Darasa Huru

Darasa Huru

Limitless Potential

Redefining learning with free, accessible educational materials.


Nafasi za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs February 2025 | Nafasi Mpya za Ajira Ualimu MDAs NA LGAs

Nafasi za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs February 2025

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs), ametangaza nafasi za kazi 2,611 katika fani mbalimbali za ualimu. Tangazo hili la tarehe 10 Februari 2025 ni wito kwa Watanzania wenye sifa stahiki kujiunga na sekta ya elimu nchini. Nafasi hizi zinajumuisha walimu wa masomo ya Biashara, Ushonaji, Uchomeleaji, Useremala, Huduma ya Chakula, Upakaji Rangi, Umeme wa Magari, Muziki, Nishati ya Jua, Uzalishaji wa Chakula, na mengine mengi. Serikali inawakaribisha waombaji wenye weledi na ubunifu ili kuchangia maendeleo ya elimu nchini.

Nafasi za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs February 2025Nafasi za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs February 2025

Orodha ya Nafasi za Kazi ya Ualimu Zilizotangazwa MDAs NA LGAs February 2025

  1. Mwalimu Daraja la III C – Biashara (Business Studies) – Nafasi 2,316
  2. Mwalimu Daraja la III B – Ushonaji (Designing, Sewing and Cloth Technology) – Nafasi 18
  3. Mwalimu Daraja la III B – Uchomeleaji na Utengenezaji wa Vyuma (Welding and Metal Fabrication) – Nafasi 13
  4. Mwalimu Daraja la III B – Useremala (Carpentry and Joinery) – Nafasi 33
  5. Mwalimu Daraja la III B – Huduma ya Chakula, Vinywaji na Mauzo (Food and Beverage, Sales and Services) – Nafasi 28
  6. Mwalimu Daraja la III B – Upakaji Rangi na Uandishi Maandishi (Painting and Sign Writing) – Nafasi 6
  7. Mwalimu Daraja la III B – Umeme wa Magari (Auto Electrical) – Nafasi 3
  8. Mwalimu Daraja la III C – Muziki (Music Performance) – Nafasi 2
  9. Mwalimu Daraja la III C – Nishati ya Jua (Solar Power Installation) – Nafasi 28
  10. Mwalimu Daraja la III B – Uzalishaji wa Chakula (Food Production) – Nafasi 14
  11. Mwalimu Daraja la III B – Refrigeration and Air Conditioning – Nafasi 8
  12. Mwalimu Daraja la III B – Technical Drawing – Nafasi 2
  13. Mwalimu Daraja la III B – Draughting – Nafasi 2
  14. Mwalimu Daraja la III B – Manufacturing Engineering – Nafasi 2
  15. Mwalimu Daraja la III B – Leather Goods and Footwear Production – Nafasi 2
  16. Mwalimu Daraja la III C – Electronics and Communication Engineering – Nafasi 3
  17. Mwalimu Daraja la III B – Surveying and Building Construction – Nafasi 1
  18. Mwalimu Daraja la III B – Fasihi ya Kiingereza (English Literature) – Nafasi 5
  19. Mwalimu Daraja la III C – Utengenezaji wa Nguo (Textile) – Nafasi 1
  20. Mwalimu Daraja la III C – Graphics Designing – Nafasi 17
  21. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II (Office Management Secretary II) – Nafasi 50
  22. Mpishi Daraja la Pili (Cook II) – Nafasi 51
  23. Daktari wa Mifugo Daraja la II (Veterinary Officer II) – Nafasi 1
  24. Msanifu Majengo Daraja la II (Architect II) – Nafasi 5

Sifa za Waombaji Wa Nafasi Mpya za Ajira Ualimu MDAs NA LGAs

  1. Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45.
  2. Wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na kutaja hali yao kwenye mfumo wa maombi.
  3. Waombaji waambatishe vyeti vyao vya taaluma vilivyothibitishwa.
  4. Watumishi wa umma waliopo hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kwa kibali maalum.
  5. Waombaji waambatishe CV yenye maelezo binafsi na anwani za waaminifu tatu.

Majukumu ya Kazi kwa Undani

Walimu watakaopata ajira hizi watakuwa na wigo mpana wa majukumu ya kila siku, kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora na malezi stahiki. Baadhi ya majukumu hayo ni:

  1. Kuandaa mipango ya kazi: Hii inajumuisha kuandaa azimio la kazi la mwaka, maandalizi ya kila somo, nukuu za masomo, na mpango wa kazi wa majukumu mengineyo aliyokabidhiwa na mkuu wa shule.
  2. Ubunifu wa vifaa vya kufundishia: Mwalimu anatakiwa kuwa mbunifu na kutengeneza vifaa vya kufundishia na kujifunzia, na pia kufaraghu vifaa vilivyopo ili kuhakikisha upatikanaji wa zana mbalimbali darasani.
  3. Kufundisha na kutathmini: Mwalimu atahusika na kufundisha masomo kwa wanafunzi, kufanya tathmini mbalimbali ili kupima uelewa wao, na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya kila mwanafunzi.
  4. Usimamizi wa wanafunzi: Katika majukumu yake, mwalimu anatarajiwa kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi shuleni na darasani, na pia kusimamia malezi yao kwa ujumla, katika nyanja za kiakili, kimwili, na kiroho. Mwalimu pia atatoa ushauri nasaha na unasihi kwa wanafunzi pale inapohitajika.
  5. Ushauri wa kitaalamu: Mwalimu atatoa ushauri wa kitaalamu kuhusu maendeleo ya elimu kwa ujumla, kwa kushirikiana na walimu wengine na uongozi wa shule.
  6. Utunzaji wa vifaa vya shule: Mwalimu atahusika na usimamizi na utunzaji wa vifaa na mali za shule, kuhakikisha vinatumika kwa usahihi na kwa malengo yaliyokusudiwa.
  7. Majukumu mengine: Mwalimu atafanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wa shule kulingana na mahitaji ya shule.

Jinsi ya Kutuma Maombi Ya Nafasi za Kazi Ualimu MDAs NA LGAs February 2025

Waombaji wote wanapaswa kutuma maombi kupitia mfumo wa kielektroniki wa ajira kwa anuani: Maombi yasiyozingatia utaratibu huu hayatafanyiwa kazi.

Mwisho wa kutuma maombi: 20 Februari 2025.

Hii ni fursa adhimu kwa wale wote waliohitimu masomo yao ya ualimu kujiunga na sekta ya elimu na kushiriki katika ujenzi wa taifa kupitia utoaji wa elimu bora kwa kizazi cha sasa na kijacho. Jiandae sasa na tumia nafasi hii kuboresha taaluma yako na kuchangia maendeleo ya elimu nchini.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi TRA (Tanzania Revenue Authority)
  2. Mfumo wa Kutuma Maombi ya Ajira TRA (TRA recruitment Portal Login)
  3. Nafasi za Kazi TRA Februari 2025: Ajira Zaidi ya 1000 kwa Fani Mbalimbali
  4. Majina waliochaguliwa kujiunga na Mafunzo Jeshi la Uhamiaji 2025
  5. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Ualimu 2025 (Mikoa Mbalimbali)
  6. Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Uhamiaji 2025
  7. Ajira Portal | Ajira Mpya za Walimu December 2024
  8. Mfumo wa Maombi ya Ajira Uhamiaji Recruitment Portal (Immigration Recruitment Portal)
  9. Nafasi za Kazi Benki Kuu ya Tanzania BOT December 2024



Related Post

Nafasi Ya Kazi :- 6 Active Jobs At VisionFund

VisionFund Tanzania Microfinance Bank Ltd (VFT...

Nafasi Ya Kazi :- 10 Exciting Job Opportuniti

Johari Rotana is an esteemed name in the hospi...

Nafasi Ya Kazi :- Project Coordinator At NIMR

United Republic of TanzaniaMinistry of HealthN...

Leave a Comment

Agricultural Development

What is Agriculture? Agriculture refers to a fundamental human activity, which i...

Population and Development

POPULATION STUDIES Is the general activities carried out for the purpose of acqu...

Study of Soil

CONCEPT OF SOIL AND SOIL PROFILE Soil appears very complex and thus differe...

Water Masses

GROUND WATER WATER CYCLE Rain falls on the earth surface in filtrates (soaks int...

Topic

The Dynamic-Earth And Consequence

THEORIES THEORY OF ISOSTASY Denudation has been going on the continents where to...

Position Behaviours And Structure Of The Earth

GLOBE Is the model of the earth Earth Is ball of rock partly covered by wat...

Photograph interpretation

Photograph are the true image pictures showing truly appearance of the earth’s...

Maps and map interpretation

What is a map? Map is a scaled conventional representation of the whole or any o...

Simple survey and mapping

INTRODUCTION TO SURVEYING Surveying is an art or a science of measuring and reco...

Field research techniques

Definitions of Research – Research is the systematic investigation into a...

Application of statistics in geography

STATISTICS Statistics is a branch that deals with every aspect of the data. Stat...

Chat Icon Close Icon