tunajitoa zaidi kihisia, kama kuna asilimia basi kimwili ni 40% tu ama chini ya hapo na asilimia nyingi huenda kwenye hisia. Tunatekwa haswa. Kwa hiyo ni muhimu kujilinda, kwani furaha au huzuni inapotawala kutokana na mapenzi, vitu vingine vyote ikiwemo shule, familia n.k vinatoweka akilini.

Tuwe marafiki

  • Usidanganyike rafiki yangu, uhusiano mzuri ni ule uliojengwa juu ya msingi imara. Msingi huo ni urafiki. Mapenzi ni kuzoeana, kuelewana na kuheshimiana. Ukichemka mwanzoni maana yake umechemsha moja kwa moja.
  • Kuharakisha mapenzi badala ya kujenga urafiki inaweza kuumiza uhusiano wenu na hasa hisia zako.

Shikilia uamuzi wako

  • Tatizo linakuja hapa, umeshaamua hutaki kufanya mapenzi kwa sasa. Mpenzi wako unampenda ndio umefika, utawezaje kushikilia uamuzi wako bila kuumiza hisia zake.
  • Mwisho wa siku,haya ni maisha yako,mkimbilie Mungu wako mwenye upendo unaodumu, naye atakuongoza njia ya kupita.Unaweza kuwa bora,unaweza kuwa jasiri,unaweza kuwa chochote unachotaka kuwa iwapo utaamini.

Leave a Comment

Share this Doc

Msichana na Mahusiano

Or copy link

CONTENTS

Agricultural Development

What is Agriculture? Agriculture refers to a fundamental human activity, which i...

Population and Development

POPULATION STUDIES Is the general activities carried out for the purpose of acqu...

Study of Soil

CONCEPT OF SOIL AND SOIL PROFILE Soil appears very complex and thus differe...

Water Masses

GROUND WATER WATER CYCLE Rain falls on the earth surface in filtrates (soaks int...

Topic

The Dynamic-Earth And Consequence

THEORIES THEORY OF ISOSTASY Denudation has been going on the continents where to...

Position Behaviours And Structure Of The Earth

GLOBE Is the model of the earth Earth Is ball of rock partly covered by wat...

Photograph interpretation

Photograph are the true image pictures showing truly appearance of the earth’s...

Maps and map interpretation

What is a map? Map is a scaled conventional representation of the whole or any o...

Simple survey and mapping

INTRODUCTION TO SURVEYING Surveying is an art or a science of measuring and reco...

Field research techniques

Definitions of Research – Research is the systematic investigation into a...

Application of statistics in geography

STATISTICS Statistics is a branch that deals with every aspect of the data. Stat...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel