Comment

Darasa Huru

Darasa Huru

Limitless Potential

From Kindergarten to University — your education, your way.

Topic

Kuongeza Msamiati Wa Kiswahili

Estimated reading: 3 minutes 87 views

Uundaji wa Maneno

Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili msamiati uongezeke katika lugha, sharti maneno mapya yaundwe.

Njia za Uundaji Maneno

Njia za Uundaji Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo:

  1. Kubadili mpangilio wa herufi
  2. Kuambatanisha maneno
  3. Kutohoa maneno ya lugha nyingine
  4. Uambishaji wa maneno
  5. Kufananisha sauti, umbo, mlio na sura

Kuunda Msamiati kwa Kubadili Mpangilio wa Herufi

Neno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno lingine.

Mfano 1:

  • Neno “lima” lina herufi l, i, m, a. Herufi hizi huweza kujenga maneno kama mali, kumi, imla, mila.
  • Neno “tua” lina herufi t, u, a. Herufi hizi zinaweza kujenga maneno kama tatu, tua, viatu, tatua.

Njia ya Kuambatanisha Maneno

Kuna njia tatu za kuambatanisha maneno:

  1. Njia ya kurudufisha au kukariri neno
  • Mfano: barabara, sawasawa, polepole, katikati, vilevile.
  1. Njia ya uundaji wa msamiati kwa kuunganisha maneno mawili tofauti
  • Nomino na Nomino:
    • Punda + mlia = Pundamilia
    • Bibi + Shamba = Bibishamba
    • Afisa + Elimu = Afisaelimu
    • Mwana + Siasa = Mwanasiasa
    • Bata + maji = Batamaji
  • Kitenzi na Nomino/Jina:
    • Changa + moto = Changamoto
    • Chemsha + bongo = Chemshabongo
    • Piga + mbizi = Pigambizi
    • Zima + moto = Zimamoto
  1. Kuunganisha maneno mawili na kudondosha baadhi ya herufi
  • Mfano 2:
    • Baraza la Kiswahili Tanzania = BAKITA
    • Mzaliwa wa mahali Fulani = MZAWA
    • Chama cha Mapinduzi = CCM
    • Nyamamfu = NYAMAFU

Kutohoa Maneno Kutoka Lugha Nyingine

Kila lugha ina tabia ya kuchukua maneno kutoka lugha nyingine ili kukidhi mahitaji ya msamiati. Maneno yanapotoholewa kutoka lugha nyingine hubadilishwa kimatamshi ili yafuate kanuni za Kiswahili. Maneno haya husanifishwa na asasi za lugha ya Kiswahili kabla ya kutumiwa rasmi.

Mfano 3:

  • Neno la Kiswahili – Lugha ya Mwanzo – Neno Lililotoholewa
  • Shule – Kijerumani – Schule
  • Salama – Kiarabu – Salaam
  • Duka – Kihindi – Dukan
  • Karoti – Kiingereza – Carrot
  • Shati – Kiingereza – Shirt
  • Picha – Kiingereza – Picture
  • Papai – Kihispania – Papaya
  • Meza – Kireno – Mezi
  • Shukrani – Kiarabu – Shukran
  • Ngeli – Kihaya – Engeli
  • Ikulu – Kinyamwezi – Ikulu
  • Ng’atuka – Kizanaki – Ng’atuka
  • Ndafu – Kichaga – Ndafu

Kuunda Maneno kwa Njia ya Uambishaji wa Maneno

Hii ni njia ya kubandika viambishi awali na tamati kwenye kiini cha neno. Ujenzi wa maneno hutokana na mzizi mmoja kuonesha maana tofauti ingawa maana hizo zina husiana.

Mfano:

  • Mzizi: -lim-
  • Lima, analima, walilima, kilimo, limiana, halitalimwa, ukulima.

Kufananisha Sauti, Sura, au Tabia

Mfano 4:

  • Kengele – hutokana na sauti ya kengele inapopigwa.
  • Pikipiki – hutokana na muungurumo wa pikipiki.
  • Ndizi mkono wa tembo – Ndizi inayo fananishwa na mkono wa mnyama tembo.
  • Chubwi – Jiwe au chura atumbukiapo katika kina cha maji.

Mazingira Yanayoelezea Kuhitaji Maneno Mapya

Mabadiliko mengi yanatokea kila siku katika nyanja mbalimbali za kimaisha, kama vile mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa, kisayansi, na kiteknolojia. Katika mazingira kama haya, watu watahitaji kuwasiliana na hivyo lugha itahitaji kuunda maneno mapya ili kuwasilisha dhana mpya zilizoibuka.

Mfano:

  • Maneno kama vile nywila, kisakuzi, udukuzi, puku, talakirishi yameundwa ili kuwasilisha dhana za kiteknolojia kwa Kiswahili.

Undaji wa Maneno katika Miktadha Mbalimbali

Mabadiliko ya kimaendeleo yanafanya lugha ihitaji maneno ya kuyafikisha na kutumiwa na jamii. Ili kukidhi mahitaji hayo, maneno mapya yanazuka. Maneno hayo yanaweza kuwa katika fani mbalimbali kama vile sayansi na teknolojia, siasa, utamaduni, na uchumi kulingana na mkondo wa maendeleo.

Mfano wa Msamiati:

  • Fedha, ushuru, kumpyuta, ukoloni, hospitali, suruali, n.k.

Activity 1: Unda Maneno katika Miktadha Mbalimbali

Tafadhali unda maneno mapya kulingana na mazingira yako. Fikiria maendeleo ya kiteknolojia, kisayansi, kiuchumi, na kisiasa na jinsi unavyoweza kuwasilisha dhana mpya kupitia maneno mapya ya Kiswahili.

Leave a Comment

Share this Doc

Kuongeza Msamiati Wa Kiswahili

Or copy link

CONTENTS

Agricultural Development

What is Agriculture? Agriculture refers to a fundamental human activity, which i...

Population and Development

POPULATION STUDIES Is the general activities carried out for the purpose of acqu...

Study of Soil

CONCEPT OF SOIL AND SOIL PROFILE Soil appears very complex and thus differe...

Water Masses

GROUND WATER WATER CYCLE Rain falls on the earth surface in filtrates (soaks int...

Topic

The Dynamic-Earth And Consequence

THEORIES THEORY OF ISOSTASY Denudation has been going on the continents where to...

Position Behaviours And Structure Of The Earth

GLOBE Is the model of the earth Earth Is ball of rock partly covered by wat...

Photograph interpretation

Photograph are the true image pictures showing truly appearance of the earth’s...

Maps and map interpretation

What is a map? Map is a scaled conventional representation of the whole or any o...

Simple survey and mapping

INTRODUCTION TO SURVEYING Surveying is an art or a science of measuring and reco...

Field research techniques

Definitions of Research – Research is the systematic investigation into a...

Application of statistics in geography

STATISTICS Statistics is a branch that deals with every aspect of the data. Stat...

Chat Icon Close Icon

Subscribe

×
Cancel