Comment

Darasa Huru

Darasa Huru

Limitless Potential

Education at your fingertips, with no price tag attached.

Topic

Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi

Estimated reading: 96 minutes 555 views

Summary: Fasihi andishi ni tawi la fasihi linalotumia sanaa ya maneno kufikisha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya maandishi. Zipo aina nyingi za fasihi andishi, miongoni mwa hizo ni pamoja na hadithi fupi, riwaya, tamthiliya na mashairi.

Hakiki ya Fani Katika Tamthiliya ya “Orodha”

Jina la Kitabu

Kitabu “Orodha” kina jina linaloendana kabisa na yaliyomo. Ndani ya kitabu hiki, orodha ya mambo yanayosaidia kuepusha UKIMWI inatajwa, na inatolewa na mhusika Furaha ambaye aliomba isomwe katika mazishi yake. Mambo yaliyomo kwenye orodha ni pamoja na uwazi, ukweli, uadilifu, matumizi ya kondomu, uelewa, upendo, elimu, uwajibikaji, na msamaha. Mwandishi anaamini kwamba kufuatia mambo haya, maambukizi ya virusi vya UKIMWI yatapungua.

Utangulizi

Tamthiliya ya “Orodha” inahusu ugonjwa wa UKIMWI na madhara yake katika jamii. Mwandishi anafafanua ugonjwa huu waziwazi. Mhusika mkuu, Furaha, anaathiriwa na ugonjwa huu na kufariki dunia. Tamthiliya hii inasawiri maisha ya sasa ya jamii ya Watanzania kwani ugonjwa huu bado ni tishio. Kwa upande wa fani, mwandishi ameunda vyema wahusika wake, na muundo wake una mvuto unaomfanya msomaji kutaka kujua kitakachofuata. Lugha iliyotumika ni ya kisanaa na ya kuvutia.

Muundo

Mwandishi ametumia muundo changamano. Sehemu ya 1 na 2 zinaonesha mazishi ya Furaha, huku sehemu ya 3 hadi 20 zinaelezea maisha yake hadi kifo chake, ambao ni muundo sahili. Sehemu ya 17-20 inaonesha mzozo wa orodha na hatima ya mazishi ya Furaha. Tamthiliya imeandikwa kwa onyesho moja lenye sehemu ndogo ndogo ishirini zinazokamilisha tamthiliya nzima.

Muundo wa Sehemu:

  1. Sehemu ya Kwanza:
  • Vifani vinne vimeganda, wahusika wameganda katika mikao inayotambulisha wasifu wa wahusika.
  • Wagonjwa wakiwa katika mateso na maumivu makali.
  1. Sehemu ya Pili:
  • Siku ya msiba wa Furaha.
  • Mama yake Furaha anatoa orodha aliyoiomba isomwe katika mazishi yake, ambayo inazua mgogoro na hofu kwa watu.
  • Padre James anajaribu kuzuia barua isisomwe.
  1. Sehemu ya Tatu:
  • Maisha ya Furaha nyumbani kwao, baba na mama yake, na wadogo zake.
  • Baba yake anaonyesha kutoridhika na mwenendo wa Furaha.
  1. Sehemu ya Nne:
  • Furaha anatoroka nyumbani usiku wa manane kwenda baa na rafiki yake Mary.
  • Mdogo wake anatishia kumshitaki kwa wazazi, lakini Furaha anamtishia.
  1. Sehemu ya Tano:
  • Furaha na Mary wako baa wakinywa pombe na kucheza na wanaume.
  • Furaha anaanza mahusiano ya mapenzi na Bw. Ecko.
  1. Sehemu ya Sita:
  • Furaha anamwendea Padre James kwa ajili ya maungamo.
  • Padre James anamtaka Furaha aende katika chumba chake cha kujisomea na kisha wanazini.
  1. Sehemu ya Saba:
  • Baba na Mama Furaha wanamkanya Furaha kuhusu tabia yake ya umalaya na ulevi.
  1. Sehemu ya Nane:
  • Furaha anakutana na Kitunda sokoni, ambaye anamshawishi Furaha avute bangi.
  1. Sehemu ya Tisa:
  • Salim anarudi kutoka masomoni Dar es Salaam na kukutana na Furaha.
  1. Sehemu ya Kumi:
    • Salim na Furaha wanakutana na kupanga mipango ya mahusiano yao.
  2. Sehemu ya Kumi na Moja:
    • Wanakijiji wanazungumzia tabia ya umalaya ya Furaha na mahusiano yake na Salim.
  3. Sehemu ya Kumi na Mbili:
    • Mama Furaha anamhoji mwanae juu ya tabia yake.
    • Hali ya Furaha inaanza kudhoofu.
  4. Sehemu ya Kumi na Tatu:
    • Furaha akisali, baba yake anamuonya zaidi na kumshauri aolewe na Salim.
  5. Sehemu ya Kumi na Nne:
    • Furaha anachukuliwa vipimo vya damu na kugundulika ana virusi vya UKIMWI.
  6. Sehemu ya Kumi na Tano:
    • Wanakijiji wanapata habari juu ya kuumwa kwa Furaha.
  7. Sehemu ya Kumi na Sita:
    • Salim anamtembelea Furaha nyumbani na kuambiwa ukweli juu ya kuathirika kwake.
  8. Sehemu ya Kumi na Saba:
    • Bw. Ecko na Juma wanataka kuiba barua yenye orodha kutoka chumba cha maiti ya Furaha.
  9. Sehemu ya Kumi na Nane:
    • Padre James anajaribu kusomewa barua hiyo kabla ya mazishi, lakini mama Furaha anakataa.
  10. Sehemu ya Kumi na Tisa:
    • Asubuhi siku ya mazishi, Ecko, Juma na Salim wanatafuta suluhu ya kuzuia orodha isisomwe.
  11. Sehemu ya Ishirini:
    • Siku ya mazishi, mama Furaha anaisoma barua ya orodha mbele ya wanakijiji wote.

