Nafasi Mpya za kazi Jeshi la Uhamiaji November 2024 | Nafasi Mpya za Ajira Uhamiaji 2024/2025

Nafasi Mpya za kazi Jeshi la Uhamiaji November 2024

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kanuni Namba 11(1) ya Kanuni za Uendeshaji za Uhamiaji za Mwaka 2018, ametangaza rasmi nafasi mpya za ajira za Askari wa Uhamiaji kwa vijana wa Kitanzania. Tangazo hili linatoa fursa ya kipekee kwa vijana wenye sifa zinazostahili kujiunga na Idara ya Uhamiaji, mojawapo ya taasisi muhimu za usalama na huduma nchini Tanzania.

Nafasi Mpya za kazi Jeshi la Uhamiaji November 2024Nafasi Mpya za kazi Jeshi la Uhamiaji November 2024

Sifa za Waombaji

Ili kuomba nafasi hizi, waombaji wanapaswa kutimiza vigezo vifuatavyo:

Ili kuwa na nafasi ya kuajiriwa, mwombaji lazima atimize sifa maalum zilizowekwa na Idara ya Uhamiaji. Hapa ni baadhi ya sifa muhimu ambazo kila mwombaji lazima awe nazo:

  1. Raia wa Tanzania: Mwombaji lazima awe raia wa Tanzania bila shaka yoyote.
  2. Elimu: Mwombaji anayetaka kuomba ajira hizi anapaswa kuwa na elimu inayohitajika kulingana na nafasi anayotaka. Kwa mfano:
    • Kidato cha Nne: Umri kati ya miaka 18 hadi 22.
    • Kidato cha Sita na Stashahada: Umri kati ya miaka 18 hadi 25.
    • Shahada/Stashahada ya Juu: Umri kati ya miaka 18 hadi 30.
  3. Uwezo wa Kimwili na Kiakili: Mwombaji lazima awe na siha njema ya mwili na akili, bila matatizo ya afya yanayoweza kuathiri utendaji kazi.
  4. Uongozi na Taaluma: Kwa maombi yaliyopangwa kuwa na kipaumbele, ujuzi maalum kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali kama vile fani za lugha, sheria, takwimu, na uhasibu zitakuwa na faida kubwa.
  5. Utu na Tabia: Mwombaji hatakiwi kuwa na rekodi yoyote ya kihalifu, au kuwa na alama za tatoo mwilini.

Kipaumbele cha Maombi

Maombi yatakayopewa kipaumbele ni ya waombaji wenye taaluma katika fani mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:

  • Lugha za kimataifa
  • Utawala
  • Sheria
  • Uhasibu
  • TEHAMA
  • Ufundi wa magari na umeme
  • Usimamizi wa ununuzi na ugavi
  • Cyber Security
  • Masijala na Ukatibu mahsusi

Jinsi ya Kutuma Maombi Nafasi Mpya za kazi Jeshi la Uhamiaji November 2024

Waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia tovuti rasmi ya Idara ya Uhamiaji (immigration.go.tz) kuanzia tarehe 29 Novemba, 2024 hadi 13 Disemba, 2024. Nyaraka zifuatazo zinapaswa kuambatishwa kwa mfumo wa PDF (zisiwe na ukubwa zaidi ya 300KB):

  • Picha ya pasipoti ya hivi karibuni.
  • Barua ya maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono.
  • Barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia.
  • Vyeti vya kitaaluma vilivyohakikiwa.
  • Wasifu wa Mwombaji (CV).

Bofya hapa Kutuma Maombi

Wakati wa kufanya Maombi, Mwombaji anatakiwa kuambatisha (upload) kwenye mfumo wa Ajira nyaraka zilizo katika mfumo wa PDF na picha ya mwombaji (passportsize) katika mfumo wa jpg/png na kila Nyaraka moja isizidi ukubwa wa 300Kb.

Orodha ya nyaraka hizo ni kama ifuatavyo;

  1. Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa
  2. Awe na namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kwa ajili ya kujisajili kwenye mfumo.
  3. Barua ya maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono.
  4. Barua ya Utambulisho toka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia; kwa walio Makambini JKT/JKU wawe na barua za Utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Kambi.
  5. Picha (passport size) ya hivi karibuni iliyo katika mfumo wa jpg/png na isiyozidi 300kb
  6. Awe na namba (index no) ya cheti cha Kidato cha Nne na Sita kwa waliohitimu kidato hicho ambapo atajaza namba hizo kwenye mfumo wa ajira.
  7. Nakala ya vyeti vya kuhitimu fani mbalimbali ngazi ya Astashahada, Stashahada, na Shahada/Stashahada ya Juu (kama anavyo na viwe
    vimehakikiwa katika vyuo husika).
  8. Nakala ya cheti cha kuhitimu JKT/JKU(kwa walionavyo).
  9. Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili wa Bodi
  10. Wasifu wa Mwombaji (CV)

Tahadhari Muhimu

  • Maombi yatakayofikishwa nje ya mfumo uliotangazwa hayatazingatiwa.
  • Waombaji wanaotumia nyaraka za kughushi watachukuliwa hatua kali za kisheria.
  • Waombaji wanatahadharishwa dhidi ya matapeli wanaodai kutoa ajira kwa malipo ya aina yoyote.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina Ya Walioitwa Kazini Utumishi Na Ajira Portal 30 November 2024
  2. Nafasi Mpya za Kazi Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Novemba 2024
  3. Nafasi 3 za Kazi ya Dereva Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi | Mwisho 06 November 2024
  4. Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira za Walimu 2024 MDAs & LGAs
  5. Majina Ya Walimu Walioitwa Kwenye Usaili 2024
  6. Nafasi Za Kazi Baraza La Mitihani Tanzania NECTA – October 2024
  7. Nafasi 10 Za Kazi Msaidizi Maendeleo Ya Jamii Halmashauri Ya Wilaya Ya Kyela



Related Post

Nafasi Ya Kazi :- Process & Recoveries E

Job type: Full-timeJob PurposeImplementing wo...

Nafasi Ya Kazi :- Head Of ICT At SOS Children

SOS Children’s Villages Vacancy Announcement...

Nafasi Ya Kazi :-  T24 Application And Digit

Job Description: T24 Application and Digital C...

Leave a Comment


Translation And Interpretation | English Form 5 & 6

Translation is a process by which ideas that are written in one language ar...

Writing Skills | English Form 5 & 6

Are the abilities that allow you to write effectively and concisely. A competent...

Reading Skills | English Form 5 & 6

Reading is the process of going through written information or piece of wor...

Speaking Skills | English Form 5 & 6

What is Speaking? SPEAKING SKILLS: Speaking is simply the act of talking wh...

Listening Skills | English Form 5 & 6

Listening is ability to accurately receive and interpret messages in the communi...

Word Formation | English Form 5 & 6

This is the field or branch of morphology which studies different principles or ...

Introduction To Language | English Form 5 & 6

Language is a symbol system based on pure or arbitrary  conventions…...

Topic

Form Five and Form Six

Ecology

Ecology is the study of the interactions between living things, such as humans, ...

Evolution

EVOLUTION Evolution is  a change in the genetic composition of a population...

Genetics

Genetics is the study of heredity and variationHeredity- is the passage of chara...

Chat Icon Close Icon