Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza rasmi majina ya waombaji kazi waliofanikiwa kupita hatua ya awali ya mchakato wa ajira kwa nafasi 1,596 zilizotangazwa hivi karibuni.
Tangazo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa TRA, Bw. Moshi Jonathan Kabengwe, ambaye alieleza kuwa majina hayo yamewekwa kwenye tovuti ya TRA (www.tra.go.tz) rasmi leo, Machi 22, 2025. Waombaji walioitwa kwenye usaili wanatarajiwa kufika kwenye vituo maalum kwa ajili ya hatua ya pili ya usaili itakayofanyika tarehe 29 na 30 Machi 2025.
TRA, ambayo ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na.11 ya mwaka 1995, ina jukumu la kutathmini, kukusanya, na kuhasibu mapato ya Serikali, huku ikitekeleza mipango ya maendeleo ili kuimarisha utendaji wake. Katika kuendelea kutimiza majukumu hayo, TRA inatekeleza mpango wa sita wa kazi (CP6:2022/23 – 2026/27) wenye lengo la kuwa Taasisi ya Mapato Inayoaminika kwa Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi.
Kwa waombaji ambao majina yao yametangazwa kwenye orodha ya usaili, ni muhimu kufuata maelekezo yafuatayo ili kuhakikisha kuwa mchakato wa usaili unafanyika kwa ufanisi:
Tarehe na Sehemu ya Usaili: Usaili utafanyika tarehe 29 na 30 Machi 2025, katika vituo 9 vilivyotangazwa na TRA. Wasailiwa wanatakiwa kufika kwenye kituo kilichopangwa kwao kwa wakati.
Nyaraka za Usaili: Kila msailiwa atahitaji kufika na barua ya kuitwa kwenye usaili yenye namba ya mtahiniwa iliyopelekwa kwao kupitia anuani ya barua pepe. Namba hii itatumika wakati wa usaili.
Vitambulisho na Vyeti: Wasailiwa wanapaswa kuleta vitambulisho vya utambulisho kama vile Kitambulisho cha Uraia, Kitambulisho cha Mkaazi, au Leseni ya Udereva. Aidha, ni muhimu kufika na vyeti halisi vya kitaaluma, ikiwa ni pamoja na vyeti vya Kidato cha IV na VI, Astashahada, Stashahada, Shahada, na vyeti vingine vinavyohitajika kwa kada husika.
Hati za Matokeo: Wasailiwa ambao watapeleka Testimonials, Provisional Results, Statement of Results, au Transcript bila vyeti halisi hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
Waombaji Waliosoma Nje ya Nchi: Waombaji waliofanya masomo nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika kama TCU, NACTE au NECTA.
Vigezo vya Kitaaluma: Kwa waombaji wa kada zinazohitaji usajili na leseni za kitaaluma, ni lazima kuleta vyeti halisi vya usajili na leseni za kufanyia kazi.
Uhakiki wa vyeti utaanza mapema, saa 12:00 asubuhi kwa wasailiwa wa ratiba ya asubuhi, na saa 6:00 mchana kwa wasailiwa wa ratiba ya mchana. Wasailiwa wanashauriwa kufika kwa wakati na kuhakikisha vyeti vyao vyote viko kamili ili kuepuka usumbufu.
Wasailiwa wanatakiwa kujigharamia kwa chakula, usafiri, na malazi. Pia, wasailiwa wenye mahitaji maalum wanashauriwa kufika mapema ili kuripoti kwa Msimamizi wa Kituo cha Usaili kwa msaada utakaohitajika.
Kuhusu Waombaji Wasioitwa kwa Usaili: Waombaji ambao majina yao hayaonekani kwenye orodha ya walioitwa kwenye usaili wanatakiwa kuelewa kuwa hawakukidhi vigezo vya awali vilivyowekwa na TRA. Hata hivyo, wanashauriwa kuendelea kufuatilia tangazo la nafasi za ajira zijazo na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
Ili kuweza kupakua pdf yenye majina ya walioitwa kwenye usaili TRA, bofya kiungo kilichopo hapa chini
BOFYA HAPA KUPAKUA PDF
Mapendekezo ya Mhariri:
NEW VACANCYLet’s grow together, become part ...
Join Mwanga Hakika Bank: Shape the Future of ...
Careers at the U.S. Embassy in Tanzania: Exciti...
Save my name, email, and website in this browser for the next time I comment.
Δ
Translation is a process by which ideas that are written in one language ar...
Are the abilities that allow you to write effectively and concisely. A competent...
Reading is the process of going through written information or piece of wor...
What is Speaking? SPEAKING SKILLS: Speaking is simply the act of talking wh...
Listening is ability to accurately receive and interpret messages in the communi...
This is the field or branch of morphology which studies different principles or ...
Language is a symbol system based on pure or arbitrary conventions…...
Ecology is the study of the interactions between living things, such as humans, ...
EVOLUTION Evolution is a change in the genetic composition of a population...
Genetics is the study of heredity and variationHeredity- is the passage of chara...