Mtindo

Mtindo uliotumika na mwandishi ni wa dayalojia au majibizano. Pia kwa kiasi kidogo ametumia mtindo wa monolojia na barua. Barua hiyo ilisema hivi:

Kwa Kijiji changu kipendwa,

Nawashukuru kwa kufika na kuyasikiliza maneno yangu ya mwisho. Msiogope kwani nadhani maneno haya yanaweza kuwasaidia. Katika miezi ya mwisho nimelala kitandani nikifa, nikizidi kuugua. Nilipata muda mwingi wa kufikiri, kubadilika, na kukua kama mtu. Katika ukurasa unaofuata kuna orodha ya vitu ambavyo vilisaidia kuyafupisha maisha yangu, orodha ambayo inaonesha ukweli juu ya kifo changu. Mama, tafadhali wasomee watu wote orodha hii:

  • Uepukaji
  • Kondomu
  • Uaminifu
  • Elimu
  • Uelewa
  • Uwazi
  • Uadilifu
  • Uwajibikaji
  • Ukweli
  • Upendo
  • Msamaha

Ukosefu wa mambo haya ndiyo ulioniua. Ufuatiliaji wa mambo haya unaweza kuwaokoa nyote. Chukueni orodha yangu na muipeleke kwenye vijiji vingine, miji mingine na majiji mengine katika nchi yetu hii nzuri. Wanusuruni watu wetu ili waweze kufaidi maisha kikamilifu. Wanusuruni watoto wetu ili wasiwe yatima. Muinusuru Afrika yetu nzuri.

Kwa kijiji changu, kiishi maisha marefu na kiwe na furaha! Msihukumu mapema mno. Kwa mama, baba, na dada zangu, nawapenda. Jaribuni kuwa wenye furaha wakati mnaweza kufanya hivyo.

Wenu awapendae,

Furaha

Matumizi ya Lugha

Lugha iliyotumika ni fasaha na inayoeleweka kwa wasomaji wake. Tamathali za semi kama sitiari, tashibiha, mubaalagha, tafsida, mdokezo, nidaa, takriri, tashtiti, na tanakali za sauti zimetumika kwa ustadi mkubwa.

Matumizi ya Nafsi

Mwandishi ametumia nafsi mbalimbali kama ifuatavyo:

  • Nafsi ya Kwanza Umoja na Wingi:
  • “Nilidhani sitakuona tena…”
  • “Oh huwezi kuamini jinsi tulivyojaribu…”
  • Nafsi ya Pili:
  • “Usifurahi kupita kiasi…”
  • “Usiwe hivyo wewe ni mtoto mzuri.”
  • Nafsi ya Tatu:
  • “Mama Furaha: kabla Furaha hajafa alitaka niahidi…”

Matumizi ya Semi

  • Misemo: “Furaha anavuna mbegu ya kifo aliyopanda.”

WAHUSIKA

FURAHA

  • Ni binti mdogo wa miaka kati ya 13-19.
  • Ni Malaya.
  • Anaathirika kwa ugonjwa wa UKIMWI.
  • Alikuwa na bidii na mwenye kujituma.
  • Ana tamaa.
  • Ni mlevi.
  • Ni mkweli na muwazi.
  • Ni jasiri.

