Topic Ngeli Za Nomino Estimated reading: 3 minutes 66 views Kuzielewa ya Ngeli na Upatanishi wa Kisarufi katika SentensiUpatanishi wa Kisarufi katika SentensiNgeli ni vikundi vya majina ya Kiswahili. Ngeli za nomino ni utaratibu unaotumika kuweka nomino katika matabaka au makundi yanayofanana.Mfano 1Maji yakimwagika hayazolekiMayai yaliyooza yananuka sanaYai lililooza linanuka sanaMaji liliomwagika halizolekiKatika mifano hii, tunaona kwamba sentensi (1), (2), na (3) ziko sahihi, wakati sentensi (4) si sahihi. Hii ni kwa sababu imekiuka upatanisho wa kisarufi. Sentensi ya kwanza ipo katika ngeli ya YA-YA, na sentensi ya pili na ya tatu zipo katika ngeli ya LI-YA. Sentensi ya nne si sahihi kwa sababu nomino “maji” haina wingi, hivyo haiwezi kuingia katika ngeli ya LI-YA. Kwa msingi huu, ngeli za nomino huzingatia sana upatanisho wa kisarufi.Jedwali la Ngeli za Nomino kwa Misingi ya Upatanisho wa KisarufiNGELIUFAFANUZIMIFANOA-WANgeli hii inahusisha majina ya viumbe hai kama vile wanyama, watu, wadudu, ndege n.kSungura mjanja ameumiaSungura wajanja wameumiaMkuu anawasiliLI-YAMajina yenye kiambisha awali li- katika umoja na ya- katika wingi huingia katika ngeli hiiJambia la babu limepoteaMajambia ya babu yamepatikanaKI-VINi ngeli ya majina ya vitu visivyo hai, yanayoanza kwa KI- au CH- (umoja); na VI- au VY- (wingi). Pia ngeli hii hujumuisha majina ya vitu vingine katika hali ya udogo k.v, kijito, kilimaChakula kimekwishaVyakula vimekwishaKijito kimekaukaVijito vimekaukaU-IHuwakilisha majina ya vitu visivyo hai, yaanzayo kwa sauti M- (umoja) na MI- (wingi). Pia majina ya baadhi ya viungo vya mwili huingia humu, kwa mfano mkono, mguu, mkia n.kMlima umeporomokaMilima imeporomokaMkono umevunjikaMikono imevunjikaMto huu una mamba wengiMito hii ina mamba wengiU-ZIHurejelea majina ambayo huanza kwa U- (umoja) na huchukua ZI- kama kiambishi kiwakilishi cha ngeli katika wingi. Majina yenye silabi tatu au zaidi hubadilishwa kwa wingi kwa kutoa sauti /u/ k.v ukuta-kuta. Majina ya silabi mbili huongezewa /ny/ katika wingi. k.v ufa – nyufaUkuta umebomokaKuta zimebomokaWimbo huu unavutiaNyimbo hizi zinavutiaUfa umeonekanaNyufa zimeonekanaI-ZIHutumiwa kwa majina yasiyobadilika kwa umoja wala kwa wingi lakini huchukua viambishi viwakilishi tofauti: I- (umoja) na ZI- (wingi).Nyumba imejengwaNyumba zimejengwaSalam imefikaSalam zimefikaU-YANgeli hii inajumuisha nomino ambazo zina kiambishi awali u- katika umoja na ma- katika wingi.Ukuu umekuponzaMakuu yamekuponzaUnyoya unapepeaManyoya yanapepeaKUMajina yanayotokana na vitenzi yanayoanza na ku- (vitenzi-jina)Kusoma kwako kumekusaidiaKuchelewa kumemponzaPA/MU/KU-Huonesha mahaliAmekaa pale palipo na wadudu wengiAmelala mule mulimojaa siafuAmepita kule mbaliMatumizi ya NgeliBaadhi ya matumizi ya ngeli ni pamoja na haya yafuatayo:Kuweka Majina katika Makundi: Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.Umoja na Wingi: Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi.Upatanishi wa Kisarufi: Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.Uhusiano wa Lugha: Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.Kwa kuzingatia upatanishi wa kisarufi, sentensi zinakuwa na muundo sahihi wa kisarufi ambao hufanya lugha kuwa ya kueleweka zaidi na ya kuvutia.Tagged:Form 3kidato cha tatuKiswahili Next - Topic Mjengo Wa Tungo