BABA

  • Ni baba yake Furaha.
  • Ni mkali.
  • Ana upendo.

MAMA FURAHA

  • Ni mama yake Furaha.
  • Ni mkweli na muwazi.
  • Ana upendo.
  • Ni jasiri.
  • Ni mchapakazi.
  • Ni mpole.
  • Ana msimamo.
  • Anafaa kuigwa na jamii.

MARY

  • Ni binti mdogo.
  • Ni Malaya.
  • Si rafiki mwema.
  • Anachangia kuharibu maisha ya Furaha.
  • Ni mlevi.
  • Anapenda anasa.
  • Ana tamaa.
  • Hafai kuigwa na jamii.

BW. ECKO

  • Ni mwanaume mtu mzima.
  • Ni Malaya.
  • Si muaminifu katika ndoa yake.
  • Ni mrubuni kwa mabinti wadogo.
  • Ni mlevi.
  • Ni mfanyabiashara.
  • Ni muathirika wa UKIMWI.

JUMA

  • Ni mwanaume mtu mzima.
  • Ni Malaya.
  • Ni laghai kwa mabinti wadogo.
  • Ni mlevi.
  • Anapenda anasa.
  • Ana tamaa.
  • Ni rafiki wa Bw. Ecko.

PADRI JAMES

  • Ni mtumishi wa Mungu katika kanisa katoliki.
  • Si muadilifu.
  • Anaogopa ukweli na uwazi.
  • Ni dhaifu kwa wanawake.
  • Anaweza kuwa ni muathirika wa UKIMWI.

KITUNDA

  • Ni kijana wa mtaani.
  • Anapenda anasa.
  • Ana tamaa.
  • Ni mlaghai kwa wasichana.
  • Ni muhuni.
  • Ni mlevi na mvuta bangi.
  • Ana lugha ya kihuni.

SALIM

  • Ni kijana wa kiume.
  • Ni msomi.
  • Ni mchumba wa Furaha.
  • Anaweza kuwa ni muathirika wa UKIMWI.
  • Si mkweli na muwazi.
  • Si muadilifu.

WANAKIJIJI 1, 2 NA 3

  • Ni wanakijiji katika kijiji cha Furaha.
  • Hawana elimu juu ya UKIMWI.
  • Ni wambea.
  • Wana imani potofu.

DADA MDOGO

  • Ni mdogo wake Furaha.
  • Ana tabia njema.
  • Ni mkweli lakini muoga.
  • Hapendezwi na tabia ya dada yake.

MANDHARI

Mandhari aliyotumia mwandishi ni ya vijiji vya Afrika Mashariki kwa ujumla wake. Mwandishi ametumia mandhari hii makusudi kwani imeendana na yale anayoyazungumza katika kitabu. Suala la ujinga na upotofu wa dhana kuhusu UKIMWI lipo zaidi vijijini. Wanakijiji hawaelewi juu ya UKIMWI. Mambo anayoyaibua mwandishi yanaendana na jamii ya watu wa vijiji hivyo, hivyo mandhari ni sadifu.

Leave a Comment

Share this Doc

Uhakiki Wa Kazi Za Fasihi Andishi

Or copy link

CONTENTS

Agricultural Development

What is Agriculture? Agriculture refers to a fundamental human activity, which i...

Population and Development

POPULATION STUDIES Is the general activities carried out for the purpose of acqu...

Study of Soil

CONCEPT OF SOIL AND SOIL PROFILE Soil appears very complex and thus differe...

Water Masses

GROUND WATER WATER CYCLE Rain falls on the earth surface in filtrates (soaks int...

Topic

The Dynamic-Earth And Consequence

WIND Is air in motion or is the movement of air from the region of high pressure...

Position Behaviours And Structure Of The Earth

GLOBE Is the model of the earth Earth Is ball of rock partly covered by wat...

Photograph interpretation

PHOTOGRAPHS OVERLAPING, PHOTOGRAMMERTRY, MAP MAKING AND DIAGRAMS SKETCHING. 1. P...

Maps and map interpretation

SETTLEMENTS. Settlement is a layout of dwellings in the habitable area where peo...

Simple survey and mapping

INTRODUCTION TO SURVEYING Surveying is an art or a science of measuring and reco...

Field research techniques

Definitions of Research – Research is the systematic investigation into a...

Application of statistics in geography

STATISTICS Statistics is a branch that deals with every aspect of the data. Stat...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel